Moon Jae In: Vitu 10 kumhusu rais wa Korea Kusini

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
522
1,000
Habari zenu wakuu. Kwa wale wapenzi wa Korean dramas huyu ndiye Rais wa Korea.

Jina lake ni Moon Jae In. Alipata urais mwaka 2017 baada Park Geun Hye kuponzwa na rafiki yake Soon Sil hivyo kuondolewa madarakani.

15 . Moon alizaliwa mwaka wa vita. Alizaliwa 1953 miezi michache baada ya korean war kuisha.

14 Wazazi wa Moon wametokea North Korea na waliingia South Korea kama wakimbizi.

13. Moon amezaliwa kwenye maisha ya kifukara. Ilifikia hatua kipindi akawa anategemea unga wa mahindi na maziwa ya unga kama msaada kutoka Kanisa Catholic.

12. Moon alianza harakati mwaka 1969, akiwa na miaka 16 tu. Rais Park alikuwa anataka abadilishe katiba hivyo Moon Jae akiwa bado mtoto aliungana na waandamanaji wengine kupinga jambo hilo.

11. Amesoma Kyung Nam High School shule iliyoanzishwa mwaka 1942 (ipo mpaka sasa) na shule hiyo hiyo ndio alisoma Kim Young Sam ambaye pia alikuwa ni Rais wa Korea Kusini.

10. Alishawahi kuzimia akiwa kwenye maandamano baada ya kupigwa na bomu la machozi.

9. Moon amebobea kwenye sheria na kwenye miaka 1980 alikuwa ni campaign manager wa mgombea urais Roh Moo Hyun, japo hakushinda.

8.Mwaka 1988 alikuwa ni mmojawapo wa waanzilishi wa Gazeti la HANKYOON gazeti ambalo kati ya mwaka 2015 na 2016 linatajwa kuwa ndio chombo cha habari kinachoaminika zaidi South Korea kuliko chombo kingine chochote cha habari.

7. Alishawahi kufungwa gerezani pale Seodaemun Detention Centre baada ya kushiriki kwenye maandamano.

6. Moon ana watoto wawili, wa kike na wa kiume.

5. Alikutana na mkewe akiwa chuoni Kyung Hee University mwaka 1974 walioana miaka 7 baadae 1981

4. Moon pia amepishana mwaka mmoja na mkewe. Moon amezaliwa January 24 1953 huku mkewe Kim Jung Sook alizaliwa November 15 1954.

3.Kabla ya kuwa Rais, Moon alishawahi kuwa Senior Presidential Secretary ambapo alikuwa ni mshauri wa Roh Moo Hyun katika urais wake.

2. Moon na mkewe Kim wanapenda wanyama especially Pets. Wana jumla mbwa na paka wanne

1. Moon ni Mkatoliki. Ni Rais wa tatu wa Korea kuwa mkatoliki baada ya Kim Dar Jung na Roh Moon Hyun.

moon_jae_in_photo_kim_min_hee_pool_getty_images_675839706_500x500.jpg
 

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
6,587
2,000
Alifanyiwa nin mpaka akacheua bila kupenda!!??
Ilikua wanafanya biashara na Iran, Marekani ikawaambia ishikilie hela zake ili itekeleze vikwazo ilivyoekewa na marekani, Iran ilidai hela yake jamaa wakabana hawatoi, ilipita miaka kimya kingi, juzi jeshi la wanamaji la Iran likaiteka meli lao la mafuta iliokua ikitokea Saudia, jamaa wakapiga kelele iachiliwe, Iran ikasema achia hela zetu tukuachilie meli lenu, huku marekani akapiga kelele meli liachiwe maramoja akaambiwa stay away katika huu mgogoro haukuhusu, mwisho wa siku Iran ikalipwa hela zake zote na meli likaachiliwa
 

Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
1,809
2,000
Ilikua wanafanya biashara na Iran, Marekani ikawaambia ishikilie hela zake ili itekeleze vikwazo ilivyoekewa na marekani, Iran ilidai hela yake jamaa wakabana hawatoi, ilipita miaka kimya kingi, juzi jeshi la wanamaji la Iran likaiteka meli lao la mafuta iliokua ikitokea Saudia, jamaa wakapiga kelele iachiliwe, Iran ikasema achia hela zetu tukuachilie meli lenu, huku marekani akapiga kelele meli liachiwe maramoja akaambiwa stay away katika huu mgogoro haukuhusu, mwisho wa siku Iran ikalipwa hela zake zote na meli likaachiliwa
Iran walikua sahih kwa sabab bila kufanya hivyo wasingefanikiwa lkn hata wamagharib wanatumiaga njia hii kushinikiza kulipwa kwa kutumia kigezo cha zuio kutoka mahkama zao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom