Monica Mbega Ameondoa hadi Mapazia Ofisi ya Mbunge wa Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Monica Mbega Ameondoa hadi Mapazia Ofisi ya Mbunge wa Chadema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ndallo, Dec 3, 2010.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Vitendo vya wabunge wa CCM kuhamisha samani na vitu vingine kwenye ofisi za wabunge majimboni,jana liliibukia Iringa mjini ambako mbunge mpya kwa tiketi ya chama cha Chadema,Peter Msigwa kukuta ofisi imeondolewa kila kitu pamoja na kung'olewa kwa mapazia! Duh hii kali CHUKUA CHAKO MAPEMA:target:
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kabla ya hukumu, nadhani tungefahamishwa kama kunao mwongozo wowote unaosimamia vifaa vya ofisi za umma . Kama hakuna basi hilo ni ombwe linaloweza kupelekea kwa wahusika kufanya kufuatana na matashi yao. Mtu anaweza kuweka samani na vifaa ofisi za umma na hatimaye kuviondoa. Ungekuwepo mwongozo nadhani ungetusaidia yafuatayo:
  1. Kuzuia kuingiza na kutoa vifaa kiholela - mtu angeambiwa huwezi kuweka vifaa vyake binafsi kwenye ofisi za umma, labda itokee kuwa anafadhili na hapa ingekuwa ni sharti uviache utakapoondoka.

  2. Kiongozi asingeruhusiwa kufanya ofisi ya umma kama mali yake, au kuwa kama mpangaji anayeingia na vitu vyake na kuondoka navyo upangaji" unapokoma.

  Viongozi hawa wameonyesha mfano mbaya sana kwa jamii hata kama kweli hivyo vitu ni vyao.
   
 3. B

  BA-MUSHKA Member

  #3
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilimsikia mara kadhaa mikutanoni akisema ofisi ni yake, sintashangaa kitu akitoa bati.
   
 4. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu hebu rekebisha heading,ni mbunge wa ĂŚringa mjini na si wa chadema.
   
 5. N

  Newvision JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa Wabunge wa CCM vipi mbona kila wakipigika wanaleta mambo ya Kishamba. Monica ni mke wa Kibopa, alikuwa waziri (naibu), Mbunge, baado ni Mkuu wa Mkoa, sasa nini kudeal na petty things like this??? AIBU
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mbona hii ni kawaida jamani,mwashangaa nini?
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,592
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Labda Kwenu!
   
 8. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wengi tunakawaida ya kupendezesha ofisi kwa kutumia fedha zetu. Maana ukitegemea fedha za serikali ofisi itakuwa kituko. Sasa inawezekana huyo mama alinunua mapazia yake kwa milioni 2 halafu ayaache tu. Kama ni ya serikali hilo ni jingine.
   
 9. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Waacheni wachukue, those are are minor stuff. Basically tumeshajua tulikkuwa tunaongozwa na watu wa aina gani. Nitashangaa waiba mapazia na vitasa kama watapewa nafasi tena
   
 10. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  kawaida! wewe utakuwa fisadi bure!
   
 11. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2010
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Jamani Monica Mbega kwani alikuwa Mbunge? Inakuwaje amiliki Ofisi ya Mbunge? AU ukiwa Mkuu wa Mkoa ndiyo kila kitu??
   
Loading...