Elections 2010 Monica Mbega Ameondoa hadi Mapazia Ofisi ya Mbunge wa Chadema

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Vitendo vya wabunge wa CCM kuhamisha samani na vitu vingine kwenye ofisi za wabunge majimboni,jana liliibukia Iringa mjini ambako mbunge mpya kwa tiketi ya chama cha Chadema,Peter Msigwa kukuta ofisi imeondolewa kila kitu pamoja na kung'olewa kwa mapazia! Duh hii kali CHUKUA CHAKO MAPEMA:target:
 
Kabla ya hukumu, nadhani tungefahamishwa kama kunao mwongozo wowote unaosimamia vifaa vya ofisi za umma . Kama hakuna basi hilo ni ombwe linaloweza kupelekea kwa wahusika kufanya kufuatana na matashi yao. Mtu anaweza kuweka samani na vifaa ofisi za umma na hatimaye kuviondoa. Ungekuwepo mwongozo nadhani ungetusaidia yafuatayo:
1. Kuzuia kuingiza na kutoa vifaa kiholela - mtu angeambiwa huwezi kuweka vifaa vyake binafsi kwenye ofisi za umma, labda itokee kuwa anafadhili na hapa ingekuwa ni sharti uviache utakapoondoka.

2. Kiongozi asingeruhusiwa kufanya ofisi ya umma kama mali yake, au kuwa kama mpangaji anayeingia na vitu vyake na kuondoka navyo upangaji" unapokoma.

Viongozi hawa wameonyesha mfano mbaya sana kwa jamii hata kama kweli hivyo vitu ni vyao.
 
Vitendo vya wabunge wa CCM kuhamisha samani na vitu vingine kwenye ofisi za wabunge majimboni,jana liliibukia Iringa mjini ambako mbunge mpya kwa tiketi ya chama cha Chadema,Peter Msigwa kukuta ofisi imeondolewa kila kitu pamoja na kung'olewa kwa mapazia! Duh hii kali CHUKUA CHAKO MAPEMA:target:
Mkuu hebu rekebisha heading,ni mbunge wa Ìringa mjini na si wa chadema.
 
Hawa Wabunge wa CCM vipi mbona kila wakipigika wanaleta mambo ya Kishamba. Monica ni mke wa Kibopa, alikuwa waziri (naibu), Mbunge, baado ni Mkuu wa Mkoa, sasa nini kudeal na petty things like this??? AIBU
 
Wengi tunakawaida ya kupendezesha ofisi kwa kutumia fedha zetu. Maana ukitegemea fedha za serikali ofisi itakuwa kituko. Sasa inawezekana huyo mama alinunua mapazia yake kwa milioni 2 halafu ayaache tu. Kama ni ya serikali hilo ni jingine.
 
Waacheni wachukue, those are are minor stuff. Basically tumeshajua tulikkuwa tunaongozwa na watu wa aina gani. Nitashangaa waiba mapazia na vitasa kama watapewa nafasi tena
 
Jamani Monica Mbega kwani alikuwa Mbunge? Inakuwaje amiliki Ofisi ya Mbunge? AU ukiwa Mkuu wa Mkoa ndiyo kila kitu??
 
Back
Top Bottom