Mola hakupenda. Kumbe Rais Nkurunziza ilikuwa awe mgeni wetu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Habari ya kusikitisha, kumbe bwana Nkurunziza (rip), ilikuwa awe mgeni wetu. Mapenzi makubwa kiasi gani kwetu sisi kuwa katika ratiba za mwisho mwisho za marehemu?

Ikumbukwe kuwa tangia jaribio lile la Mapinduzi 2015 Nkurunziza alisafiri nje ya Burundi mara moja tu na alipofanya hivyo alikuja Tanzania.

Heshima kwako mzee wa Msoga, mzee Kikwete. Hukuwa na longo longo na koleo uliliita kwa jina lake.

Japo mara hii ilikuwa aje kwa ajili ya ku jipiga nyungu, bado ugeni ulikuwa ugeni tu na tungefarijika mno kuwa naye:

Secret Exposed as Details Leak on What Really Killed Pierre Nkurunziza

Kwa sababu hata katika dakika za mwisho za marehemu tulikuwamo katika orodha ya kuwa wenyeji wake, itakuwa jambo jema nasi kufikiria kwenda kumzika na kumsindikiza ndugu yetu huyu.

Napendekeza angalau tupeleke dream-liner moja ya waombolezaji. CNDD/FDD alichokuwa akikiongoza ni chama rafiki wa moja ya vyama vyetu vikuu sana vya siasa hapa nchini.

Mashirikiano ya vyama rafiki katika dhiki na raha ndiyo u "africanacity" wetu.

Ikumbukwe pia kuwa, Burundi na sisi tuko katika boti moja. Mabeberu wanatuandama mno. Katika mikopo na grants zote kuhusiana na Corona ni sisi na Burundi peke yetu ambao ndiyo wahanga.

Tusiwatelekeze hawa ndugu zetu hasa katika kipindi hiki kigumu mno kwao. Siyo siri ndugu zetu hawa hawana mwingine hata wa kuwafariji tu ila sisi.
 
Kuongeza siku ni jambo la kheri. Katika kumwomboleza marehemu, Profesa Kabudi alimtambua kuwa marehemu ametutoka akiwa kijana mno.

Sina hakika huu umri wa ujana ni hadi miaka mingapi au ni lini mtu anakuwa mzee?

Kwa hakika heri kujaribu kuongeza siku hata kwa kucheka tu.


Ofcourse bado ni kijana yule ! Huwez mfananisha na Kangi Au Kabudi mwenyewe!
 
Mtu alowaua watu huruma wa nini? Au huifaham historia ya Burundi? Hujaona video za watu wakishangilia kifo chake huko Burundi? Ebu lete uzi mwingine bhana.
Wanaomuonea huruma na wanaoshangilia kifo chake wote sawa, maana huruma haitomsaidia huyo marehemu wala kushangilia kifo chake haiwasaidii lolote wanaoshangilia.

Ilikuwa lazima atakufa kama wengine japo ilikuwa haijulikani lini, ila jamaa kaishi maisha na kufanikisha mambo yake.
 
Mtu alowaua watu huruma wa nini? Au huifaham historia ya Burundi? Hujaona video za watu wakishangilia kifo chake huko Burundi? Ebu lete uzi mwingine bhana.

Mkuu ninaandaa uzi mwingine ila ni kweli kuwa huyu bwana alikuwa ni mgeni wetu mtarajiwa, tena mahsusi kabisa kwenye yale mambo yetu. Yale mambo ya kupiga nyungu.

Ilikuwa fursa. Fursa adimu sana mkuu.

Tungekuwa kwenye nafasi njema sana ya ku boost utalii wetu. Kuitangaza nyungu vilivyo kimataifa hata kufikiria kuanzisha wizara kamili inayojitegemea: Wizara ya Nyungu.

Tunakumbushwa kuwa wazalendo na kuiweka Tanzania yetu mbele!
 
Back
Top Bottom