Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

MAGUFULI, MGUFULI, MAGUFULI!!!!!!!!
kweli barabara zilijengwa, lakini mnafahamu nyumba yake ambayo yeye alijiuzia, kabla hajajiuzia alifanya nini, yani kweli waTanzania sijui tunakoelekea. Alijenga kitu kipya kikali ndani ya huo uwanja, kwa fedha za serikali baadae akajikabidhi kiulaini kwa hela zetu ambazo zingesaidia wanaokaa chini wakisoma. Na kulikuwa kuna mvutano kati yake na Gray Mgonja alipomkatalia kuchukua nyuma (ambayo nayo ilileta kashfa kwa gharama alzonununua nilisikia kama alianza lipa gharama za juu alizoficha). Mgonja alipokataliwa kununua nyumba, akainama kama Kobe, simnajua mafisadi, hata uje na hoja gani wanakuja na jambo jipya. Akamwambia Magufuli kuwa Waziri ni cheo cha kisiasa, hivyo hatakiwi naye kupata nyumba kwa sababu wanaohitajika ni wafanyakazi wa serikali. Basi katika mvutano Magufuli akaridhia kumkatia naye pande lake Mgonja. Ila kwa nini Magufuli alikuwa anamkatalia Mgonja, ni stori nyingine tofauti.

Hivyo munaomtetea Magufuli, ni sawa na Mvi zilizopakwa rangi nyeusi. Huyu bwana naye hafai, na ni mtu wa kulalamika kila kona kuwa anaonewa. Ukiwa ndani ya CCM, wa njia moja ama nyingine utakuwa FISADI, angalia hela walizokuwa wanagaiwa kila mgombea Ubunge zilitoka wapi?

Yani nachoka kabisa hata kufikiri......
 
Mkuu Gembe,

Rais amkabidhi kijana mwingine hiyo nafasi. Haya mambo ya kung'ang'ania na watu wale wale ambao pamoja na kwamba ni nafuu kuliko wengine lakini hakuna la maana kubwa walilolifanya, mimi naona ni kama kupiga mark time hnapo hapo.

Tuiwe tayari kuwajaribu watu wapya ili waje na mawazo mapya ya kuijenga nchi yetu.

Najua JK amewapa vijana nafasi nyingi, hilo ni jambo jema. Inabidi aendelee, pamoja na kwamba kuna wengine wameharibu, lakini watakuja kizazi kipya ambacho kinataka maendeleo na kipo tayari kuchakarika.

Challenge ya 2010 ni kwa vijana wanaotaka maendeleo, kuamua kufanya kweli na kuwa tayari kuchukua uongozi wa nchi kwenye sehemu mbalimbali. Naamini wana JF wengi tu wanaweza wakafanya mengi mazuri kuliko viongozi wengi tu tulio nao sasa.

Yes Am in 2010..ule mkakati wa CHADME umefikia wapi??
 
Mi naona hakuna haja ya kuiziba nafasi ya chenge, iachwe waiz tu kwa sababu nadhani atakayekuja na yeye atatoka miongoni mwao ambamo nimebaini kuwa hawataleta mabadiliko yoyote.

Naungana na wazo lako moja kwa moja..Hiyo wizara ikae wazi mpaka mtu mpya safi na mwenye sifa muafaka apatikane ndio aapishwe..sio hawa hawa ambao wengi wao ndio walioidhinisha uuzwaji wa property lukuki za sirikali..tumeishachelewa mengi hivyo hatuna haja ya kukurupuka katika hili...
 
mawazo mengine bwana!! mambo kama ya kubaki wazi ni jambo ambalo haliwezekani hata nyie mnajua..cha msingi tujadili nani anafaa kama mnaona magufuri hafai (mtazamo wenu) basi mseme nani anafaa
 
Kama JK anataka kuonyesha ubabe wake basi amrudishe Magufuli katika hiyo wizara,lakini kimsingi ni kwamba kwa hali ilivyo tete juu ya nyumba za serikali Magufuli hafai kupewa wizara hiyo na kama itawezekana wangemuondoa hata katika baraza la mawaziri.

Magufuli asipewe hiyo wizara kwa sababu aliishauri vibaya serikali ktk mpango wa kuuziana nyumba za serikali,halafu alimuuzia mdogo wake ambae mimi nimemaliza nae pale mlimani na hakua mtumishi wa serikali.Hii ni kashfa ambayo ambayo kwa nchi zilizokomaa kisiasa asingepewa hata ubunge.
 
Mimi nafikiri JK amteue kijana mmoja anaitwa Msalalilo Kakwami Bhunoge yuko pale majita A ili awe mbunge kisha amteue kuwa waziri wa miundombinu.Huyu kijana mimi namjua kwa muda mrefu uwa anaziba barabara pale kijijini mvua ikizibomoa kwa kutumia jembe lake.Ni msafi kabisa kwani kwa umri wake sijawahi kusikia hata anasingiziwa kuwa na gurl friend pale kijijini achilia mbali kuwa anatumwa mara kwa mara dukani kununua vitu na kurudisha chenji inavyotakiwa.

Sasa nyie waungwana hapa kila mtu anaetajwa amekuwa mbaya kwenu.Kulaumu tuuuuuu,mkiombwa ushahihi mnaanza mara RAV4 mara geology mara walewale wa awamu ya Ben,.

Nambieni nani aliwahi kufanya kazi wizara ya ujenzi kama magufuri toka nchi hii imepata uhuru.Nani alithubutu kugusa barabara za Mwanza-Dar.Nani alijua Singida kutakuwa na Lami hata siku moja.Si mlikuwa na kina Kiula.Acheni hizo.

Kwani maamuzi ya kuuza nyumba za serikali yalikuwa ya serikali au ya Wizara??Mbona hivyo???
Na wewe unae umia JPM kuwa watoto kwa huyo mnaemwita wa mabibo hostel nyie mlitaka azae na nani.
My take:-
Magufuri Pombe John ndie pekee kwa sasa anaefaa kuongoza wizara hiyo.
Ndo yale yale ya Nyamagana.Pombe kaondoka tuu Nyamagana yetu hiyoo.
 
Mpango wa Waziri Magufuli wanasa wavuvi haramu wa kimataifa

*Walikuwa na tani 70 za samaki
*Wapelekwa rumande
*Rais Kikwete ashangilia

Festo Polea na Leon Bahati

MIKAKATI ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Pombe Magufuli, kudhibiti maliasili za baharini imeanza kuonyesha makali baada ya kunasa meli iliyokuwa imebeba tani 70 za samaki waliovuliwa eneo la Tanzania kwenye pwani ya Bahari ya Hindi.

Waziri Magufuli, ambaye alipata umaarufu mkubwa wakati akitekeleza mipango ya serikali akiwa Waziri wa Miundombinu, aliagiza wafanyakazi 35 wa meli hiyo ya Tawariq I kuwekwa mahabusu wakati taratibu nyingine za kisheria zikifanywa.

“Leo nina furaha kwa kuwa maharamia hawa watalala katika jela yetu na hivyo kujua kuwa Tanzania inachukia wizi wa samaki na haina mchezo katika hilo,” Magufuli alisema akionyesha kufurahia mafanikio hayo baada ya kuhaha muda mrefu kutafuta dawa ya wezi wa maliasili za baharini.

“Walikuwa wakifanya uvuvi eneo la Tanzania kama vile ni shamba la bibi. Sasa nawafahamisha shamba la bibi halipo tena; bibi amekufa; hawa ni watoto wa bibi. Leo (jana) lazima wakalale (gerezani) Keko.”

Alisema kuwa kukamatwa kwa watu hao ni jambo la kujivunia kwa sababu kwa miaka 50 iliyopita, maharamia wamekuwa wakivua samaki kwenye pwani ya Tanzania bila kikwazo chochote, lakini akasema sasa Tanzania imeandika historia katika ramani ya kimataifa.

Alisema wanatarajia kuwafikisha mahakamani wakati wowote na kuwashtaki kwa mujibu wa sheria. Iwapo mahakama itabaini kuwa watu hao wana hatia, wanaweza kutozwa faini ya dola 20 milioni za Kimarekani au meli yao kutaifishwa ama adhabu zote kwa pamoja, kwa mujibu wa Magufuli.

Meli hiyo, ambayo ilikamatwa juzi ikiwa karibu maili 60 kutoka ufukweni, ilifikishwa Bandari ya Dar es salaam jana asubuhi.

Ilikuwa haina bendera ya nchi inakotoka na wafanyakazi wake hawakuwa na leseni wala vitambulisho na hadi jana lugha waliyokuwa wanatumia ilikuwa haieleweki.

Magufuli alisema kuwa meli iliyokamatwa haijulikani ni ya nchi gani, lakini mmoja wa vibarua wa meli hiyo aliiambia Mwananchi kuwa inamilikiwa na kampuni moja ya Taiwan, ingawa ubavuni imeandikwa Vietnam.

Mfanyakazi huyo wa meli hiyo alisema kuwa mmiliki wa kampuni hiyo ni raia wa Tawain ambaye muda mwingi huutumia nchini Kenya.

Waziri Magufuli alisema kabla hawajawekwa rumande, walitakiwa kuchomwa sindano za kinga kama ilivyo sheria ya kimataifa ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na kwamba, kati ya mabaharia 35 ni wanne tu ambao walikuwa wamepata chanjo hiyo, jambo alilosema litawafanya wawe na uangalifu mkubwa.

Kemn Govender, mkurugenzi msaidizi wa meli ya Sarah Baartman iliyokodishwa kwa ajili ya kusaka wavuvi haramu kwenye pwani ya Tanzania, alisema maharamia hao waligoma kujisalimisha hadi walipotishiwa kuwa zitatumika silaha za moto.

Govender alisema meli hiyo ilionekana juzi mchana ikiwa umbali wa maili 60 kwenye eneo la Tanzania na ndipo walipoanza kuwasiliana kwa njia ya simu, lakini hawakupata majibu yoyote kutoka kwenye meli hiyo.

“Tulipoitaka ijisalimishe, hatukupata majibu yoyote na walikuwa wamezima rada hadi tulipotaka kutumia mtutu na vyombo vya moto kukabiliana nao ndipo walipoamua kujisalimisha,” alisema Govender.

Govender alisema baada ya kufanya uchunguzi, walibaini tani 70 za samaki aina ya tuna ambao kwa kilo huuzwa kati ya Dola 8 na 10 za Kimarekani (sawa na takriban Sh13,100 za Kitanzania).

Alisema meli hiyo haina kibali wala leseni yoyote ya uvuvi na haikuwa na kitu chochote kinachoipa haki ya kufanya uvuvi na kwamba meli hiyo ilizima rada zake.

Operesheni ya kukamata meli zinazofanya uvuvi haramu kwenye pwani ya Tanzania inaendeshwa na meli ya Sarah Baartman.

Tangu kuanza zoezi la kusaka meli zinazofanya uharamia huo Februari 25, kumekuwepo na mafanikio makubwa baada ya meli nne kukamatwa. Tayari meli 31 zimeshakaguliwa na meli hiyo ya juzi ni ya kwanza kukamatwa nchini Tanzania.

Naye mmoja wa Wakenya wanaofanya kazi kwenye meli hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Juma Kombo, alisema meli hiyo imekuwa ikifanya uvuvi eneo la Tanzania kwa zaidi ya miezi sita iliyopita.

Alisema meli hiyo ni maalumu kwa ajili ya uvuvi na kwamba kila baada ya siku kadhaa, meli nyingine hufika kubeba samaki wanaovuliwa na kuondoka nao, huku meli hiyo ikiendelea na kazi ya kuvua.

Akiwa na wenzake wengine wawili, Ally Ally Mkota na Sitta Walikoni kutoka maeneo ya Likon na Kisauni mjini Mombasa, alisema walichukuliwa na meli hiyo kwa muda wa miezi sita na hulipwa dola 200 kwa mwezi.

“Sisi tunafanya kazi meli hii ilituchukua tukavue na ukiangalia ugumu wa maisha na shida ya ajira tukaingia kwenye kazi ya uvuvi. Kama wana kibali ama hawana sisi hatujui tunachotafuta ni fedha. Wanatufanyisha kazi ya uvuvi na kutulipa kiwango ambacho kinaturidhisha,” alisema Kombo.

“Meli zipo zaidi ya hii ingawa ni ajabu kukamatwa kwani meli nyingi hazifiki eneo tulilokuwepo kwa sababu ni vigumu kufikika kutokana na eneo hilo kuwa la maficho sana.

"Lakini kwa kuwa meli hiyo iliyotukamata ni kubwa, waliweza kutuona na kutufikia kirahisi. Meli bado zipo nyingi wakienda tena na tena watakamata nyingine zaidi.”

Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete ameishukuru Afrika Kusini, na mabaharia wote waliofanikisha kukamatwa kwa meli kubwa iliyokuwa inavua samaki wa Tanzania kinyume cha sheria.

Meli hiyo inayoitwa Tawariq I ilikamatwa jana katika operesheni maalum iliyoshirikisha mabaharia kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji na Kenya.

Meli hiyo ilikamatwa katika siku ya pili ya operesheni maalum iliyoanzishwa na Tanzania kukomesha wizi wa samaki katika eneo lake la Bahari ya Hindi.

