Mohamed Siad Barre: Dikteta wa Somalia aliyejiamini Kupindukia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mohamed Siad Barre: Dikteta wa Somalia aliyejiamini Kupindukia

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by KAMBOTA, Nov 1, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Mohamed Siad Barre
  Na Nova Kambota Mwanaharakati,
  Ukitaja nchi za kisoshalisti za kiafrika za miaka 1970 hutaacha kuitaja Somalia ya jenerali Mohamed Siad Barre aliyewahi kuongoza Somalia kuanzia mwaka 1969 mpaka 1991.

  Mohamed Siad Barre alizaliwa mnamo tarehe 6 oktoba mwaka 1919 katika kijiji cha Shilavo jimbo la Ogaden magharibi mwa Somalia akitokea kwenye kabila la Marehan, akiwa na umri wa miaka 10 Barre wazazi wake wote wawili walifariki hivyo alijikuta akiwa yatima katika umri huo mdogo.

  Mohamed Siad Barre alianza elimu yake ya sekondari katika mji wa Liquu kusini mwa Somalia na baadaye mwaka 1940 alienda mjini Mogadishu kujiunga na elimu ya sekondari hata hivyo utaratibu ulimtaka kupitia kwanza jeshini hivyo akajiunga na jeshi chini ya ukoloni wa Italia , wakati huo ndiyo vita kuu ya pili ya dunia ilikuwa imelipuka mwaka 1939 hivyo Barre na yeye akalazimishwa kwenda vitani ambapo alienda nchini Kenya alipopigania kwenye jeshi la Italy na Ujerumani dhidi ya Uingereza na ufaransa.

  Mwaka 1952 Barre alipata nafasi ya kuhudhuria mafunzo katika chuo cha kijeshi cha Carabinieri nchini Italia kwa miaka miwili na baadaye aliporudi Somalia alizidi kupanda vyeo kwenye jeshi, hadi kufikia mwaka 1960 Somalia ilipopata uhuru wake Barre aliteuliwa kuwa mkuu wa kikosi cha anga huku pia akifanywa kuwa mkuu wa jeshi msaidizi.

  Muda wote huu akiwa jeshini Barre hakuacha kuonyesha mapenzi yake makubwa kwa mfumo wa kisoshalisti wa Urusi hali iliyochochea ukaribu wake na maofisa mbalimbali wa jeshi wa taifa hilo ambalo lilikuwa kitovu cha ujamaa ulimwenguni kwa kipindi kile.

  Kufuatia mgogoro wa katiba nchini Somalia mwaka 1969 mwanajeshi wa cheo cha chini kabisa alimpiga risasi rais wa pili wa Somalia Abdirashid Ali Shermarke,tukio hili lilikuwa ni bahati ya mtende kwa Barre kwani kutokana na tabia yake ya kujiamini tena kuongea bila woga mbele ya wenzake hali iliyomjengea ushawishi mkubwa hivyo siku ya mazishi ya rais aliyeuwawa Abdirashid Ali Shermarke tarehe 21 oktoba mwaka 1969 jeshi lilitwaa nchi katika mapinduzi yasiyo na umwagaji damu na Mohamed Siad Barre akafanywa rasmi kuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Somalia huku pia akifanywa kiongozi wa baraza la mapinduzi "Supreme Revolutionary Council" SRC.
  [​IMG]
  Mji wa Mogadishu ulivyokuwa ukionekana enzi za Barre
  Kuingia kwa Barre katika urais wa taifa kulibadili kabisa historia ya Somalia na pengine historia ya pembe ya Afrika "Horn of Africa" kwani kutokana na tabia yake ya kujiamini kupindukia alitangaza rasmi mkakati wake wa kuijenga upya Somalia huku akidai kuwa anataka Somalia iwe taifa kubwa na pengine iogopwe ndani na nje ya Afrika.

