Uchaguzi 2020 Moja ya mambo mazuri aliyofanya Rais Magufuli kuhusu kodi

RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
1,314
1,703
Wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015, kodi ya majengo (property tax) iliyokuwa inatozwa kila mwaka na serikali za mitaa (LGA) kwa kila nyumba/jengo ilitegemea thamani ya nyumba. Kodi hiyo ilitozwa kwa asilimia 0.1. Hivyo watu wote wenye nyumba/majengo mijini katika maeneo yaliyopimwa na yasiyopimwa walilipa kodi hiyo. Nyumba za hali ya chini zilitozwa kuanzia shilingi 30,000/=, nyumba nyingi za kawaida self-contained ziligharimu kati ya shilingi 80,000 hadi laki mbili na zingine wamiliki walilipa hadi shilimgi milioni. Wenye maghorofa ndio usiseme, wamiliki waliyalipia hadi shilingi milioni mbili na zaidi.

Ilifikia hatua baadhi ya wamiliki hasa wastaafu walilazimika kupangisha nyumba zao za kuishi ili tu wapate pesa ya kulipa kodi ya majengo. Fikiria mtu alipata hela sehemu akajenga nyumba ya thamani ya shilingi milioni 200 na baada ya muda akawa hana uwezo ule aliokuwa nao aidha kwa kustaafu au kupungua kwa kipato hivyo kodi hiyo ilikuwa mzigo mkubwa. Pia thamani ya nyumba kila baada ya miaka mitano ilitathminiwa upya na kwa sababu thamani ya nyumba huwa inaongezeka sio kupungua, mmiliki wake alijikuta akitakiwa kulipa kodi zaidi kila baada ya muda wa miaka fulani.

Rais Magufuli alipoingia madarakani, alifanya mambo matatu kuhusu kodi hii: Mosi, aliishusha kodi hii na kuweka kiwango kimoja (flat rate) cha shilingi elfu kumi tu kwa nyumba ya kawaida ya kuishi bila kujali thamani yake, pili kwa nyumba za ghorofa, kila floor ilitozwa shilingi elfu hamsini tu badala ya mamilioni yaliyokuwa yakilipwa awali, tatu katika zile nyumba ambazo wamiliki wake ni wastaafu na wanaishi humo walisamehewa kulipa hiyo shilingi elfu kumi. Maamuzi haya yalileta unafuu mkubwa sana ambao kila mtu mwenye nyumba mijini alinufaika nao. Huu ni mfano mmoja miongoni mwa maamuzi mengi ya kisera yaliyofanywa na Rais Magufuli na kunufaisha watanzania karibia familia zote. Nina hakika hata Lissu ile nyumba yake ya Tegeta kabla ya maamuzi hayo ya JPM alikuwa analipa zaidi ya shilingi elfu hamsini lakini sasa analipia shilingi elfu kumi tu kila mwaka. Hali kadhalika Zitto na wapinzani wengine kwa nyumba zao ni hivyo hivyo

Ikumbukwe pia kabla ya Rais Magufuli kuishusha kodi hii, kulikuwa na mpango wa kupandisha viwango vya kodi hii kutoka asilimia 0.1 kwenda asilimia 0.15 na mchakato wake uliishaanza; hii inamaanisha kama mtu alikuwa analipa shilingi laki moja angelipa laki moja na nusu. Hivyo maamuzi ya Rais Magufuli yalikuja wakati sahihi na yalikuwa na impact kubwa sana kwa maisha ya watanzania wote.

Hivyo wapinzani wanaposema Rais Magufuli anajali maendeleo ya vitu tu na sio ya watu hawasemi ukweli bali wanaongozwa na chuki binafsi kama ukweli huu kuhusu kushushwa kodi ya majengo unavyothibitisha. Fikiria hiyo nyumba yako ulikuwa unailipia shilingi ngapi kila mwaka kama kodi ya majengo na sasa unalipa shilingi elfu kumi tu, Je, hayo sio maendeleo ya watu?
 
Kwenye Kodi usiongee lolote mkuu. Sisi wenye kampuni neo tunajua machungu tunayokutana. Kama huna courage unaweza funga ofisi yako, tunafanya biashara ni Kwa sababu hatuna jinsi tu.

Watu wanalipa kodi huku mioyo Yao haina furaha hata Tra wanapewa target ambayo ni ngumu. Tunalipa Kodi Kwa kulazimishwa.
Jamaa ameharibu mfumo wa taasisi zote nchini.

Amekuwa ni ndo kwenye mamlaka na kufanya mamuzi kwenye taasisi za umma. Bodi za wakurugenzi zipo kama jina tu hazina mamuzi.

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
 
Kero za Kodi Ni nyingi mno

Kuanzisha biashara unatakiwa kulipa Kodi Kwanza

Pili....msururu wa Kodi 19 ...

TRA wanakadiria kwa macho, hawana principles.

Inatakiwa kuwe na econometrics rules..mfano.. ukipata faida kwa mwaka, unalipia Labda, example 8% ya Faida.

Badala yake TRA wanabambikiza Kodi za kuua biashara.

Maafisa wa TRA hasa kipindi hiki cha Jiwe, ndio wanakula rushwa mno
 
Kuhusu kodi huyu mzee ndipo nilijua mnafiki kiasi gani, kuna mahala alifanya mkutano wa nje na wananchi, wananchi wakamlalamikia juu ya kodi na juu ya mistreatment wanazofanyiwa na maafisa wa TRA, akafoka foka hapo na kuwataka maafisa wa TRA wawe polite na kuwatreat vizuri wananchi, Then kukawa na kikao cha ndani na maafisa wa TRA, maneno ninayoyakumbuka aliyowaambia ni “fanyeni mfanyavyo mi ninachotaka ni kodi”!
 
Sasa
Inahitaji ujasiri wa mtu kula mavi adharani ili kumpongeza na kumtetea JPM... So satanic, insane and imbecile...
Kama unavyoona hapa Kuna vilaza hohehahe wamekuja kuanzisha Uzi wengine ndo wanamtetea hapa ..maskini wa kutupwa
 
Wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015, kodi ya majengo (property tax) iliyokuwa inatozwa kila mwaka na serikali za mitaa (LGA) kwa kila nyumba/jengo ilitegemea thamani ya nyumba. Kodi hiyo ilitozwa kwa asilimia 0.1. Hivyo watu wote wenye nyumba/majengo mijini katika maeneo yaliyopimwa na yasiyopimwa walilipa kodi hiyo. Nyumba za hali ya chini zilitozwa kuanzia shilingi 30,000/=, nyumba nyingi za kawaida self-contained ziligharimu kati ya shilingi 80,000 hadi laki mbili na zingine wamiliki walilipa hadi shilimgi milioni. Wenye maghorofa ndio usiseme, wamiliki waliyalipia hadi shilingi milioni mbili na zaidi.

Ilifikia hatua baadhi ya wamiliki hasa wastaafu walilazimika kupangisha nyumba zao za kuishi ili tu wapate pesa ya kulipa kodi ya majengo. Fikiria mtu alipata hela sehemu akajenga nyumba ya thamani ya shilingi milioni 200 na baada ya muda akawa hana uwezo ule aliokuwa nao aidha kwa kustaafu au kupungua kwa kipato hivyo kodi hiyo ilikuwa mzigo mkubwa. Pia thamani ya nyumba kila baada ya miaka mitano ilitathminiwa upya na kwa sababu thamani ya nyumba huwa inaongezeka sio kupungua, mmiliki wake alijikuta akitakiwa kulipa kodi zaidi kila baada ya muda wa miaka fulani.

Rais Magufuli alipoingia madarakani, alifanya mambo matatu kuhusu kodi hii: Mosi, aliishusha kodi hii na kuweka kiwango kimoja (flat rate) cha shilingi elfu kumi tu kwa nyumba ya kawaida ya kuishi bila kujali thamani yake, pili kwa nyumba za ghorofa, kila floor ilitozwa shilingi elfu hamsini tu badala ya mamilioni yaliyokuwa yakilipwa awali, tatu katika zile nyumba ambazo wamiliki wake ni wastaafu na wanaishi humo walisamehewa kulipa hiyo shilingi elfu kumi. Maamuzi haya yalileta unafuu mkubwa sana ambao kila mtu mwenye nyumba mijini alinufaika nao. Huu ni mfano mmoja miongoni mwa maamuzi mengi ya kisera yaliyofanywa na Rais Magufuli na kunufaisha watanzania karibia familia zote. Nina hakika hata Lissu ile nyumba yake ya Tegeta kabla ya maamuzi hayo ya JPM alikuwa analipa zaidi ya shilingi elfu hamsini lakini sasa analipia shilingi elfu kumi tu kila mwaka. Hali kadhalika Zitto na wapinzani wengine kwa nyumba zao ni hivyo hivyo

Ikumbukwe pia kabla ya Rais Magufuli kuishusha kodi hii, kulikuwa na mpango wa kupandisha viwango vya kodi hii kutoka asilimia 0.1 kwenda asilimia 0.15 na mchakato wake uliishaanza; hii inamaanisha kama mtu alikuwa analipa shilingi laki moja angelipa laki moja na nusu. Hivyo maamuzi ya Rais Magufuli yalikuja wakati sahihi na yalikuwa na impact kubwa sana kwa maisha ya watanzania wote.

Hivyo wapinzani wanaposema Rais Magufuli anajali maendeleo ya vitu tu na sio ya watu hawasemi ukweli bali wanaongozwa na chuki binafsi kama ukweli huu kuhusu kushushwa kodi ya majengo unavyothibitisha. Fikiria hiyo nyumba yako ulikuwa unailipia shilingi ngapi kila mwaka kama kodi ya majengo na sasa unalipa shilingi elfu kumi tu, Je, hayo sio maendeleo ya watu?
Hivi ndivyo chama cha mapinduzi kinatakiwa kutetewa.

Sio kuimba mapambio ya mitano tena.
 
  • Thanks
Reactions: RMC
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom