Moja ya kosa la wapinzani ni kushiriki katika ziara za huyu mtu na wakati mwingine kumpongeza wakati anaangamiza wanachama wao

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,327
Wapinzani ni lazima muonyeshe kuchukizwa na huyu mtu wa kukalia kimya vitendo hivi vinavyowaangamiza wanachama wenu na njia moja wapo ni kutoshiriki katika ziara zake katika maeneo yenu na kuepuka kabisa kumsifu au kumpongeza kwani pongezi hizi zinamfanya aone anayowatendea watu wenu ni sahihi na kwamba nyinyi ni wepesi wa kusahau hivyo mnampa nguvu ya kuendelea kukalia kimya vitendo hivi viovu.

Nawashauri mjifunze kwa yule kamanda alieko ughaibuni ambae kamwe hana muda wa kumsifu na kumpongeza na ninaamini anafanya hivi kuepuka kumuonyesha kuwa anaweza kuwatendea uovu na bado akasifiwa licha ya uovu wake jambo ambalo si sawa kabisa na hata mimi binafsi huwa nawashangaa sana na huwa siwaelewi huwa mnafuata nini katika ziara zake hizo ambazo wakati mwingine anazitumia hata kunanga upinzani na kusifia chama chake.

Isitoshe, hata mkieleza matatizo yenu,sidhani kama kuna la maana huwa linafanyika na kama lipo,basi nionyesheni mfano wa alilowahi kulitekeleza baada ya nyie kumuomba alitekeleza.Binafsi sijaona zaidi ya kuwahujumu tu.

Kama ndio ustaarabu mnaonyesha kwa kufanya hivi,basi muwe teyari kuyashuhudia na kuyavumila haya yanayoendelea kwani mbaya wenu anaowaona hamko seriuos hivyo ataendelea tu.

Jambo hil niliwahi lisema humu na leo nimelirudia kama kuwakumbusha tu japo kwa style tofauti.

Mimi naishia hapa, nawaachia muamue cha kufanya, ila all in all, ni lazima muonyesha kutomkubali vinginevo atazidi kujisahau.
 
Huu ushauri wako Usubiri kwanza utakapokua mbunge uje ushauri tena..

Na huo ubunge labda ndotoni..
 
nakubaliana na ww! ilibidi atengwe! huwez kuhubiri atengwe na mataifa ya nje huku ndan mnashirikiana
 
Mkuu Salary Slip, Wabunge Was Upinzani sasa hivi Wengine wameingiwa na hofu pamoja na hofu na Wengine wameendekeza Njaa! Yaani ni Wachache saana Ambao nawaona namisimamo yao akiwemo Heche, Mdee na Wengine Wachache. Lakini Walio wengi Unafiki Umetamalaki. Ukimuondoa TL mwenyewe Kujiamini haswa na kajitoa nani mwingine Mbunge aliyedhulika kama Wanachama Wengine wanaodhulika kila Uchao! Siasa za Upinzani zinawavunja Moyo kweli wenye nia ya dhati.
 
Kwakeli sometimes inasikitisha na kukatisha tamaa mno.Yule wa Mbeya siku ile alinisikitisha sana,.

Wanajitahidi kuwa wastaarabu wakati mwenzao hathamini ustaarabu wao bali anawaangamizi huku anawachekea!Sijui kwanini hawajifunzi na kumuonyesha kuwa uovu wake haukubaliki
 
Afrika hakuna Siasa za Kistaarabu, Ukiingia kwenye Siasa uwe tayari kwa lolote. Sasa wanawatesa wenye Mapenzi ya kweli na hawalipwi chochote! Kama ulivyosema ilitakiwa kuonesha kukera kwa Kuachana nao! Sugu alituangusha saana! Hizi Njaa hizi siyo Nzuri, mbona tunakufa Mali tunaziacha!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom