Tanzania tunashindwa udhibiti wa bei ya mafuta na Congo wanaopigana vita kila siku na raslimali zao kuporwa na mabeberu. Na mafuta yao yanasafirishwa na kulipiwa nauli ya km elfu kadhaa za barabara.
Hatushindwi bali kila Nchi ina policy zake kwenye ishu ya mafuta..

Tzn tumeweka Kodi za kutosha kwenye mafuta Ili kupata mapato..

Hata hivyo nitoe ushauri kwa Serikali,,pamoja na kuandaa vyanzo vingine vya mapato,waajiri vijana wa mikataba Ili kufuatilia maduka na manunuzi yote kwa wananchi wadai risiti na wenye maduka watoe risiti,ukibainika kinyume chake uchukuliwe hatua kali..

Nchi hii watu hawatoi risiti kabisa kwenye manunuzi ya bidhaa,Sasa hapa pekee kuna pesa kubwa Sana inapotea..
 
Shabiby atoa mwarobaini kupanda bei mafuta​

MBUNGE wa Gairo Mohammed Shabib ameitaka Serikali kuruhusu kampuni binafsi kuagiza mafuta wenyewe bila kutumia uagizaji wa pamoja.

Shabiby ametoa ushauri huo leo Jumatano tarehe 6 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema mfumo wa uagizaji wa pamoja unafanya kutokuwepo kwa ushindani wa bei na hivyo bei inapopanda kwenye soko ambalo mafuta yanaagizwa kunakuwa hakuna mbadala.

“Leo hii mkiruhusu kampuni binafsi ziagize mafuta na kama mtu anaona kuna unafuu kwenye uagizaji wa pamoja afanye hivyo na kama ataona haina unafuu alete yeye,” amesema.

Ameongeza kuwa zimekuwa zikitolewa hoja za upotoshaji kwamba uagizaji wa mtu mmoja mmoja unasabisha ukwepaji wa ushuru.

“Meli zote zinashusha kwenye mita wanakwepaje ushuru? Hii kazi waachieni TRA utasikia TRA wanakula dili lakini ukiangalia tangu huu mfumo wa uagizaji wa pamoja mita imekufa mara nyingi kuliko kipindi cha uagizaji binafsi,” amesema.

“Naombeni sana turuhusu hayo na bei ya mafuta itashuka kuliko tulivyotarajia na wala tusidanganyane watu kwamba Serikali inaweza kutoa kodi kwenye mafuta, haiwezekani kodi ndiyo inayolipa mishahara na kununua madawa,” amesema Shabiby.
View attachment 2178669
Hii inji Ina kazi sana
 
Haya yote wametuletea wazungu k*** zao
Sa hivi tungekua zetu porini hatuna habari ya Yesu wala Muhammad wala ngonjera za umeme, magari tungekua zetu tunalima, tunacheza ngoma, tunaoa wake kibwena, tunawinda na kuvua. Hizo ndio zilikua shughuli kuu za mwanadamu hapa duniani.
 
Huyu Mbunge ameongea kitu kimoja kwamba mita za kupima mafuta bandarini zinaaribiwa makusudi. Lkaini cha ajabu sio serikali au wabunge wengine wanataka kuongelea hili kwasababu inawezekana kabisa wanajua wahusika!

Shabiby atoa mwarobaini kupanda bei mafuta​

MBUNGE wa Gairo Mohammed Shabib ameitaka Serikali kuruhusu kampuni binafsi kuagiza mafuta wenyewe bila kutumia uagizaji wa pamoja.

Shabiby ametoa ushauri huo leo Jumatano tarehe 6 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema mfumo wa uagizaji wa pamoja unafanya kutokuwepo kwa ushindani wa bei na hivyo bei inapopanda kwenye soko ambalo mafuta yanaagizwa kunakuwa hakuna mbadala.

“Leo hii mkiruhusu kampuni binafsi ziagize mafuta na kama mtu anaona kuna unafuu kwenye uagizaji wa pamoja afanye hivyo na kama ataona haina unafuu alete yeye,” amesema.

Ameongeza kuwa zimekuwa zikitolewa hoja za upotoshaji kwamba uagizaji wa mtu mmoja mmoja unasabisha ukwepaji wa ushuru.

“Meli zote zinashusha kwenye mita wanakwepaje ushuru? Hii kazi waachieni TRA utasikia TRA wanakula dili lakini ukiangalia tangu huu mfumo wa uagizaji wa pamoja mita imekufa mara nyingi kuliko kipindi cha uagizaji binafsi,” amesema.

“Naombeni sana turuhusu hayo na bei ya mafuta itashuka kuliko tulivyotarajia na wala tusidanganyane watu kwamba Serikali inaweza kutoa kodi kwenye mafuta, haiwezekani kodi ndiyo inayolipa mishahara na kununua madawa,” amesema Shabiby.
View attachment 2178669
Shabiby apewe maua yake,ushauri wake uheshimiwe.
 
Back
Top Bottom