gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Kwa maneno yake mwenyewe mh mkuu wa mkoa wa Mwanza(Mongela) ametambua mchango mkubwa uliofanywa na bodaboda mmoja kuwapa taarifa police haraka baada ya kumpakia jambazi na kumshusha mahali huko mwanza.
Taarifa za bodaboda huyu zilizaa matunda kwani jambazi huyu alifanikiwa kuuawa na police.
Kimsingi haitoshi kutoa pongezi za mdomo pekee kwani huyu bodaboda kwakutoa taarifa ame risk maisha yake na hata sasa bado pia anahitaji walau kuhakikishiwa usalama wake kwani ni rahisi kukatokea hata ulipizwaji wa kisasi.
Ni vizuri mh Mongela angeiga mfano uliooneshwa na mkuu wa mkoa wa Dar Mh paul makonda kwakumzawadia huyo bodaboda hii itaongeza hamasa kwa wengine.
Lazima tukubali bodaboda hawa kama watakua wakipewa motisha kwenye haya mambo ya ujambazi itasaidia sana kufanikisha kukomesha ujambazi kwani hawa wapo kila mahali na mara nyingi hua hata wakitumika kuwabeba hawa majambazi kutoka sehem moja kwenda nyingine.