Mombasa: Gari linginge latumbukia baharini katika kivuko cha Likoni, uokoaji unaendelea

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Gari moja ndogo limetumbukia baharini katika kivuko cha Likoni alfajiri ya leo Jumamosi Desema 7, 2019 miezi miwili baada ya gari lingine kuhusika katika mkasa kama huo kwenye kivuko hicho.

Kulingana na Shirika la Huduma za Feri nchini (KFS), bado haijulikani idadi ya watu waliokuwa ndani ya gari hilo ambapo mkasa huo ukitokea saa kumi na dakika ishirini alfajiri.

Kwenye taarifa, KFS imethibitisha kisa hicho ikisema dereva wa gari hilo alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi mno, licha ya maafisa wake kumuashiria apunguze mwendo.

"Tuna huzuni kuthibitisha kuwa majira ya saa kumi na dakika ishirini alfajiri katika upande wa nchi kavu wa kivuko cha Likoni, dereva wa gari ndogo ambalo namba za usajili hazijatambulika baada ya kukata tiketi aliondoka kwa mwendo wa kasi na kutumbukia ndani Bahari ya Hindi licha ya kuashiriwa asimamishe gari na maafisa wetu",

Waliokuwemo hawajatambulika lakini boti za KFS za ukoaji zimeanza shughuli ya kulisaka gari hilo zikishirikiana na jeshi la majini, polisi na mashirika mengine ya uokoaji", ilisema taarifa hiyo.
FB_IMG_1575691843839.jpeg
 
Dah, huyu dereva alipatwa na nini ilichompelekea speed kali hadi baharini..! Poleni
 
Poleni sana wanakenya, navy ya wanakenya ambayo huwa tunaiona inajimwambafai kila kukicha tunataka tuone ubabe wake lazivyo ni sawa na bure kabisa.
 
Update..The body of john mutinda has been recovered and his car,a Toyota allion kbx 475b retrieved from the ocean
 
Poleni sana wanakenya, navy ya wanakenya ambayo huwa tunaiona inajimwambafai kila kukicha tunataka tuone ubabe wake lazivyo ni sawa na bure kabisa.
Gari limeopolewa. Omba msamaha kwa navy yetu.
 
Poleni sana majirani
Inaonekana jamaa alikuwa kwenye suicide mission na amefanikiwa hapo tunaomba mtupe mrejesho wa upelelezi ingawa kesi zetu huwa zinaisha hivi hivi bila kujua undani wake
 
Back
Top Bottom