Moja ya Kazi za Bunge ni kuikosoa Serikali,Je wananchi kulikosoa Bunge ni haramu?

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,149
33,308
Wabunge wawapo Bungeni huikisoa serikali vikali kwelikweli,huwabana mawaziri wa serikali kwa nguvu za hoja na hata kwa kejeli,huikosoa serikali Sana na mara nyingine hutoa maneno makali Sana.yes hiyo ndio Kazi ya wabunge na Bunge dhidi ya serikali.

Je, ni makosa kwa wananchi kulikosoa Bunge?
Je, halitaki maoni ya wananchi?
Nakumbuka kila wananchi wakijaribu kutoa tu maoni yao tofauti na Bunge basi Spika wa Bunge hasa ndugai huwaka kwelikweli.

Mfano wa watu waliotoa maoni yao tofauti na Bunge au kulikosoa Bunge au kumkosoa Spika waliitwa kuonnywa ama kusemwa ama kukemewa na Bunge ama kupitia kamati ya maadili ama Spika mwenyewe.

Mfano ni
Pascal Mayala na sasa Genelali Ulimwengu.
Hata Makonda aliwahi kuitwa na kukanywa.
Je ni halali Bunge kuikososa serikali lakini ni haramu kwa wananchi kulikosoa Bunge?
 
Wabunge wawapo Bungeni huikisoa serikali vikali kwelikweli,huwabana mawaziri wa serikali kwa nguvu za hoja na hata kwa kejeli,huikosoa serikali Sana na mara nyingine hutoa maneno makali Sana.yes hiyo ndio Kazi ya wabunge na Bunge dhidi ya serikali...
Wananchi KULIKOSOA BUNGE Haiwezi kuwa Haramu kwani Wananchi ndio waliowaajiri Wabunge je kumkosoa Mfanyakazi wako ni KOSA?
 
Wabunge wawapo Bungeni huikisoa serikali vikali kwelikweli,huwabana mawaziri wa serikali kwa nguvu za hoja na hata kwa kejeli,huikosoa serikali Sana na mara nyingine hutoa maneno makali Sana.yes hiyo ndio Kazi ya wabunge na Bunge dhidi ya serikal....
Ukishakuwa na spika anayejipendekeza ili asitolewe na wabunge bali mkuu wa nchi. Ukishakuwa na wabunge wanaojipendekeza ili wateuliwe uwaziri. Ukishakuwa na chama kinachojiona kushika hatamu muda wote.

Ujue hakuna Bunge hapo la kuikosoa serikali. Bali kuna watu waliomo humo kulinda viti vyao.
 
Hapana siyo haramu, bali ni ubabe tu wa wenye mamlaka...

Hata Rais ametusihi tukosoane kwa staha...
 
Wananchi KULIKOSOA BUNGE Haiwezi kuwa Haramu kwani Wananchi ndio waliowaajiri Wabunge je kumkosoa Mfanyakazi wako ni KOSA?
Ni kosa ndio. Hupaswi kumkosoa, unapaswa KUMUWAJIBISHA. kukosoa ni kama Huna nguvu ya kumuwajibisha!
 
Back
Top Bottom