Mohamed Shomvi wa Mlimani TV na Mohamed Said: Sikukuu za Kumbukumbu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,906
30,248
MOHAMED SHOMVI MLIMANI TV NA MOHAMED SAID: SIKUKUU ZA KUMBUKUMBU

Leo asubuhi nilialikwa Mlimani TV kwa ajili ya mazungumzo kuhusu sikukuu za kumbukumbu na maadhimisho ya kitaifa.

Mtangazaji Mohamed Shomvi alinipitisha katika kumbukumbu ya Saba Saba siku kilipoasisiwa chama cha TANU tarehe 7 Julai 1954, siku ya kuadhimisha uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba na siku ya mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964.

Nilimchekesha mtangazaji kwa kumuuliza mbona kasahau tarehe 10 Desemba, 1963 siku ya uhuru wa Zanzibar?

Basi katika mazungumzo likaja suala la mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Mtangazaji Mohamed Shomvi akayaeleza mapinduzi kwa kuyaita, ''Mapinduzi matukufu.''
Mimi nikamtahadharisha kuhusu kauli yake hii kuwa achukue tahadhari katika maneno yale yake.

Kipindi kilikuwa kinarushwa mubashara.
Tukaingia katika mapinduzi na yaliyotokea katika mapinduzi.

Hapa tukawa na mazungumzo marefu kidogo.
Nilijaribu kueleza kuwa kama watu hawataijua historia ya watu waliohusika katika historia ya nchi yao hawatajua thamani ya historia yao.

Katika mazungumzo haya nikaeleza kuwa mimi binafsi nimeshangaa siku nilipoingia Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba Avenue nikakuta kuta ziko tupu hakuna picha za waasisi wa African Association, TAA wala TANU.

Kuta zipo tupu hazijabeba historia ya jengo lilikuwapo pale mwaka wa 1933 wala picha za wazalendo waliojenga jengo la kwanza la chama hicho wala picha za wale waasisi 17 wa TANU.

Ikiwa hali ndiyo hii vipi watu wataijua historia yao na kuithamini?

May be an image of 2 people, people sitting and indoor
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom