Moja kati ya mapungufu ya katiba ni wepesi wa kufanya mapinduzi kwa serikali iliopo madarakani: Msajili ana uwezo wa kupindua nchi

Abuu hanifa

JF-Expert Member
Aug 17, 2021
256
274
Kufanya mapinduzi ni kukamatwa na kuondolewa kwa serikali na mamlaka yake. Kwa kawaida, ni kukamata madaraka kinyume cha katiba na kikundi cha kisiasa, jeshi, au dikteta.

Hata hivyo vipi katiba yenyewe inaporuhusu kumuondoa raid kutokana na mapungufu ya kisheria.....

Hilo ni moja tu kati ya mapungufu mengi yaliyo ndani ya katiba.

Nguvu walizonazo policcm sasa kana kwamba ni kama vile hakuna chombo kingine kinachoweza kuwazuia jamii huona kama vile policcm imefanya mapinduzi.

Katika mahojiano na star TV Makamu wa Rais wa Kwanza Znz; ametoa darasa jengine. Anasema Serikali imempa mamlaka zaidi msajili wa vyama vya siasa. Si kwa ajili ya nafasi ya kuwa mlezi wa vyama hivyo , Bali kapewa nguvu ya kuvimiliki vyama na wanachama.

Leo hii msajili wa vyama ana mamlaka ya kumvua uanachama hata Rais wa nchi.

Msajili akitangaza kuwa rais wa nchi si mwanachama wa chama Fulani..... Rais hupoteza nafasi yake ya Urais.

Jambo ambalo ni sawa na kampindua Rais aliepo madarakani

 
Msajili usipoteze muda ,changamkia kauli hio tuone kama Makamo wa wapemba kasema kweli..
 
Back
Top Bottom