Mombasa Republican Council - kikundi kinachotaka kuwa nchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mombasa Republican Council - kikundi kinachotaka kuwa nchi!

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Nzi, Apr 17, 2012.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  Kundi la Mombasa linalotaka kujitenga na kuwa nchi kamili.
  Tayari kundi lina rais na baraza la mawaziri ambao wapo tayari kuendesha hiyo "nchi" yao. Kundi hili limekuwa na ajenda ya kujitenga na kutengeneza jamhuri ya Mombasa toka mwaka 1999!
  Wanadai wamekuwa chini ya utawala wa Kenya,utawala ambao umewasahau na hauwatendei haki.

  Baadhi ya viongozi wa dini zote, wakristo na waislamu huko Mombasa wanaonekana kuliunga mkono kundi hilo. Ingawa serikali ya Kenya imeliita kundi hilo ni haramu,tena ni la kuogopwa zaidi ya Al-Shaabab.

  Nasikia harufu ya udini mkali sana hapa. Kwani walio kwenye harakati hizi wengi ni waislamu. Na sasa hali imekuwa mbaya kwa kundi hili kuonekana kuwa TISHIO zaidi ya Al-Shaabab!
  Mh! Yangu macho.
  Source: Citizen-Nipashe.
   
 2. J

  John W. Mlacha Verified User

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  na hawa wakiamua wanaweza , ila wapemba hawawezi kwani wameshapewa madaraka huku bara basi hawataki kusikia lolote
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,983
  Trophy Points: 280
  ..eneo lau ni dogo sana na it doesnt make any sense kwao kuwa nchi huru.

  ..sababu hiyo, na the fact kwamba Kenya huru ilihitaji kuwa na access na bahari, ndizo zilizopelekea SULTANI wa Zanzibar KULIUZA eneo hilo kwa Kenya.

  ..sasa kama hawa wako makini, na wanataka kufuata sheria, na historia yao, basi wadai kuunganishwa na Zanzibar, lakini siyo kuwa nchi yao wenyewe.

  NB:

  ..mimi siungi mkono kwa eneo hilo kujitenga na Kenya.
   
 4. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MRC Hata nami nimeishuhudia hii kitu nikashangaa sana wanataka wawe km wazanzibari. Ila maisha ya watu wa mombasa ni ya duni ukweli ni kuwa wengi wao hawahusudi shule na kujituma ktk kazi ni uswahili ndio maana kwenye ajira wako wachache na maendeleo yao ni hafifu. Hili kundi lishugulikiwa tu mara baada ya uchaguzi.
   
 5. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  Eneo kuwa dogo sidhani kama ni hoja ya kukifanya kikundi hicho kudai wao kuwa nchi huru. Angalia Vatican,kwa mfano.

  Hilo la wao kujiunga na Zanzibar,ni mjadala mkubwa sana ambao unaweza kutishia uwepo wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Kwani wakenya hawatapenda hilo jambo. Mombasa ni tourist heaven in Africa,wakenya hawatakubali kuliachia eneo hilo.
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli,licha ya eneo la Mombasa kuchangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa kupitia utalii,wakaazi wake wanaishi maisha duni kupita kiasi. Ingawa kuna sababu nyingi,lakini ili la wakaazi hao kuwa wavivu kama waswahili wetu wa Pwani,Lindi na Mtwara,ni moja ya sababu kubwa sana.

  Sasa wameshaonekana ni zaidi ya Al-Shaabab,wakileta chokochoko tu,majeshi ya Kenya yatahamishia operation huko.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,983
  Trophy Points: 280

  Nzi,

  ..tume iliyopendekeza waunganishwe na Kenya iliekeza kwamba eneo hilo ni dogo sana kuweza kuwa dola huru inayojitegemea.

  ..labda ingekusaidia zaidi kama ungetafuta taarifa zinazoelezea historia ya Mombasa mpaka Sultani alipowauza kwa Kenya.


  ..sasa unapo-invoke status ya Vatican, je unataka Mombasa nayo iendeshwe kama Vatican??
   
 8. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  MRC ni wahuni na wazusha fujo wanaotumiwa na mabwana zao toka Arabuni. Hawana sera wala hoja zaidi ya kutafuta kuganga njaa na kujulikana. Ila kwa Kenya wamenoa. Maana watawapoteza mmoja mmoja hadi MRC igeuke past tense. Wanachodai kuwa ni taifa lao hakina msingi wa kisheria wala mantiki zaidi ya fujo za kawaida zikisukumwa na udini wa kipumbavu.
   
 9. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  Sawa mzee.

  Sikumaanisha kwamba Mombasa iendeshwe kama Vatican,nilitaka kuzifananisha kwa msingi wa ukubwa wa eneo.

  Sawa. Nitasoma tena kwa makini historia ya Mombasa na jinsi ilivyouzwa kwa Kenya.
   
 10. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana wameonekana ni tishio zaidi ya Al-Shaabaa. Hiyo inaliweka kundi katika kiwango cha kikundi cha kigaidi.
   
 11. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Mkuu JK,
  Sidhani kama hawa jamaa wana eneo dogo kama jina la kundi lao linavyosadifu, ni Mombasa RC, sawa? Ila madai yao ni kutaka mkoa mzima wa Pwani ujijenge na Jamhuri ya Kenya, mkoa wa Pwani unaweza kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya Rift Valley (kumbuka Kenya yote ina mikoa minane tu).
  Ambako sikubaliani na hawa MRC ni pale wanapojaribu kutumia ushahidi wa kihistoria kudai eneo huru la pwani, kwani itawalazimu kuidai na Zanzibar pamoja na upwa wa Tanganyika, bila kusahau kuwa na Tanganyika itatumia grounds hizo hizo kuzidai Rwanda na Burundi
   
 12. Kabaridi

  Kabaridi JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 2,028
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mombasa Republican Council wao wanataka kuleta migwanyiko kati za sehemu za wapwani. Nimejaribu kufuatilia malalamishi yao na
  ninakuta kuwa wanalalamikia zaidi kutopata makazi na swala la ardhi. Wangalijua wangalitumia jina lingine. pwani ni sehemu kubwa kutoka Lamu hadi kilifi na malindi. Hii ni kama vita vya kidini vya nukia
   
 13. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Be sure of yourself mkuu.
  Harakati za hiki kikundi hakiko powered na dini, bali ukanda. Pwani ni kubwa, inasogea mpaka TAVETA, kwenye miteremko ya Ml. Kilimanjaro, image ya udini unaijenga wewe kwa kuwa ni Mtanzania and thats common amongst ourselves. Wale wanasukumwa na ukanda...
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Apr 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,983
  Trophy Points: 280
  Mphamvu,

  ..I thought wanadai lile eneo lililokuwa mali ya Sultani wa Zanzibar kabla hajalipiga bei kwa Kenya.

  ..kuhusu ukanda wa Pwani ya Tanganyika na Afrika Mashariki eneo hilo nalo Sultani alilipiga bei kwa Wajerumani.

  ..viongozi wa OAU walioamua tufuate mipaka iliyoko sasa hivi walikuwa na busara sana. tukienda kinyume na hapo ni kujitafutia matatizo yasiyokuwa na mwisho, inawezekana ikapelekea tutawaliwe tena.
   
 15. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Makundi kama haya yasichukuliwe ki-juu juu tu. Huu ndio mwanzo wa 'waasi', nk.
  Mambo huanza hivi hivi, kidogo-kidogo. Ghafla unasikia wanapata support ya watu na kuanza kukubalika.
  Vikundi vyote vya uasi na kujitenga katika nchi mbali mbali Afrika vilianza kaka hivyo.
  Kenya, kuweni waangalifu kwa kulitatua swala hili mapema.
   
 16. Kabaridi

  Kabaridi JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 2,028
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Usijali mwenzangu, vitu kama hivi haviwezi faulu. Kama SLDF hawakuweza kule sehemu za mlima Elgon, wataweza hawa? This a replica of a Biafran ideology without the presence of the military involved.
   
 17. Kabaridi

  Kabaridi JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 2,028
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mimi naona Mombasa sasa hivi Kuna Kundi la magaidi wa kiilsamu wanapata ufadhili wa pesa kutoka mataifa ya Iran na Pakistan, maana wana azimio kali la kutengua pwani zima waungane kujenga taifa la pwani huku wakitafuta Malkia wa uingereza awasaidie kuvunja taifa. La kushangaza ni Kenya na wakaazi na pwani wamekuwa na amani na vizazi vyote vya kuanzia UHURU isipokuwa hiki tulicho nacho.
   
 18. livefire

  livefire JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mzalendo i beg to differ, this are idle chaps but ruling out sponsoring from foreign nationalities can not be conclusively deduced so probably some funding mayb flowing. Nway; If you have read the administration mood, specifically administration arm of the police, (AP) which are willingly and so abeiting for a reason to strike the MRC circle I wouldnt loose a pinch of sleep coz of certain bloggers. Rem the extermination of mungiki in the urban centers? Rem the operation against SLDF? MRC is being pushed to the corner by a govt that is silent on their activities, almost assuming they dont exist. when they make good their threat to disrupt elections youl bear me witness, some pipo will be bloody, some missing without a trace and some will be like osama, 'seeing on clips only'......thats if it goes the bloody way buh this is a coward lot. deployment of combat personell will be adequate to cow them. They shoud be championing for economic reforms, not secession...the adminstration authority in Kenya knows not Sultan Hamud, Kenya had several Kingdoms including wanga of the western province..Kalenjins had there own admistration. Kikuyus, dont know about luo but i gez so. MRC is just a bunch of losers!!!
   
 19. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hao MRC hawawezi kufanikiwa kabisa kwasababu hawana hoja ya msingi. Sababu wanayotoa haiwezi kusikilizwa maana itasababisha enzi mpya ya migogoro barani Africa. Africa na mabara mengine yaliyotawaliwa yaliamua kuheshimu mipaka iliyokuwepo wakati wa uhuru na sasa hawa jamaa kama hawatambui hilo wanatakiwa watoe sababu zinazoeleweka (bila shaka hazipo) kuwa ni kwanini wafuate mipaka ya sultan na sio ile ya tawala za kiafrika kabla ya waarabu kuja pwani ya Afrika mashariki. Lakini pia haishangazi kuona vikundi kama hivyo ktk Afrika maana umaskini umekithiri na uwajibikaji haupo.
   
 20. Kabaridi

  Kabaridi JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 2,028
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Let me assure you there is a huge number of MRC fuelled activities in mombasa, you actually heard what went down near kongowea market. 4 guards were exterminated by gangstars. Whether mungiki or MRC, the philosophy of the matter is innocent civilians are facing a full brunt of terror activities. Right now, the politics of negotiations to foster or babysit terror groups is the last thing we need as a country.

  .......Second do you actually know why such groups exist? just like political parties, they are like campaign vehicles but at least this time, tyrannical forms of vehicles to force the votes of a block to swing to a paricular angle. trust me they are. remeber the Moi era when such groups like jeshi la mzee were given room to thrive and while under there, hooligans who could just do anything under the name of vigilante groups.
   
Loading...