Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Mara kadhaa tumezungumzia kuhusu umuhimu wa ‘moral authority’ na tukasema hii ni jambo la msingi sana kwa kiongozi au chama chochote pengine kuliko mambo mengine yote. Mada hii inaendelea kufafanua umuhimu wa jambo hili na linavyofanya kazi kwa namna chanya au hasi.
Wakati, Mzee Kikwete akiwa Rais, alikuwa akisisitiza mara kwa mara kuhusu kufuata taratibu na sheria zilizokuwepo wakati wake na kutotumia madaraka nje ya sheria. Pia alipenda uhuru wa watu, ushirikishwaji, ushirikiano miongoni mwa vyama, maridhiano n.k.
Kutokana na tabia yake hivyo (ambayo lengo la uzi huu si kujadili kama ilikuwa hasi au chanya), Mnyika ambaye kwa sasa ni katibu mkuu wa CHADEMA, alitangaza hadharani kwamba mzee Kikwete alikuwa ni “Dhaifu”.
Hoja ilikuwa ni kwa nini Mzee Kikwete hakuwa anatumia mamlaka yake kama Rais kusukuma maamuzi kwenye mambo mbali mbali ama iwe kwa mujibu wa sheria au nje ya sheria; kinyume chake anasema ‘sheria na taratibu zifuatwe’. Kauli hiyo ya Mnyika haikuwahi kukanushwa na yeye mwenyewe au chama chake.
Sasa basi, ikiwa Mnyika na chama chake bado wanaamini kwamba hiyo ilikuwa ni sahihi, ‘It is ok’ lakini kama hawaamini hivyo; sioni ni kwa nini wasijitokeze hadharani na kumuomba msamaha mzee Kikwete?
Lakini kwa upande mwingine, kama bado wanaamini kwamba hiyo ilikuwa ni kweli na sahihi kabisa; hakuna sababu ya kutojitokeza hadharani na kumuunga mkono Mh. Rais Magufuli kwa kuwa sasa anaonekana anatekeleza hoja nyingi za akina Mnyika wa zama za Mzee Kikwete.
Mtu anaweza kujiuliza ni nini hiki? Maana yake nini? Ili iwe nini? Kwa faida ya nani? n.k. Hii ni muhimu sana kwa sababu zifuatazo;-
Kwanza msingi mkuu wa uongozi ni fikra; ni kipi unaamini ni kizuri na kipi unaamini ni kibaya na unaowaongoza wakuelewe hivyo. Kama utakuwa hueleweki unaamini kipi kizuri na kipi kibaya, unapoteza ‘moral authority’ na ukiongea kitu kabla ya watu kuangalia uzuri wake au ubaya wake; watafikiria kwanza unapata wapi ‘moral authority’ ya kusema unachosema?
Nitoe mfano, Shekhe au Mchungaji, ni lazima kwanza aeleweke anaamini pombe ni nzuri au ni mbaya. Kama wakati flani anasema pombe mbaya, wakati fulani anasema nzuri, kama anasema mbaya kwa mfano halafu watu wakiacha anawapinga anataka wanywe, wakianza kunywa tena anasema mbaya waache; watu hawatawaza ubaya au uzuri wa pombe kwanza bali watawaza kwanza shekhe au mchungaji huyo anapata wapi ‘Moral authority’ ya kuwaeleza uzuri au ubaya wa pombe?
Pili, kama ni vizuri pale viongozi wa CCM wanapokosea wakakubali na kukiri kisha kujisahihisha; kwa nini pia ninyi msione umuhimu wa kukubali na kukiri hadharani pale mnapokosea ili kujenga ‘precedence’?
Tatu, ili watu wenye utulivu wa akili wakuchukulie serious, ni lazima waelewe na wajiridhishe; unaamini nini na huamini nini, unaunga mkono nini na huungi mkono nini, na wewe unafanya nini ili iwe nini.
Kama hayo hayako wazi, maana yake hata muelekeo wa taasisi unayoongoza utakuwa haueleweki na hautabiriki “Uncertain” na hapo kinachofuata ni “Total failure”, na ni vigumu mtu kuku/kuwaamini kwenye jambo lolote, na usipoaminika ‘then what is there?'
Nne, ni vizuri kujifunza kutokana na matukio, na katika hili kuona umuhimu wa; kwanza kujiridhisha kabla ya kusema au kufanya jambo kama kweli unaamini juu ya unachosema au kufanya na pili, ikiwa unashauri au kukosoa mtu mwingine; kutumia lugha ambayo baadae haitakuhukumu.
Hili ni muhimu katika kuhakikisha kwamba hujutii maamuzi yako kesho na kesho kutwa.
Sasa najua kuna watu watakuja hapa kuuliza kwa nini haya usiwaambie CCM, ni sawa tu maana kila mtu na kichwa chake.
Mwisho, ni ukweli pekee unaoweza kuwa na manufaa ya muda mrefu, hata hivyo huu ni ushauri tu.