Monica Ngenzi Mbega atangaza rasmi kutetea kiti chake cha ubunge

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,960
2,464
Jana Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro na mbunge wa Iringa mjini kaweka wazi nia yake ya kutetea jimbo lake, Mama huyu ambaye hakubaliki sana kwenye jimbo lake kiasi cha watu kuamini kuwa hupita kiccm jana ametangaza kuwa anagombea tena.
Akiongea kwa kujisifu eti kuwa ukuu wa mkoa alioupata ndio mafanikio na ni kitu cha kujivunia kwa wananchi wa Iringa kwa kuwa wao kumchagua kwake kumemfanya aonekane na rais na kupewa nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa. amerbainisha msimamo wake jana kwenye mkutano ulioandaliwa na taasisi ya ISICO kati yake na wnanchi.
 
Afadhali amenikumbusha huyu ndio top katika list yangu ya wabunge ambao asilani sitaki wakanyage mjengoni!
 
wanyalukolo naombeni data zake naona tu mmemponda sana!mie nipo kutali na mtazamo wangu ulikuwa tofauti yaani nilimwamini na kuona mchapa kazi sana!na nimekuwa nikimsikia kama mkuu wa mkoa kilimanjaro!plz tunaomba explanation zaidi juu ya utendaji wake!na mtazamo wa wananchi je asilimia ngapi watamtosa na ngapi wanamkubali!
 
Anatimiza haki yake, na wapiga kura nao watimize haki yao kama atapitishwa katika kura ya maoni ya chama chake (CCM). Hongera sana kuweka wazi.
 
Mama huyu ambaye hakubaliki sana kwenye jimbo lake kiasi cha watu kuamini kuwa hupita kiccm

Mkuu hebu fafanua hapo kupita KICCM ndiyo kupitaje? na je hii ina athari gani kwa wananchi wasiomkubali?. Maana hapa tuelewane mapema kuwa njia yoyote isiyo ya kuchaguliwa kihalali na wananchi ni CRIMINAL act which needs to be stoped. Tulisihalalishe misamiati ya uvunjaji wa sheria, siku wananchi wakichoka patakuwa hapatoshi
 
Jana Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro na mbunge wa Iringa mjini kaweka wazi nia yake ya kutetea jimbo lake, Mama huyu ambaye hakubaliki sana kwenye jimbo lake kiasi cha watu kuamini kuwa hupita kiccm jana ametangaza kuwa anagombea tena.
Akiongea kwa kujisifu eti kuwa ukuu wa mkoa alioupata ndio mafanikio na ni kitu cha kujivunia kwa wananchi wa Iringa kwa kuwa wao kumchagua kwake kumemfanya aonekane na rais na kupewa nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa. amerbainisha msimamo wake jana kwenye mkutano ulioandaliwa na taasisi ya ISICO kati yake na wnanchi.

hakubaliki vipi? au ndiyo kampeni zimeanza?
hii ni unfair judgement, labda kama ungekuja na kautafiti na ukatoa statistics hapa. otherwise sie wengine tunaona umetumwa na umelipwa kufanya hivyo
 
Jana Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro na mbunge wa Iringa mjini kaweka wazi nia yake ya kutetea jimbo lake, Mama huyu ambaye hakubaliki sana kwenye jimbo lake kiasi cha watu kuamini kuwa hupita kiccm jana ametangaza kuwa anagombea tena.
Akiongea kwa kujisifu eti kuwa ukuu wa mkoa alioupata ndio mafanikio na ni kitu cha kujivunia kwa wananchi wa Iringa kwa kuwa wao kumchagua kwake kumemfanya aonekane na rais na kupewa nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa. amerbainisha msimamo wake jana kwenye mkutano ulioandaliwa na taasisi ya ISICO kati yake na wnanchi.
siasa za bongo bana,huku mkuu wa mkoa kilimanjaro,huku mbunge wa iringa mjini,yaani hata haieleweki,mmh nimemkumbuka kajaajaa hivi kibantu haswa,na ni mama wa kimjinimjini,kubebwa muhimu hata ningekua mimi ningempendelea potelea karibu.
 
