Moja ya majibu kama sio jibu pee la swali watanzania tumekosea wapi? Nani katuloga?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,348
6,472
Imekuwa ikisikika mara nyingi swali ni wapi watanzania tumekosea mpaka kuwa nchi masikini na tabia za kupelekea huko. Baadhi wanahisi tumelogwa kama sio msemo tu. Rais mmoja mstaafu aliwahi kuulizwa swali juu ya chanzo cha umasikini wa Tanzania, na kujibu hafahamu.
Makosa tunayoendelea kufanya yanaweza kuwa ni mengi ila kubwa na laweza kuwa chanzo haswa ni malezi yasiyo bora kwa watoto wetu hasa katika kujenga ubora wa afya kwa ujumla wake. Binadamu anatungwa mimba, mimba inahitaji huduma bora, mazingira ya kujifungua yawe bora, anapokua mpaka miaka mitatu baada ya kuzaliwa, maisha yanatakiwa kuwa bora. Zaidi, mama na baba wa mtoto wanatakiwa nao kuwemo kwenye ubora tangu kutungwa mimba, kuzaliwa, na kukua.

Changamoto kubwa ni kuvunja huo mzunguko na kuelekea kwenye ubora.

Kwa kifupi ni afya ya mama na mtoto na elimu ndio sources kubwa za tunayoshuhudia, ingawaje elimu sijaizungumzia hapo juu ila ni sehemu ya child development.
 
Tungeweza kuwa na mjadala wa kitaifa kwenye hili... Lakini utakapojaribu kufanya hivyo cha kwanza ni kuchunguzwa uraia wako
Hv ilikuwaje siasa ndo ikawa mungu na muamuzi wa maisha ya watu wote. Nani alipanga kwamba wanasiasa ndo wanatakiwa kuongoza nchi?
 
Tutazunguka kote na kuandika mengi lakini tatizo letu la msingi ni moja tu... TULIKOSEA PAKUBWA TULIPOIPA SIASA THAMANI KUBWA KULIKO TAALUMA

Na mbaya zaidi siasa imeendelea kupewa kipaumbele na kuthaminiwa kuliko mifumo mingine yote kwenye jamii! Wanasiasa wamejigeuza kuwa miungu watu! Wanaona fahari kutukuzwa na kuabudiwa kwa kila jambo hata liwe ni la kijinga kiasi gani. Binafsi huwa ninawadharau sana "wanasiasa".
 
Mwanasiasa zero kabisa kichwani formless anapewa hadhi na heshima kubwa kuliko mtaaluma...
Kuliko daktari
Kuliko mwalimu
Kuliko bwana shamba
Kuliko bwana afya nknk
 
Tutazunguka kote na kuandika mengi lakini tatizo letu la msingi ni moja tu... TULIKOSEA PAKUBWA TULIPOIPA SIASA THAMANI KUBWA KULIKO TAALUMA
Je, sio kuwa kosa hili linatokana na malezi mabovu kuanzia tumboni mwa mama zetu?
 
Back
Top Bottom