Moja ya Maamuzi Magumu ya JK ilikuwa kukulazimisha wewe Lowassa Kujiuzulu; Asema Nape Nauye

ninachojua ni kwamba vurugu zote hz ni kwamba mbio za Urais 2015,na Mgombea wa ccm ndie atakae kuwa Rais wa Nchi hii na si Vinginevo,Chadema walie tuu,hawajakomaa kupewa Nchi yet wanahitaji muda mwingi zaidi kujifunza,Angalia hawaelewani wao kwa wao,ref.Shibuda na chadema,Madiwani chadema Arusha,utajifunza mengi sana,nwasilisha.
 
Mopaozi, heshima yako, nilitegemea ungesema yote niliyosema pale kuliko kukata kipande kidogo tu ambaye hakusikiliza kabisa atadhani niliishia hapo na HIVYO itakuwa umempotosha, hii SI sawa NADHANI . HATA HIVYO nakushukuru kwa kunisikiliza.
Afadhali tuwe chama cha upinzani lakini tusimamie maadili yetu kuliko kuwa chama tawala ksichosimamia maadili yake.
 
Anachofanya Nape ni kukiingiza chama kwenye mgogoro mkubwa ambao kusuruhisha haitawezekana labda hadi Nyerere arudi, CCM wangekuwa makini wangesimamisha uanachama wa Nape

nape mtoto wa juzi hawezi kuwashughulikia watu ambao maisha yao yote wame invest kwenye chama, kwa sisi wenye akili Nape hauwezi huu mziki wa kiutu uzima. Ni vita kati ya SITA na Lowassa. Nani zaidi. - ngoma ISAMBE.
 
ninachojua ni kwamba vurugu zote hz ni kwamba mbio za Urais 2015,na Mgombea wa ccm ndie atakae kuwa Rais wa Nchi hii na si Vinginevo,Chadema walie tuu,hawajakomaa kupewa Nchi yet wanahitaji muda mwingi zaidi kujifunza,Angalia hawaelewani wao kwa wao,ref.Shibuda na chadema,Madiwani chadema Arusha,utajifunza mengi sana,nwasilisha.

ccm imeshakufa for your info. hiki chama hakirudi kamwe - amini kauli yangu, kama na wewe ni kada basi nakupa pole sana.
 
Safi sana, Nape Nnauye na Samuel Sitta wamemjibu vizuri sana Lowassa. Yeye anajigamba kwa kufanya maamuzi magumu gani, kuchukua mlungula wa Richmond? Haya ndiyo majibu ya kumgonga nayo Lowassa kwa tuhuma zake lukuki za ufisadi. Next step iwe kumpeleka mahakamani. Ukicheza na Mbwa atakufuata mpaka msikitini!

Naona safari za kurudi Nape, Sitta na wewe CCJ zimeanza!
 
Nape acha longolongo chapa kazi ni mapema mno kuanza kukimbia kivuli chako.

eti kweli umesema mafanikio ya sera ya magamba ni pamoja na watu mitaani na vijiweni kuongea neno Gamba, you are not serious.

siku hizi hata kubadili demu ni kujivua gamba.

Hapo kwenye red, labda nao (magamba) wanataka kuacha cha kukumbukwa kama ilivyo kwa mwanzilishi wa neno UFISADI ambalo mwanzoni walisema halipo hata kwenye misamiati yao. Aibu kwao.
 
Kama kweli Nape kasema hata kujenga UDOM na shule za kata ni maamuzi magumu sasa naanza kujuliza kwa nini kapewa nafasi hiyo.

Alitaka serikali isijenge shule halafu iweje. Wamejenga shule kwa sababu ndiyo moja ya kazi zake na pesa za wananchi pamoja na nguvu zao zilitumika. Pengine Nape haelewi maana ya hii sentensi: "Fanyeni maamuzi magumu" msaidieni jamani.


HIZO SHULE ZA KATA KWA JINA JINGINE TUZIITE SHULE ZA LOWASA. Tulikuwa tukishuhudia wakati ule akiwaita Wakuu wa mikuu pale ofisi kwake na kuwapa maelekezo kuhusu kujenga shule za kata. Huwezi kuzungumzia shule za kata bila kumzunguzia Lowasa na Watanzania Maskini ambao walichangishwa kwa lazima.

Kinachowasumbua CCM ni Uraisi wa 2015,
 
Ni kweli Nape uliyasema haya? LOWASA Mbona alisema mwenyewe "Nimeamua kumwandikia raisi barua ya kujiudhuru" wapi alipolazimishwa kujiudhuru,tumwamin nani wewe au Lowasa,Sijui unawaza nin Nape! Waziri mkuu akijiudhuru baraza zima la mawaziri linavunjika automatically wewe unadanganya kikwete alifanya maamuzi magumu ya kuvunja baraza la mawaziri' yapi hapo? Kama hata kujenga miradi ya maendeleo mnaita uamuzi mgumu basi mmeishiwa! Kujenga chuo kikuu Dodoma ni uamuzi mgumu?! Eti uamuzi mgumu mwingine ni kujenga shule za kata duh' aibu kweli, kila kitu kwenu ni uamuzi mgumu? Halafu mbona wananchi walichangishwa kujenga hizo shule tena wengine wakikamatwa au ndo uamuzi mgumu huo?!
 
ninachojua ni kwamba vurugu zote hz ni kwamba mbio za Urais 2015,na Mgombea wa ccm ndie atakae kuwa Rais wa Nchi hii na si Vinginevo,Chadema walie tuu,hawajakomaa kupewa Nchi yet wanahitaji muda mwingi zaidi kujifunza,Angalia hawaelewani wao kwa wao,ref.Shibuda na chadema,Madiwani chadema Arusha,utajifunza mengi sana,nwasilisha.
Wag'waga shi
 
Ujenzi wa chuo kikuu na ujenzi wa shule za kata si uamzi mgumu. Ni utekelezaji wa programu ambazo serikali iwayo yote inapaswa kufanya ikiwapo madarakani, yaani kuboresha elimu. Kama huo nao ni uamzi mgumu tumekwisha, kwa vile si muda mrefu hata kusafirisha chakula kutoka sehemu moja ya nchi kupeleka sehemu nyingine zilizo na njaa tutaambiwa ni uamzi mugumu!!
 
Back
Top Bottom