  Mwaka 1970 Barre aliitangaza Somalia kuwa taifa la kijamaa huku mwenyewe akiipaachika jina la "The Great Socialist Somali" ambapo aliamua kabisa kujiegemeza kwa Urusi akipokea misaada mingi ya kijeshi na kijamii, pia alianzisha matumizi ya lugha ya kisomali mashuleni na vyuoni huku akipinga lugha za kigeni hususani kingereza na kiitaliano. Huku akiwa anavalia gwanda la jeshi na miwani miyeusi ya jua Barre alitamka kwa sauti kubwa "sikuja kuwagawa wasomalia bali kuwaunganisha , nitamheshimu kila msomali kwasababu anastahili heshima ila yeyote atakayethubutu kupinga utawala wangu litakalompata asilalamike"

  Mwaka 1973 Barre alifanywa kuwa mwenyekiti wa OAU nafasi ambayo aliitumia vizuri kuimarisha jeshi lake kwa kujipatia silaha za kisasa kutoka Urusi kwa kutumia kkigezo cha kuharakisha ukombozi kwenye mataifa yaliyokuwa bado yakitawaliwa. Alianzisha vijiji vya ujamaa, akajenga barabara na kupiga marufuku ukabila nchini humo kwa kile alichodai wasomalia ni wamoja tu.

  Mwaka 1976 Barre aliingia kwenye mgogoro na maswahiba zake warusi , ili kuwaonyesha yeye si mtu wa kutishwa Barre aliwatimua wataalamu wote wa kirusi waliokuwa nchini Somalia huku akisisitiza kuwa hawezi kutishwa wala kuogiopa mtu yeyote kwasababu anaungwa mkono na wasomali wote.

  Mwaka 1977 Barre alianza vituko vyake pale alipotaka kuongeza eneo la jimbo la Ogaden hali iliyomfanya kuvamia eneo la Ethiopia , hii ilichochea kile kilichoitwa vita ya Ogaden ambapo urusi waliamua kuisaidia Ethiopia ili kumkomoa Barre, mwanzoni vikosi vya Barre vilipata ushindi hata hivyo mwaka 1978 Barre alizidiwa na kuamua kuliachia eneo hilo. Kutoka hapo Barre aliamua kujiegemeza kwa Marekani hali iliyomfanya kujiimarisha tena hata hivyo upinzani wa ndani ya nchi dhidi ya uongozi wake ulizidi mno.

  Mwaka 1986 Barre alipata ajali kubwa ya gari mjini Mogadishu ambapo inaelezwa kuwa aligongwa na lori kufuatia mvua kubwa hivyo dereva wake kulivaa lori, Barre alijeruhiwa vibaya akapelekwa kulazwa nchini Saudi Arabia kwa miezi miwili huku makamu wake Luteni jenerali Mohamed Ali Samatar.

  Baada ya kurejea nchini Somalia Barre alijitahidi kuonyesha kuwa bado anaweza kuendelea kuwatumikia wasomalia hata hivyo tayari vuguvugu la nani atamrithi lilipamba moto nchini humo huku wengi wakiamini hana uwezo tena wa kuendelea kuongoza taifa hilo.
  [​IMG]
  Tangu kuondoka kwa Barre Somalia imetawaliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe

  Mwaka 1988 uasi uliongezeka nchini Somalia hali iliyofanya maisha kuwa magumu mwishowe mwaka huohuo Barre alianza kuua watu hovyo hali iliyokoleza chuki dhidi yake. Mnamo januari 26 mwaka 1991 vikosi vya bwana wa vita aliyefahamika kama Mohamed Farrah Aididvilifanikiwa kumpindua Barre .

  Mohamed Farrah Aidid hakufanikiwa kutwaa madaraka badala yake ukazuka mzozo kati yake na mwenzake Ali Mahdi Muhammad. Baada ya kupinduliwa Barre alikimbilia kwenye eneo la Gezo kwenye jimbo la Ogaden ambapo ndiyo asili yake, baadaye alikimbilia nchini kenya mbapo hata hivyo hakudumu kwani baadaye alihamia mjini Lagos nchini Nigeria hadi mauti yalipomkuta tarehe 2 januari mwaka 1995 na kurudishwa kuzikwa kwenye mji wa Gezo magharibi mwa Somallia.
  [​IMG]
  Mji wa Mogadishu umebaki magofu matupu mara baada ya kung'olewa kwa Barre

  Hadi mauti yanamkuta Barre aliacha wake wawili ambao ni Khadija Maalin na Dalyad Haji Hashi na watoto 12. Mohamed Siad Barre atakumbukwa zaidi kwa kauli yake maarufu aliyowahi kuitoa alipokuwa ukingoni mwa utawala wake kabla ya kuangushwa ambapo alisema "nilipokuja Mogadishu nilikuta waitalia wamejenga barabara moja mkinilazimisha kuachia madaraka basi hali itarudi kama awali lakini pia kumbukeni kuwa mimi nimepata madaraka kwa bunduki hivyo nitaondoka kwa bunduki pia".

  Hata hivyo tangu kupinduliwa kwa Barre Somalia haijakuwa na serikali imara mpaka leo pia kuna vyanzo vingine vinavyodai kuwa Barre aliuwawa kwa kutunguliwa kwenye ndege mjini Mogadishu mwaka 1991.

  Nova Kambota Mwanaharakati,
  +255717 709618
  novakambota@gmail.com
  Kwa Uchambuzi zaidi tembelea Nova Tzdream -
   
 2. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  I said thank you for this useful post.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kambota asante nimekusoma.
   
 4. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dah. Asante Sana Mkuu.
   
 5. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  USEFUL POST
  :eyebrows:
   
 6. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #6
  Nov 1, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  dah mkuu hii nilikua siijui kiundani lkn safi sana thanks
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hii habari yako umeinakiri vema, ila kuna mambo ambayo yameachwa kuhusiana na Rais Barre.

  Katika watawala wa Somalia ukiwaondoa wakoloni wa Kitaliano, huyu ni rais pekee aliye waweza Wasomali. Kilicho mponza ni kukataza Ukabila... Kitu ambacho Wasomali hawataki kuachana nacho mpaka sasa.

  Ukabila ndio unawamaliza Wasomali, na kila kabila linazungumza lugha yake tofauti na lingine. Kuna makabila makubwa ambayo yamegawanyika makundi madogomadogo. Makabila makubwa Somalia ni Darod, Dir, Hawiye, na Isaaq, na kila kabila limegawanyika si chini ya matawi 10 na zaidi. Haya makabila si rahisi kuingiliana kijamii kama vile kuoleana au kuwa na mahusiano ya karibu. Wengi upenda kushika destiri na mila zao kwa sababu kila kabila linajiona kuwa ndio lenye haki ya kutawala somalia.

  Saidi Barre, alitajaribu sana kuondoa ukabila na ndiye aliyekuwa akisisitiza lugha moja ya kitaifa, Kisomali (Af Soomaali). Lakini wakuu wa kikabila hawakutaka ilo jambo kwa sababu lilikuwa linawaondolea madaraka. Rais Barre alitoa amri kwa kila ofisa wa serkali kujifunza Lugha ya Kisomali kwa muda wa miezi sita tu. Kwa sababu alitaka kuondoa Lugha za Kikabila na Kitaliano. Wasomali mpaka sasa wana tabia ya kuuliza makabila kila wanapokutana, wewe kabila gani... toka ukoo gani... unamjua mkuu gani wa kikabila na mambo kama hayo. Ili jambo ndio Saidi Barre alikuwa analipiga vita sana... Na ndicho kilicho mponza na haswa alipotoa amri ya kuwakamata wakuu wa kikabila ambao walikuwa wanawashawishi raiya wasitoe ushirikiano kwa serikali kuu... Aliwauwa na hapo ndipo mauwaji ya kulipizana kisasi yalipoanza.

  Saidi barre, alikuwa hakubaliani na mipaka iliyowekwa na Wakoloni, alikuwa na idea ya kuiunganisha Afrika nzima, japokuwa yeye alikuwa anataka kurejesha somali ile ya miaka kabla ya kuingia mkoloni, na ndio kwenye bendera ya Somali kuna alama ya Nyota yenye pembe tano, ikimaanisha Great Somali, na kila pembe ikiwakilisha sehemu moja ya somali... i.e Somali Mogadishu (British Somaliland), Somali Kenya, somaliland (Italian Somaliland), Somali Djibouti (French Somaliland Djibouti), Somali Ethipia (Eneo la Ogaden, ambalo linamilikiwa na Ethiopia).

  Somali ilingia kwenye matatizo ya vita wenyewe kwa wenyewe, walipomuuwa Saidi Barre, na kila kabila likataka kuongoza nchi, japokuwa Mohamed Farrah Aidid alijitahidi sana kuwaunganisha, lakini alishindwa kwa sababu hakuweza kuwaunganisha Wasomali ambao kila kabila lilikuwa katika harakati za kulipiza kisasi na kugombea madaraka ya kuongoza nchi.

  Mgawanyiko wa Makabila:

  Darod
  : Awrtable, Dhulbahante, Jidwaq, Leelkase, Majeerteen, Marehan, Mora'ase, Ogaden and Warsangali.

  Dir: Akisho, Biyomaal, Gaadsan, Gadabuursi and Issa (Ciise).

  Hawiye
  : Abgaal, Ajuran, Jijeele, Baadicadde, Degodia, Duduble, Gaaljecel, Garre, Habar Gidir, Hawadle, Murule, Murusade, Silcis, Wadalaan na Xaskul. (Angalizo herufi ya X, kwa Wasomali ni H Mfano nikiandika Hassan basi Kismoali ni Xassan).

  Isaaq
  : Arap, Ayoup, Garhajis (limegawanyika makundi mawili Eidagale na Habar Yoonis), Habar Awal (ambalo lipo makundi makubwa mawili Sacad Muuse and Ciise Muuse), Habar Jeclo and Tol Jecle (Axmed Sheikh Isaxaaq)

  Rahanweyn
  Digil: Dabare and Garre.
  Mirifle: Hadame and Leysan.

  Makabila madogo ni Ashraaf, Gabooyo, Madhiban, Reerow-Xassan,Tuni, Sheekhaal, Tumaal and Yibir.

  Makabila ambayo hayana asili ya Somali, au yalikwenda somalia miaka mingi kwa hajili ya biashara na yanafanya asilimia 15% ya Wasomali wote ni Benadiri, Bantus, Bajuni, Bravanese, Waethiopia, Waindi, Waajemi na Wazigua.

  Hao unao wasikia sasa Al shabab, ni moja ya makundi yaliojiunga tena baada ya kupangaranyika kwa kundi lilolkuwa na nguvu, likijulikana kwa jina la Mahakama Islamiiya (Islamic Courts Union). Kundi ambalo lilitawanya na majeshi ya Kiethipia yakisaidiwa na nchi za Marekani na Uingereza matokeo yake ni kuundwa kwa kundi Al shabab (maana yake ni Vijana). Ambalo makao yake makuu yapo Kismayu. Kundi la Al shabab, linakusanya wana harakati kutoka makabila mbalimbali ya Kisomali na hata baadhi ya viongozi wake ni kutoka mataifa mengine, kama vile Kenya (Fazul Abdullah Mohammed), Pakistan (Abu Musa Mombasa), Sudan (Mahmud Mujajir), Saud Arabia (Muhammad Abu Fa'id) na USA (Omar Hammami).

  Kwa ufupi naweza sema Wasomali ni Taifa lisilopendana wao kwa wao, ila huwa wamoja pale mgeni kutoka nje ya Somalia, atakapokuja kuwapiga, wakisha muondoa basi wanarudi kwenye ugomvi wao wa kikabila. Somalia inaitaji mtawala ambaye atakuwa dikteta ili ikae sawa, zaidi ya hapo ni kutwanga maji kwenye kinu.

  Serikali ya Kenya kuingia ndani ya Somali kuwasaka Alshabab, ni kuamsha hali mpya kwa Wasomali pamoja na serkali iliyoko madarakani, kujiunga na kupigana dhidi ya majeshi ya Kenya...! Kenya itakapo hamua kuondoa majeshi yake Somali, kwa kisingizio chochote aidha kwa kushindwa kwa malengo yake au kwa kukimbia gharama, Wasomali watarudi tena kupigana wao kwa wao.

  Wasomali wenyewe wana amini kuwa haya makundi yanayopigana uko Somalia yanafadhiriwa na nchi kubwa kama vile Uingereza na Marekani, lengo ni kuwafanya Wasomali wasijitawale ili lile jimbo la Ogaden ambalo inasemekana lina mafuta mengi liwezwe kumilikiwa na Ethiopia kwa faida ya nchi za Kimagharibi. Na vilevile nchi za Kimagharibi zipate sehemu ya kutupa taka za sumu kwenye bahari ya Somalia.
   
 8. Kimolah

  Kimolah JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  from the track "tribal war". .

  *one, its me and my nation against the world
  two,me and my clan against the nation
  three,me and my family against the clan
  four, me and my brother agains the family,. . . . .what has remained!!?,five, thats right...its me against my brother, we gon fight until we kill one another*
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  X Paster, katika haya:

  Kuna waarabu wengi pia somalia hususan wa asili ya ki Yemen ambao nao ni minorities, naona umewasahau.
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni kweli Wayemen ni wengi Somalia, wanakadiriwa kufikia wakaazi milioni moja.
   
 11. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  niliwahi kuwaona vijana wawili wa kisomali wakipatanishwa na kushikana mikono hatimae kukumbatiana maeneo ya Kariakoo.
  Hawa inasemekana walikuwa na uhasama kama huo uliozungumziwa hapo juu, yaani uhasama wa kikabila.

  na kitu kikubwa walichoahidiwa kupewa kwa muda wa mwezi mmoja mfululizo ni nusu kilo ya ''Mrungi'' kila mmoja.
   
 12. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  walaaalooooooo!hawa watu nawakubali sana wana roho za kijasiri!
   
 13. Radical

  Radical JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Provide some more posts like this man!
   
 14. falcon mombasa

  falcon mombasa JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2015
  Joined: Mar 5, 2015
  Messages: 7,751
  Likes Received: 4,775
  Trophy Points: 280
  noma sana
   
 15. G

  Gen. kasavubu Senior Member

  #15
  Dec 24, 2015
  Joined: Aug 15, 2015
  Messages: 142
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
  Hawa jamaa na wabaguz sana yan wanajiona wao ni bora zaid sabab ya nywele zao kuliko mbantu na kwa namna hio mpk kuja kupatana sio leo, yan dhambi ya ubaguz haimuish mtu
   
 16. Al gator

  Al gator JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2015
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,033
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Huyo Mohamed Farah Aididi alitisha sana miaka ya 1990's hadi 2000's ilikua ukifungua idhaa ya kiswahili ya DW au BBC lazma wamtaje yeye au usikie Wapaleatina wamejilipua kwenye basi huko Israel au Wamelupua gari lililo jaa mawe na vilipuzi.
   
 17. Econometrician

  Econometrician JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2015
  Joined: Oct 25, 2013
  Messages: 7,835
  Likes Received: 6,405
  Trophy Points: 280
  unatuchosha tunao tumia simu,si lazima umu kote
   
 18. kidadari

  kidadari JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2015
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 2,348
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  hapo mwisho umechanganya! unasema yasemekana aliuwawa kwa kutunguliwa kwenye ndege mjini Mogadishu mwaka 1991 na mwanzoni umesema alikimbilia Nigeria na kufariki mwaka 1995!
   
 19. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2015
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,484
  Likes Received: 4,754
  Trophy Points: 280
  very insightful
   
 20. white-frank mhiro

  white-frank mhiro JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2015
  Joined: Mar 18, 2015
  Messages: 760
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
   
Loading...