MORE PRESSURE, ANOTHER SERIOUS DEMAND; Ziko wapi silaha za Daudi Mwangosi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MORE PRESSURE, ANOTHER SERIOUS DEMAND; Ziko wapi silaha za Daudi Mwangosi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Sep 11, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wakuu

  Labda leo naweza kuendelea kuandika tena kama namna yangu ya kumuenzi Daudi Mwangosi. Maana kama ni kumuaga, kwa kweli nimekataa kumuaga. Nikimuaga, nitakuwa namumwaga. Sina sababu ya kumumwaga Mwangosi. Si mtu wa kumwagwa. Nimekataa kama ambavyo nimekuwa nikikataa kuwaaga wapiganaji wengi wa namna yake.

  Kwani maisha ni nini? Maisha si mwili pekee. Wala maisha si kiwiliwili hiki kinachotembea. Ni zaidi ya hayo. Wapiganaji wa namna ya Mwangosi niliyekuwa nikimfahamu, huendelea kuishi hata baada ya miili yao kutoweka duniani. Ukisoma kale kakitabu kadogo lakini kazuri, Intellectual Versatility, hii inaelezwa kama moja ya sifa za wanazuoni. Kuishi baada ya mwili kufa. Natumaini wengi mnajua hili.

  Leo nitaweza kuendelea kuandika kumuenzi, kwa sababu moja ya vitu vilivyokuwa vikinisumbua kabisa kichwani tangu siku ile baada ya mauaji ya mpiganaji Daudi, ilikuwa ni namna ambavyo waandishi wa habari na UMMA WA WATANZANIA, 'tulipuuza' moja ya masuala ya muhimu kabisa ambayo tulipaswa kuwa tumewa-task Jeshi la Polisi na serikali kwa ujumla, kutekeleza. Ni kuhusu vitendea kazi vya Daudi. Silaha zake muhimu, kamera na kompyuta. Viko wapi vitu hivi?

  Mapema sana nikingali Iringa, nikichangia hapa jukwaani, niliuliza swali hili hili nikitumia maneno ya Kiingereza. Niliuliza wamevichukua kwa sababu gani? Viko wapi? Wanavifanyia nini? Naona wengi tulipitwa. Bado hatukuona umuhimu wake.

  Nashukuru sana leo swali hili limepata nafasi ya kusikika dunia nzima kupitia maandamano ya wanahabari. Limehojiwa pale Jangwani (ingawa kwa kuchelewa, maana ni dhahiri halikuwa likikumbukwa).

  Nimemsikia mpiganaji Malembeka katika maandamano makubwa pale Iringa, akipaza sauti kubwa sana kuifahamisha dunia juu ya vifaa hivyo kuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi, huku akihoji kwa nini hawataki kuvitoa! Tunawataka polisi watoe vifaa hivyo vya Daudi, kamera na kompyuta. Namshukuru sana Malemebka kuwa amekumbuka kile ambacho tulikuwa tukijadili naye, siku moja ama mbili, baada ya mauaji yale yaliyofanywa na Jeshi la Polisi.

  Labda watu hawaelewei kwa nini. Si ajabu ndiyo maana hata katika press conferences mbili ambazo nimehudhuria, hasa katika presentations za still pictures and moving pictures za matukio ya siku hiyo ya mauaji pale Nyololo, (Iringa na Dar es Salaam), pamoja na suala hilo la kamera na kompyuta kusisitizwa sana kuwa viko wapi, wanahabari waliohudhuria hawakuona kama ni suala muhimu.

  Wakati akikutwa na mauaji yale ya kikatili, Daudi alikuwa yuko kazini. Alikuwa akichukua habari. Ukiangalia picha kama tatu hivi, zipo mbili zinamuonesha akiwa katika mapambano yake ya mwisho hapa duniani. Akipigania uhai. Amemkumbatia yule askari Mwampamba amuokoe kwenye mikono ya israili.

  Unaweza kuona kamera iko mikononi mwake. Upande wa kuchukulia ukiwa umefunguliwa. Ameishikilia imara. Ndiyo maana alilalama kwa ujasiri "msiniue msiniue...niko kazini." Ima fa ima na kamera yake mikononi. Israili hawakumsikiliza. Mmoja akafanya kazi aliyoagizwa kufanya. Akamlipua Daudi. Akamsambaratisha na kukatisha uhai wa mpiganaji yule!

  Sasa waweza kuona namna ambavyo Daudi alikufa akiwa kazini. Kamera yake ilikuwa kazini. Ilikuwa ikiendelea kuchukua habari. Ilikuwa ikirekodi. Hata kama katika hatua za mwisho sana za uhai wa Daudi hakuweza kurekodi kwa uzuri picha kadri alivyotaka, lakini kamera yake iliendelea kuwa kazini, ikimfanyia kazi ya kurekodi sauti yeye kutaka. Wakati yeye anapigania uhai, kamera yake ilikuwa ikimpigania 'apate' ushahidi. Iko wapi hiyo kamera?

  Katika moja ya zile picha ambazo inahitaji ujasiri mkubwa kuziangalia mara mbili ili uweze kutambua kuwa ule ni mwili wa binadamu, pembeni kabisa mwa mkono wa kushoto wa Daudi (kulia kwako mtazamaji), unaweza kuona kitu fulani kikubwa, cheusi. Hilo ni begi la kompyuta (Laptop) ya Daudi! Nayo iko wapi?

  Ukiendelea mbele kidogo, hapa utahitajika kuhoji mpaka notebook na kalamu za Daudi ziko wapi. Hizi ni silaha za mwandishi. Ziko wapi silaha za mpiganaji yule. Kama askari wanavyohoji silaha za wenzao wakiuwawa vitani, nasi tunahoji silaha za mwenzetu! Wamezichukua za nini? Wamezifanyia nini? Wameziweka wapi? Kwa nini...kwa nini...kwa nini!

  Kwa ujasiri wake, uwezo wake na kuipenda kazi yake, kamera ile ilikuwa imechukua matukio ya muhimu sana kwa siku ile. Hasa baada ya polisi kuwa wameanzisha vurugu, wakaharibu mali za raia, wakapiga na kukamata watu waliokuwa wakifanya shughuli za chama chao pale kwenye Ofisi ya Kata ya CHADEMA, Nyololo.

  Daudi alikuwa akichukua matukio kwa ukaribu sana. Maana tangu mapema, alikuwa ameikamia kweli kweli ile stori. Haki yake na wajibu wake.

  Kama havina chochote cha maana, kwa nini waendelee kubaki navyo.

  Sasa tunahoji, ziko wapi hizo silaha za Daudi?
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Makeni asante sana kwa kuendelea kuuliza hili. Polisi wana kesi nyingi sana za kujibu haka. Natamani waandishi wangekuwa wamechukua tukio la askari akibeba vile vitu. Mungu amlaze mahali pema peponi Daudi.
   
 3. Josephine

  Josephine Verified User

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wanahabari wote,
  natamani kama mngefikiria namna ya kuishitaki jamhuri kwa kukiuka sheria na mkataba ya uwandishi.ikumbukwe sheria zimetungwa na serikali na kupitishwa na bunge,Mara moja mara mbili nimemsikia Raisi Dhaifu duniani akizungumzia uhuru wa vyombo vya habari,kauli zake zinaweza kusimama kama vidhibiti vya waandishi kudhulumiwa haki yenu.
  Nachelea kusema bado misimamo yenu haiko bayana,nimesikia mkitoa siku 40 ni siku nyingi sana.mlipaswa kutotoa taarifa zote za serikali hata kwa wiki nzima mfulilizo,kushinikizwa wahusika kujiuzuru.
   
 4. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Ni kweli. Uko sahihi. Kuna jambo halijakaa sawa katika matamko yaliyotolewa leo. Who is the real enemy! Inavyoanza kuelekea wanahabari tunaweza kutegeka kwa kuamini kuwa yule askari aliyevuta na kulipua ndiye adui mkubwa, that won't be correct.

  Siku 40! Wakati kuna baadhi ya wananchi commoners tu or laymen wamehoji busara ya Waziri Nchimbi kutoa siku 30 kwa kamati yake (ya kitchen party?) kufanya uchunguzi. Kuna wahariri wamehoji busara hiyo pia. Kuna wahariri ambao wamekwenda mbali hata kuhoji busara ya kuhitaji uchunguzi wa namna ya Nchimbi kwenye suala lililo wazi.

  Lakini pia kutambua uchunguzi, tena unaofanywa na kamati aliyounda Nchimbi ni kuanza kujipiga ngwala. Ukitaka kujua uhalisia huo, angalia hadidu za rejea ilizopewa hiyo kamati, kisha angalia uhalisia wa tukio la kuuwawa kwa Daudi na mwenendo mzima wa utendaji kazi na uwajibikaji wa Jeshi la Polisi nchini na serikali kwa ujumla kwa umma wa Watanzania!
   
