Moja kati ya suluhu kwa matatizo ya Watanzania

Aug 22, 2015
15
9
MPANGO WA KUENDELEZA MICHEZO TANZANIA

1.UTANGULIZI
Tangu kupata uhuru nchi ya Tanzania mnamo mwaka 1961,kumekuwa na sintofamu kubwa kwenye maendeleo ya sekta michezo na burudani.Hakukuwahi kuwapo mafanikio yoyote ambayo ni ya kujivunia na endelevu katika mchezo wowote kwa zaidi ya miongo mitano ya kujitawala.

Ni ngumu kuamini kwamba taifa la zaidi ya watu milioni arobaini natano(kwa mujibu sensa ya watu ya mwaka 2012) wanakosekana vijana weledi wa kuliwakilisha taifa kwenye michezo ya kimataifa kiushindani. Kupata tu nafasi(tiketi) ya kushiriki michezo mikubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla imekuwa ndoto ambayo kufikiwa kwake imeonekana kuhitaji muujiaza mkuba kutimia.

Mradi wa “Study hard play hard” una malengo ya kutatua changamoto za michezo nchini Tanzania kwa kukusanya vijana wenye vipaji mbalimbali vya michezo na kuwaendelea huku wakiendelea na masomo yao ya kawaida.

Moja ya vikwazo vikubwa kwa vipaji vingi vya michezo nchini Tanzania wazazi kutotaka watotow ajihusishe na michezo wakati wakiwa wanasoma.Hivyo kwa kuliona hilo mradi wa “study hard play hard”umelenga kukusanya vipaji vingi vya michezo katika shule moja ya bweni(boarding)ambapo watakuwa wanalelewa kimichezo huku wakiendelea kupiga kitabu.

2.LENGO KUU (AIM)
Lengo kuu la mpango huu ni kuliweesha Taifa kupata timu za taifa zenye ushindani katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na kuleta mataji nchini kwetu.

3.MALENGO(OBJECTIVES)
  • Kuibua,kukusanya na kuviendelea vipaji vya soka kwa vijana wa Tanzania.
  • Kuibua,kukusanya na kuendelea vipaji vya riadha kwa vijana wa Tanzania.

4.JINSI YA UTEKELEZAJI WA MRADI(OPERATIONAL PLAN)
  • Katika kila mkoa wa Tanzania kutateuliwa shule moja ya bweni ambapo vijana wenye vipaji vya michezo(riadha na soka) watakuwa wanadahiliwa hapo. Vijana hao watakuwa wanaishi hapo shuleni wakisoma bweni na huku wakiendelea na mazoezi..(kwa kuwa vijana hao watakuwa wamekwenda huko kwa hiari,yeyote atakayezembea mazoezini atarudishwa shule za kawaida.

  • Kutakuwa na kocha(mwalimu) wa kuwafundisha hao vijana soka na riadha katika kila shule teule.

  • Mwalimu huyu wa soka atakuwa na wajibu wa kuzunguka ndani ya mkoa wake wote,akihudhuria mabonaza mbalimbali ya mashule ya sekondari ili kuwachagua hao vijana watakaofunwa kwa ngai ya mkoa.vijana hao watapewa uhamisho na kuhamia katika shule hizo za michezo.

  • Kwa kuanza vijana watakaokusanywa watakuwa ni wa sekondari(kidato cha kwana hadi cha nne),ambao kiumri ni kati ya miaka kumi na tatu hadi kumi na nane.

  • Kutakuwa na ligi ya kitaifa itakayoandaliwa kwa kuishirikisha timu ote teule,ambapo kila mkoa utatoa first eleven yake ambao wanaamini kwamba hao ndio wachezaji bora si kwenye mkoa tu bali kwenye shule ambayo wacheaji wake wote ni bora.


5.FAIDA ZA MRADI HUU
  • Kutoka katika mashindano ya kitaifa yatakayoshirikisha shule zote ilioteuliwa kutaundwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17,pia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ambazo zitaliwakilisha taifa viuri kwenye mashindano ya kimataifa.

  • Kuzalisha international players wengi ambao watakuwa wanachea nje ya nchi,kitu ambacho kitasaidia kuja kuunda timu ya taifa yenye wacheaji wenye uoefu wa ligi mbalimbali za nje ya nchi.

  • Kusambaa wacheaji kwenye ligi ya ndani kwa vilabu mbali mbali vya soka.

  • Gharama za uendeshaji wa mradi haitakuwa kubwa sana kwani serikali itahitaji kuwalipa wakufuni mshahara pamoja na gharama za kuzunguka mashuleni kuangalia hivyo vipaji. Gharama ingine za wanafunzi haitakuwa tofauti sana na shulezingine za bweni zinazoendeshwa na serikali.

By Maulid Siogopi

0653887199.

(you can not wait for a soup while boiling an empty pot).
 
Tatizo letu uchawi..yule dogo wa mbao FC ,alipata scholarship Marekani .Wahenga wakafanya yao..vipaji vingi vinapotea
 
Back
Top Bottom