MOROGORO: Adaiwa kumuua mkewe na kumtupa mtoni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia, mkazi wa kijiji cha Mamvisi Gairo kwa tuhuma za kumuua mke wake kwa kumpiga ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo chake.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema lilitokea Mei 22 mwaka huu saa 1.00 asubuhi katika kijiji cha Mamvisi, Wilayani Gairo.

Matei amesema baada ya kufanya mauaji hayo mtuhumiwa aliutupa mwili wa marehemu huyo kwenye mto Chumvi uliopo Gairo kwa lengo la kupoteza ushahidi.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya marehemu kumuomba mtuhumiwa fedha za kumpeleka mtoto wao hospitali kufuatia maradhi aliyokuwa akiugua.
 
Eehh Mungu wangu,huruma kwa huyo mtoto maana bado mgonjwa na mama ameshakufa
Dahhh
 
Sheria ifuate mkondo wake na adhabu kali ili ajifunze...Watu sijui kwa nini wanakosa utu...kama alikuwa hana hiyo pesa kulikuwa na haja gani ya kumpiga mwanamke wa watu?? Inahuzunisha..Mungu ampumzishe salama huyo Mwanamke
 
Back
Top Bottom