Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,489
- 51,067
Mheshimiwa Bilal.
Popote ulipo, bado wapo Watanzania tunaokukumbuka kwa utumishi wako makini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Elimu yako haina Chembe ya shaka, wewe ni mtaalamu wa Physics ya masuala ya Nyukilia, kwa hiyo naturally wewe ni kichwa. Ndani ya Afrika mko wachache.
Huwa nakufananisha na Mwanaanthropogia ambaye pia kitaaluma alikuwa Mwanafizikia wa Nyukilia pia aitwaye Cheikh Anta Diop, mwafrika aliyeufumbua ulimwengu juu ya kwamba Misri ya kale ilikuwa ni ya mtu mweusi.
Tunakumbuka kazi yako ya kuzindua miradi ya maendeleo kila kukicha kipindi cha utawala wa JK.
Kwa hiyo uzoefu unao, umetumikia vyuo vyetu kama mhadhiri kwa miaka mingi.
Lakini ukiacha hilo, wewe umri wako bado unakuruhusu kuwa rais wa Zanzibar, ndiyo kwanza una miaka 75. Katika mambo ya uongozi huo ni umri wa kawaida kabisa kuhudumu kwenye nafasi ya raisi.
Hawa ambao wanakimbizana kuchukua fomu kupitia CCM ili wawe rais wa Zanzibar nikiwapima katika mzani ni wepesi sana, hawajakomaa vya kutosha katika medani kuweza kuhimili mikikimikiki ya changamoto za maisha ya wananchi wa Zanzibar
Kwa upande wa ACT nako pia wansnchi hatuna wasiwasi juu ya mgombea wao, yuko mzoefu mwingine aliyeiva ambaye ni maalimu Seif. Huyo naye akichukua nchi mambo yatakuwa salama.
Hata hivyo nilikuwa nataka wewe uchukue fomu ili ukiwa rais basi maalimu atakuwa serikalini kama makamu (wa pili au wa kwanza kwa mujibu wa katiba ya Muafaka wa huko), Lakini pia kama yeye atakuwa rais basi na wewe utatwaa nafasi hiyo niliyoitaja.
Lengo ni kuwa na viongozi Matured, ambao hawataendekeza siasa za uvyama, kupata viongozi wanaojua Zanzibar imetoka wapi, iko wapi na inataka kwenda wapi.
Tunataka viongozi watakokwenda kuleta maridhiano baina ya Wazanzibari, ambao watawaweka wazinzibar pamoja na kuondoa siasa za uhasama.
Lakini pia tunataka viongozi watakaoueenzi Muungano wetu.
Kwa hiyo Dr Bilal, sioni yeyote anayeyosha huko Zanzibar kupitia CCM kama wewe.
Chukua fomu, Umri wako wa miaka 75 bado unafaa kuwa raisi wa Zanzibar. Shime Alayka!
Missile of the Nation (Kombora hatari kabisa la Ulinzi wa Taifa)