Mnyikungu tunashukuru sana kwa taarifa,..ukweli huyu Mama Mbega anatakiwa kupumzika sasa,maana sijaona michango yake bungeni ambayo ina reflect maendeleo ya manispaa ya Iringa,mie sielewi ni kwa nini pia mtu apewe ukuu wa mkoa wakati huohuo ni mwakilishi wa wananchi,tena ni mikoa miwili tofauti kabisa(kusini na kaskazini),atasikiliza saa ngapi matatizo ya wananchi anaowawakilisha,...Nene mbifile sana,wi dada mukwe,...ye tufwe tufwale suruali.
 
siasa za bongo bana,huku mkuu wa mkoa kilimanjaro,huku mbunge wa iringa mjini,yaani hata haieleweki,mmh nimemkumbuka kajaajaa hivi kibantu haswa,na ni mama wa kimjinimjini,kubebwa muhimu hata ningekua mimi ningempendelea potelea karibu.

Aaah, wapi. Mbona ka-portable kwa sana wala hana shepu ya kibantubantu.
 
Kamwene wanyalukolo,Mosi,kimsingi mimi binafsi nakubaliana na hoja ya sisi kama wapigakura tunahitaji mbunge msemaji bungeni ,hatuhitaji wawakilishi wanaokwenda kulala mjengoni,Pili,toka tumemchagua Mhe-Mbega sijawahi kumsikia hata kuchekesha tu bunge maana inawezekana hana hoja zamsingi zinazowasumbua wapiga kura wake lakini hata kuongolea namna gani jimbo lake linapambania kama si kuondoa maambukizi ya ukimwi basi hata kupunguza wapi kimya,Tatu nadhani kama kazi kishapata ya ukuu wamkoa aliache jimbo lipate mwakilishi anaetoka Iringa mjini anaeishi kila siku pale anaezifahamu nakizielewa shida na kero za wanairinga .nawaambia wanyalukoro "mlampela muhuma kudasi inyi"imekuwa kawaida ya wapita njia kujifanya wanauchungu na maisha yenu kumbe wanataka kupatia daraja tu.
Hongera Mhe Mbega kuwa RC Tuachie jimbo letu tumpate mgombeamwenye mapenzi ya kweli ya kuwatetea wanyaluu.Mwisho Serikali inapaswa kuangalia kama wananchi ambao ndio wapiga kura wanapompa madaraka mtu ni vyema akachwa awatumikie hao wapigakura wake na si kumpa madaraka mengine yanayomfanya ahame jimboni kwake na kuwa mbali na wapiga kura wake.Labda serikali ituambie hakuna watu waliona uwezo zaidi ya wabunge basi tufunge vyuo vya Uongozi na Utawala kama IDM na vyuo vingine kwani havina maana.ili kupata ufanisi bora ifike mahala Professional zichikuwe nafasi yake.
 
Hana maadili alifanya madudu alipokuwa waziri pale hazina yaliyosababisha kuondolewa kwake!!!
 
Am i missing something? Ni Mkuu wa Mkoa na ni mbunge at the same time, kwanini avae kofia mbili kwa wakati mmoja? What is so speacial with her? How does he serve Kilimajaro Region na Iringa constituent?

Kama alivurunda Wizara ya Fedha why alipewa u RC, si alikuwa wa kuwekwa kapuni? au quality ya kuwa portable ime-play part.
 
Wajuvi wa siasa za Iringa!! nilipata kusikia tetesi za mtoto wa Assas kugombea iringa mjini, kulikoni?
 
Simpendi huyu mama kutokana na tabia yake ya kujisikia na kujishaua eti kisa mbunge na hapo hapo mkuu wa mkoa, halafu analalamikiwa kwa kujaa ubinafsi, machoni kama mtu lakini ana roho mbaya kweli!ASHINDWE!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom