Mahakama hatimaye imewaachia huru wabunge wawili waliotuhumiwa kwa rushwa ya uchaguzi, hali iliyopelekea wabunge hao wawili kukosa haki yao ya msingi ya kugombea kama wanachama wa CCM katika uchaguzi uliopita. Kitendo hicho kimetokana na maombi ya TAKUKURU kuitaka mahakama ifute kesi hiyo kwa kutokuwa na nia ya kuendelea nayo, kesi ambayo ilishawaumiza wabunge hao kwa CC kutengua ugombea wao. Kitendo hiki bila shaka hakiashirii mwisho mwema wa siasa zetu, hasa ukizingatia kuwa kesi hiyo ilihusishwa sana na shinikizo la kisiasa kwa TAKUKURU. Binafsi naona kesi hii imeshusha hadhi ya TAKUKURU kwa mara nyingine tena. Bila shaka hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa, ili vita dhidi ya wala rushwa na mafisadi isitumike kama fimbo ya kuwaadhibu wale ambao wanatofautiana kimaslahi ndani ya mfumo wetu wa siasa. Naomba kuwasilisha hoja.
Wabunge CCM waachiwa
na Mustafa Leu, Arusha
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, jana, imewaachilia huru wabunge wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, na wanachama tisa wa CCM waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za rushwa.
Wabunge hao ni Elisa Mollel wa Arumeru Magharibi na Lekule Laizer wa Longido, Mkoa wa Arusha, pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, Daniel ole Porokwa.
Wengine ni mjumbe wa mkutano wa wilaya, mkoa na taifa wa chama hicho, John Ndelilio Pallangyo na mjumbe wa Wilaya ya Arumeru, Abraham Zellote Kaaya na Katibu wa Kata ya Longido, Emmanuel Luka Laizer.
Pia wamo Ndewirwa Soori Mbise, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nkoaranga na mjumbe CCM mkoa na taifa, Charles Akyoo, Ofisa Mtendaji Kata ya User River pamoja na Abubakari Shekalaghe ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM, Kata ya User River.
Akitoa uamuzi wa kuwaachia huru, Hakimu wa mahakama hiyo, George Ndabagoye alisema kesi hiyo imefutwa baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), kuomba ifutwe.
"Kutokana na maombi hayo ya Takukuru, mahakama imekubaliana nayo na inafuta kesi hiyo ya jinai kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 9 ya mwaka 1985 na washitakiwa wako huru," alisema hakimu Ndabagoye.
Wakizungumza mara baada ya kuachiwa huru, Mbunge wa Longido, Lekule Laiser aliishukuru mahakama kwa kuwatendea haki na kufutilia mbali kesi hiyo aliyosema kuwa ni ya kisiasa.
"Tumepoteza muda mwingi wa kazi za kuwatumikia wananchi, tumefika mahakamani kwa muda wa mwaka sasa hakuna siku kesi imesikilizwa, tunasikitika sana kwa hayo, lakini leo tumeona haki ikitendeka," alisema Laizer.
Alisema ingawa majina yao awali yalichafuliwa kutokana na kadhia hiyo, lakini sasa ni sura nyingine ya wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi kujua ukweli wa tuhuma dhidi yao.
Naye Mbunge wa Arumeru Magharibi, Elisa Mollel alisema suala lao limechukua muda wa mwaka mzima, lakini hakuna hata siku waliyoulizwa kitu. "Kama sisi tunafanyiwa hivyo itakuwaje kwa wananchi wa kawaida?" alihoji Mollel.
Alieleza kuwa Takukuru hawakuwa na ushahidi wowote katika shauri hilo, na kwamba ni mambo ya kisiasa ndiyo yaliwafikisha mahakamani.
Wabunge hao pamoja na watuhumiwa wengine, walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa madai ya kutoa rushwa wakati wa kampeni za uchaguzi ndani ya CCM.
Laizer alikuwa akiwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha wakati Mollel alikuwa akiwania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), kupitia mkoa huo.
Hata hivyo, watuhumiwa hao baadaye walifutwa kuwania nafasi hizo kutokana na kesi hiyo ya jinai iliyokuwa ikiwakabili.
Source: Tanzania Daima 5/07/2008