 5. Rumishaeli

  Rumishaeli JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 225
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi nina hisi yule askari aliemkumbatia kabla ya mauti kumkuta alikua anafahamu fika nini kilikua kiaenda kumtokea. Katika hali ya kawaida si rahisi sana askari kufanya jambo kama lile wakati walishaanzisha vurugu, Nafikiri ni muhimu kumhoji zaidi hata kama alikua anamfahamu
   
 6. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mwema,Kagonji,RPC Kamuhanda,Nchimbi ni fedheha kwa waajiri wake kama wamebakiwa na fedheha.Mzizi wa tatizo ni Amiri Jeshi Mkuu wa watu hawa maana hao ndiyo vetting zote zilipoishia kupata majembe ya kazi!
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu hongera kwa kufikiria kiundani zaidi juu ya hilo. Yule askari aliyedhaniwa kumsaidia Mwangosi hasa ndiye aliyemuanda kabla ya kupigwa bomu kwa namna ambavyo walivyokua wamepanga.

  Si kawaida askari wa FFU katika mazingira kama ile eti kwenda kinyume na amri ya Kamuhanda.

   
 8. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kamanda wa Polisi wala hakuwa wa kujiuzulu alitakiwa awajibishwe. Jeshi la polisi limeoza. Bahati mbaya CDM inawapa wakati mgumu watoa maamuzi wanachowaza na kupanga ni kuithibiti CDM tu.
   
 9. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Ure forcing me to have a 2nd thought on the particular action. Unajua tangu siku ile nimejitahidi sana kuilazimisha akili yangu kuelewa 'the highest level of disoder' iliyokuwa ikionekana kwa baadhi ya askari waliokuwa katika operesheni hiyo!

  Nimeilazimisha kweli kweli nielewe kwamba polisi walipewa order na mkubwa wao, lakini eti hawakumsikiliza na bado mtu mwenye cheo cha PC aka-defy order ya OCS, akafyatua na kumlipua mtu, labda hatimaye akili yangu ingelazimika kukubali, lakini nahisi hoja yako hii inanilazimisha kufikiria upya. Ngoja...
   
 10. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Kuna Watanzania wanaogopa kudai serious actions katika tukio hilo ambalo kwa ukweli ni mfululizo tu wa matukio mengi ya namna hiyo. Watu wanakufa mikononi/wanauwawa na vyombo vya dola big time but the business goes as usual.

  Sasa wengine wanafikiri haliwahusu, they are wrong. Tunatakiwa kudai very serious actions, hasa kwa top brass katika suala hili, kudai serious reformations kwenye Jeshi la Polisi. Kudai masuala ya msingi, tena yanayohusu haki na mstakabali wa taifa, haikufanyi uwe mwanachama wa chama cha siasa. Watu wanazunguka zunguka tu mbuyu...
   
 11. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Tunataka kujua utumbo wa Mwangosi uliopelekwa MR Hotel uko wapi?
   
 13. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180

  Mkuu Wakati ndiyo sasa, pole. Naona Mwananchi wamei-pick hii kitu kwenye stories zao za leo Jumatano juu ya maandamano ya waandishi. Jana ilikuwa Itv wakati wakitoa story ya maandamano ya Iringa. Bado issue hii haijapata attention ya kutosha. More pressure, silaha za Daudi ziko wapi. Hata notebook na kalamu. Nani hajui unaweza kunote vitu muhimu na kutunza huko?
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kilichoniuma sana ni kuona jinsi alivyopelekwa mahakamani!
  Huyo askari G2573 Simon ambaye ndo alimlipua inaonekana kabisa mhusika siyo yeye!
  Haiwezekani mtuhumiwa wa kesi ya kuua kwa makusudi akapelekwa kwa gari ya kifahari namna ile, badala ya karandinga kama wafungwa wengine, akiwa chini ya ulinzi mkali wa makusudi ili waandishi wa habari wasichukue picha yake!
  Pumbavu zao Jeshi la polisi, pumbavu zake Kamuhanda aliyeagizwa kuamrisha mauaji ya mpiganaji!
  Tutamkumbuka Daudi Mwangosi kuliko hata Steven Biko, Ken Saro Wiwa, Ernesto Che Guevara nk.
  Inasikitisha kuona mtuhumiwa amepelekwa mahakamani kwa mauaji ya kukusudia, halafu bado kuna tume inateketeza kodi zetu kwa makusudi! Nchimbi alijua kilichokuwa kinakwenda kufanyika hata kabla ya mauaji, inasikitisha anaunda tume za kishenzi kuteketeza kodi zetu!

  Their days are numbered!
   
 15. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #15
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Mungi, alisema Shafi Adam Shafi kwenye Kuli, "Yana mwisho haya."
   
 16. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Mungi, alisema Shafi Adam Shafi kwenye Kuli, "Yana mwisho haya."
   
Loading...