Monduli: Matairi ya gari ya mbunge wa Viti maalum Anna Giderya(CHADEMA) yamepigwa risasi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Yanayoendelea kwenye uchaguzi wa Jimbo la Monduli jijini Arusha yanasikitisha pamoja na nguvu kubwa imetumika na Jeshi la Polisi kuzuiwa mawakala wa upinzani kuingia kwenye chumba cha kupiga kura .
Muda Gari ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara, Mhe.Anna Gidarya imeshambuliwa kwa kupigwa risasi kwenye matairi muda mfupi uliopita akiwa katika kata ya Majengo watu wanaodaiwa ni Jeshi la Polisi.
Mbunge huyo amesema kitendo hicho kimetokea leo Jumapili, tarehe 16 Septemba 2018.
Amesema kuwa tukio hilo limetokea kata ya Majengo wilaya ya Monduli mkoani Arusha akiwa anasimamia uchaguzi wa ubunge wa jimbo hilo unaofanyika leo
1.jpg
.
 
Huyu mtu sijiu ni kwanini bado anaendelea kupewa heshima zote anazopewa.

Hata hapa JF watu wakiandiaka manene makali kumuhusu wacheni watu wamseme na sio kumlindalinda mradi tu hawavunji sheria wala kumtukana mtu.

Wahariri wa vyombo vya habari ni wakati wa nyinyi pia kuacha kumpamba katika media zenu.

Tukiendelea kumpa promo, kujifanya hatuoni na kumlindalinda hakika tutakuja kuona matokeo yake.

Huyu mtu ama ni mgonjwa wa akili au ni hana element za ubinadamu kabisa.

Kila mtu anapaswa kumuona ni adui kwani ameshaonyesha sifa zote za kutostahili kuungwa mkono kwa kauli na matendo yake.
.
In short, huyu ni mtu hatari sana na hana urafiki na mtu siku yoyote anaweza kukugeuka mradi tu mmepishana katika jambo fulani.

Wenzetu mnaodhani mko safe au kufikiri haya hayawahusu, mjue tu mnajidanganya na ipo siku kwa pamoja mtakiri kuwa mlichelewa kumkataa.
 
tena huko. kuna morani? iweje. mlie nyie tu? kwa nini nao walie? unaonyeshaje ustarabu kwa mtu asiyemstarabu? kwa tume hii upinzani mtapata tabu sana. huko hakuna magari ya wabunge wa ccm?
 
Huyu mtu sijiu ni kwanini bado anaendelea kupewa heshima zote anazopewa.

Hata hapa JF watu wakiandiaka manene makali kumuhusu wacheni watu wamseme na sio kumlindanda.

Wahariri wa vyombo vya habari ni wakati wa nyinyi pia kuacha kumpa nafasi katika media zenu.

Tukiendelea kumpa promo na kumlindalinda hakika tutakuja kuona matokeo yake.

Huyu mtu ama ni mgonjwa wa akili au ni hana element za ubinadamu kabisa.

Kila mtu anapaswa kumuona ni adui kwani ameshaonyesha sifa zote za kutostahili kuungwa mkono kwa kauli na matendo yake.
.
In short, huyu ni mtu hatari sana na hana urafiki na mtu siku yoyote anaweza kukugeuka mradi tu mmepishana katika jambo fulani.
Tofauti ya huyu na Idd Amin Dada ni ipi?
 
Ukishasema kuwa Watu ' wanaodaiwa ' kuwa ni Polisi tayari unakosa uhalali wote wa kuelekeza ' Shutuma ' huko unakodhani ndiyo wamehusika. Na hata kama ni kweli hilo tukio limefanywa na Jeshi la Polisi basi nina uhakika wa 100% kutokana na ' Ueledi ' wao kuna ' ukaidi ' fulani walifanyiwa na wenye hilo Gari hivyo na Wao wakawa wanatekeleza wajibu Wao kwa mujibu wa Viapo vyao.

Siku zingine tuache kukimbilia ' Kulaumu ' pale tulipoangukia ila pia tuwe tunajiuliza ' tumejikwaa ' wapi. Ni kweli huwa kuna ' madhaifu ' fulani kwa Jeshi letu la Polisi ila nashukuru kwamba kidogo kidogo kwa sasa wanaanza kuyafanyia Kazi ila nimegundua baadhi yetu tumeshaathiriwa na ' Labeling Theory ' kwa Jeshi letu la Polisi nchini Tanzania. Hebu tuwaacheni wafanye Kazi zao / Majukumu yao na kama Wewe hutaki ' bughudha ' zao basi tenda / fanya mambo yako katika misingi ya Sheria za nchi.

Halafu ni kwanini lawama zenu dhidi ya Jeshi la Polisi huwa mnaziibua / mnazileta tu wakati wa ' Chaguzi ' ila Jeshi la Polisi hili hili likifanya mambo mema kwa ajili ya Ulinzi, Usalama na Amani yetu ya Tanzania huwa hatujitokezi kuwapa Pongezi / Kongole zao? Watanzania baadhi yetu tuache huu ' Unafiki ' na kamwe hizi Siasa zetu zisitufanye tukaanza kuwadharau hata wale ambao ndiyo wanatufanya Mimi na Wewe tutembee hivi Vifua wazi huku tukiifurahia hii amani yetu japo kuna ambao kwa Upopoma / Upumbavu wao tu wanaidhihaki.
 
Mkuu kukabithi nchi kwa washamba,wale wa madaraka na vichaa madhara yake ndo haya wameona kwa haki hawawezi kutoboa wanatumia Jeshi la Polisi kufanya kila aina uhuni sasa inahuzunisha sana sasa watanzania bila kujali imani za itikadi zao wanatakiwa kumpinga huyu kichaa

Back
Top Bottom