yawezekana hali na wakati ukawa umempita lakini yawezekana pia alikuwa mjanja kuuwahi wakati so in 1995 alikuwa before time na sasa yuko on time watazamaji wantazama off time. hii inanipa shaka kama kweli forum hii ina members ambao ni critical thinkers au critical thingers au critical singers?Jana Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro na mbunge wa Iringa mjini kaweka wazi nia yake ya kutetea jimbo lake, Mama huyu ambaye hakubaliki sana kwenye jimbo lake kiasi cha watu kuamini kuwa hupita kiccm jana ametangaza kuwa anagombea tena.
Akiongea kwa kujisifu eti kuwa ukuu wa mkoa alioupata ndio mafanikio na ni kitu cha kujivunia kwa wananchi wa Iringa kwa kuwa wao kumchagua kwake kumemfanya aonekane na rais na kupewa nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa. amerbainisha msimamo wake jana kwenye mkutano ulioandaliwa na taasisi ya ISICO kati yake na wnanchi.
kupita kiccm maana yake ni kupitishwa na chama kuwa mbunge na siyo kuchaguliwa na wananchi, yaani hupita kwa kuibiwa kura ok!Mkuu hebu fafanua hapo kupita KICCM ndiyo kupitaje? na je hii ina athari gani kwa wananchi wasiomkubali?. Maana hapa tuelewane mapema kuwa njia yoyote isiyo ya kuchaguliwa kihalali na wananchi ni CRIMINAL act which needs to be stoped. Tulisihalalishe misamiati ya uvunjaji wa sheria, siku wananchi wakichoka patakuwa hapatoshi
hata kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa huyu mama alikuwa ni mgumu mno kukutana na wananchi wake, kwa kweli ukuwajiwa uchumi wa iringa ni wa kasi hivyo unahitaji wabunge waliochangamka wanaoweza kuwatetea wananchi na kuhakikisha maendeleo ya kweli yanapatikana kama alivyo mheshimiwa lukuvi ambaye anawajibika mno kwa wananchi wake na wananchi wanaziona juhudi zake ila siyo huyu mama jamani!Falesy,
Kwamba alikuwa viti maalumu kisha akaamua kugombea jimboni hiyo siyo issue,tatizo letu hapa ni uwezo wake wa kudeliver kama mwakilishi wa watu wa Manispaa ya Iringa,hapa hatusemei ushabiki au tumetumwa na watu fulani.
Binafsi sina tatizo na Mama Mbega,tatizo langu ni majukumu aliyonayo,yamekuwa mengi kiasi kwamba yamekuwa mzigo kwake.Manispaa ya iringa inahitaji mtu mwenye uwezo wa kushughulikia changamoto zinazolikabili jimbo,na mtu huyo anahitaji kuwa na muda wa kutosha wa kukutana na wananchi,kujadiliana nao jinsi ya kutatua matatizo mbalimbali nk.Sasa mtu yupo Kilimanjaro atasikiliza matatizo yetu saa ngapi?
kwa hiyo bwana falesy unataka useme kwa vile ni kinamama tukae kimya hata kama hawawajibiki? kisa haki sawa ndo tunyamaze? irirnga inahitaji mtu wa kuleta maendeleo awe wa kiume au wa kike lakini siyo mtu wa kujali tumbo lakenimeona kuna kila juhudi za kuwahimiza wanawake kugombea kupitia majimbo badala ya viti maalum sasa sijui walio na nia ya kugombea na ambao ni tayari wapo wanapigwa vijembe sasa sijui ni kina nani hao wahimizwa.
;
hatuna maana kuwa apige kelele bungeni ila tuna maanisha awajibike wananchi kwa kusaidia kuibua miradi kama tunavyojua miradi haiwezi kutekelezwa kama mbunge haitetei sawasawa.mfano kama Lukuvi anavyopigania ujenzi wa barabara ya iringa dodoma, yaani kama yeye akinyamaza kimya itachukua mda selikali kutekeleza, hinyo ndivyo huyu mama anatakiwa aweKupiga kelele sana bungeni haina maana kuwa Mbunge ni mzuri. Kinachotakiwa ni kufuatilia kero za wapiga kura wake ni kuwapa mlisho nyuma wa jinsi mambo yanavyokwenda au yanavyotatilowa!!!!! Porojo nyingi hazimsaidii mpiga kura!!!!