Tanzania, Kenya na Msumbiji zimetoa mabaharia wawili kila moja wakati Afrika Kusini imetoa mabahari watano.

Rais Kikwete alitoa shukurani hizo jana wakati alipokutana na mabaharia waliofanikisha kukamatwa kwa meli hiyo kubwa na akawakabidhi zawadi mbalimbali mabaharia hao.
 
hivi ni mpango wa maghufuli, au ni mpango wa serikali za msumbiji, afrika kusini na tanzania kupambana na uvuvi haramu wa kimataifa? manake hapa anonekana ni waziri machachari , askari wa mwavuli amefanya mambo yake! ni vema watanzania tukaacha siasa za kujisifu na majigambo kwa mambo ambayo sisi hatukuyabuni.

angalizo-huenda akili yetu inageuzwa kutoka richmond, dowans, epa, na kagoda kumshabikia askari mwavuli maghufuli kwa mambo ambayo yamebuniwa ni south afrika baada ya kuona soko lao la samaki linadorora baada ya kuzidiwa na wataiwani na wakenya, ohooo!!!!!!, NCHI YA WASANII
 
Yes yamebuniwa na nchi za SADC...na yeye katekeleza....hivyo kupongezwa ni haki yake jamani........
 
Nimemsikia akijisifu kuwa mpango wake ambao ni wa aina yake, hauna mfano kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita, tena kwa jinsi anvyoongea anasema utalinifaisha taifa kuliko madini.

Yaani tuaache kufuatilia wezi wa madini yanayochotwa mchana kutwa tujiona, tukavizie meli za kichina zikiiba samaki ambao nadhani hata kuwavua hatuwezi.

Ni ukweli tu hakuna meli itakayokuja tena kuiba samaki wetu, baada ya mwenzao kukmatwa, nini baada ya hapo? Je tutaanza kuwavua? Au tutaendelea kuwa korokoni wa kuvizia meli zitakazovunja sheria tuzizikokote mpaka magogoni pale, na kudai fidia ya 20,000,000,000.

Ninatamani tuwe na vitu endelevu na siyo uwongo uwongo wa kuwadanganya watanzania kuwa sasa mtakuwa matajiri kuliko utajiri wa madini kwa kuwa tunakamata wezi wa mali zenu na sasa mtazifaidi, wakati hamna hata meli za kuvuna hao samaki
 
Huu ni mwanzo mzuri sana, lakini kumbe meli iliyokamata maharamia hao imekodishwa!!{ kwa mujibu wa habari hii}. imekodishwa kwa kiasi gani? kwa muda gani ? Ni mwanzo mzuri sana, [ hongera kwa mkuu Magufuli } lakini kwa historia ya nchi yetu na mikataba tunayoingia unaweza kukuta faini zote zinazotolewa zikaishia kwa tuliokodisha meli za ulinzi na sisi kubaki na gharama za kulisha mabaharia hao Keko.
 
siku zote magufuli amekuwa akifanya kazi nzuri lazima apongezwe. Hata ile kashfa ya nyumba za serikali ilishinikizwa na mkapa na sumaye na yeye akaona achukue japo nyumba moja.
 
Ni kweli na mimi nadhani gharama za kukodi meli ya doria lazima uangaliwe isije ikawa faini zote zina ishia kwa mwenye meli tuliyoikodi. Lakini siku zote Magufuli yuko makini pale anapokuwa na nafasi, na ni mbunifu sana.
 
Hivi mpango ulianza baada ya Magufuli kuwa waziri wa wizara hii? Tuache kutoa credit zisizo na uhakika. Huu mpango ulianza tangia enzi za Mzee MKAPA wakati magufuli hayuko wizara hiyo. Ni sasa tu tunaanza 'kuonyeshwa" matunda yake....

omarilyas
 
Wadau lazima tukubaliane tatizo lenu ni nini? Kama tunawakamata watu wasivue, maana yake sisi hatuvui kabisa, maana kama tungekuwa tunavua tungekuwa tunakutana nao daily huko baharini...

Kuna taarifa kuwa wanaokamatwa bado ni Dagaa tu!!! Meli zenyewe hata kukamatwa hazikamatwi, mambo huishia juu kwa juu...Hawa wa-taiwan walikuwa hawana kitu...wangekuwa na kitu ohh....mambo zamani yashakwisha!!!

back kwa wale wadau hio Meli imekodishwa kiasi gani? Ina maana hata pwani yetu kuilinda hatuwezi? hadi tupate wasaidizi...magufuli come up clean iweje hadi leo hatuna Mabaharia? hadi tutoe mabaharia 2, wakat SA wametoa 5..kwa miaka 50 umeweza kutoa mabaharia 2?...Au ndio masharti ya Mwekezaji SA ili asupport lazima watu 5 waaajiririwe? nyie mnashindwa hata kufikiri kuwa watanzania wenzenu wanahitaji ajira hizohizo?...Vijana wetu wanabakia kuwa madeck Boy, Ma-Oiler tu...

Lipo wapi Jeshi letu la Baharini...? Limeshindwa? au 60Km hawawezi kufika? wanacholinda nini wakati Adui akiwepo 60Km hawana vifaa vya vya kumuona wala kumfuata...?

.... Magufuli Jisifie kwa wananchi wazembe....Hatuna Muda wa kutoa Thanks Hovyo....Tueleze kwanini bei ya samaki hadi sasa bado Ghali? wakati Bahari tunayo kuanzia Mtwara hadi Tanga...
 
Nampa big UP Waziri Magufuli.... ana hekaheka sana tokea akiwa pale mlimani....Wakurugenzi wizarani walikuwa hawahemi kuhusu performance za ujenzi wa barabara za mikoani...sasa anahamia baharini, Na tuone zao la samaki linaongezeka sasa.

Nimekaa nikafikiria kwa upande mwingine wa shilingi......Roho itasuuzika sana nikiona mheshimiwa Rais akipeana mikono kwa "job well done" na watuwatakaowaburuza na kuwaegesha pale "magogoni" wezi wa rasilimali zetu za taifa.
 
Hamna lolote ni kutaka kuonyesha kuna maendeleo si mnafaamu kuwa tunaelekea kwenye uchaguzi ,sasa unaenda kutoa zawadi jamani hawa watu wanafanya kazi na kulipwa ,hiyo ni kazi yao sasa zawadi hapa zimehusu nini ? Na hatujui meli hiyo imekodishwa kwa kiasi gani kwa mwezi ? Hivi mnahoji ,tuna jeshi la majini nini kazi ya Jeshi hili ? Nasema jeshi sio meli na mabaharia hapana JESHI LA MAJINI na ukienda pale bandarini utaziona boti za nguvu za kijeshi hivi nini kazi ya wanamaji hawa ?

Tunawalipa au wanalipwa kwa ajili ya kulinda mipaka ya Nchi na kwa vile wao ni Jeshi walikuwa lazima wawe na patrol kulinda mipaka yetu ya Bahari ?

Magufuli na Raisi Kikwete hawaoni kama wanaliweka JESHI letu la Majini katika matatizo makubwa ?

Hiyo meli iliyokamatwa ni aibu kusema jeshi letu haliwezi kuikamata ? Nasema ni aibu tena kubwa ? Pale bandarini zipo frigate ambazo ni very powerfull.Au ndio wanatumia kusafirishia mikungu ya ndizi kutoka Pemba.

Ajabu watu wanapongeza ,ulizeni meli inalipwa kiasi gani ,kwa mwezi fedha ambazo wajeshi wetu wangeweza kulipwa na kuifanya kazi kwa bidii ya kulinda nchi yao.

133100.jpg
 
Magufuli pongezi zikufikie.Ni mwanzo mzuri na kaza mwendo ,tutafika.Nadhani bie ya samaki ni Ghali kutokana na MAHARAMIA KUIBA SAMAKI WETU.Kwa hiyo mwanzo huu utaleta unafuu kwa siku zijazo na tutapata samaki wengi na kwa bei nafuu.Naamini mpango huu una maana kubwa ya kudhibiti Maharamia ili sisi wa tanzania tuweze kuvua samaki hao.Kama si maana hii basi bora tuwaache maharamia hao waendelee kuvua na kutunisha mifuko yao
 
Hii issue bado inahitaji ufafanuzi kidogo....., i do not mean to take anything from our ever creative Magufuli, lakini kwa nini hawajatumia jeshi la TZ? hiyo meli ni kweli imekodishwa ? kwa kiasi gani? kwa muda gani?Tenda ilitangazwa? au tumeomba msaada wa muda tu kutoka South Africa? Kuna tutakaosema watu haturidhiki hata mazuri tunahoji. Lakini mtu aliyeumwa na nyoka, akiona unyasi lazima ashtuke. Mikataba mingine bado inatumaliza, ndiyo maana maswali mengi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom