Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Hasa watakaopumua kwa urahisi ni viongozi ndani ya Serikali ambao kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakipokezana uchungu wa mijeledi ya maneno kwa makala ya Bw. Ali.
Kisa na maana.? Bw. Ali anayefahamika kwa makala yake ya Jicho Pevu ametangaza kujiuzulu kutoka taaluma ya kufichua maovu ya kiutawala na katika jamii, yaani uanahabari na kujiunga na siasa.
Ali katika mtandao wake wa Twitter amesema kuwa "Kwa miaka 10 mfululizo nimekuwa nikisimama nanyi kuzidisha sauti zenu za kuangaishwa. Sasa ni wakati wangu wa kuwauliza, msimame nami katika harakati zangu za kuwania ubunge wa Nyali kwa tiketi ya ODM".
Ameahidi kuwa akitimiza ndoto hiyo atakuwa mshirikishi mkuu wa utawala wa haki kwa Wakenya wote bila ubaguzi.
"Ingawa utawala wa haki na maadili umeonekana wazi kuhepa waheshimiwa bungeni, tusaidiane mimi niirejeshe haki hiyo ndani ya Bunge letu", alisema.
Huku hadi sasa akiwa amebaki katika orodha ya waajiriwa wa KTN kama mhariri wa upekuzi, habari zinasema kuwa Ali hajaonekana kazini kwa wiki moja mfululizo, sasa ameonekana katika jumba la Orange House Jijini Nairobi akikimbizana na mikakati ya uwaniaji.
Wadhifa anaoulenga kwa sasa unashikiliwa na Bw Hezron Awiti, aliye na uwezo wa kuandaa kampeni kali katika kutetea wadhifa huo tena katika uchaguzi mkuu Agosti 8, 2017.
Huku kukiwa na idadi kubwa ya wanahabari ambao wanatoka taaluma hiyo na kujiunga na siasa, Ali atahitaji kila lenye kufaa katika kumenyana na Bw Awiti na wapinzani wengine.