Mohamed Shebe camera yake ndiyo iliyohifadhi historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,887
30,233
MOHAMED SHEBE CAMERA YAKE NDIYO ILIYOTUHIFADHIA HISTORIA YA TANU, MWALIMU NYERERE NA UHURU WA TANGANYIKA

Picha hiyo hapo chini inamuonyesha Mohamed Shebe kushoto na anaefuatia ni John Rupia na kulia mwisho ni Julius Kambarage Nyerere.

Mohamed Shebe kaishi na viongozi hawa toka siku ya kwanza ilipozaliwa TANU kupigania uhuru wa Tanganyika na kupitia jicho la camera yake akahifadhi historia yote ya TANU.

1645935169568.png
 
Anachojaribu ni kuonyesha mchango wa Waislam na Uislamu kwenye kujenga hili taifa ambao anaamini umesahaulika au unadharaulika.
Uislamu wala waislamu hawajasahaulika bali wamejisahau. Kujisahau kwao ni tatizo lao wenyewe na halina uhusiano na nafasi yao katika taifa bali linahusiana zaidi na nafasi wanayoitaka katika taifa.

Kwa mtazamo wao ni kwamba wao wananyimwa haki katika nchi yao wanachosahau ni kwamba hata hao wakristu kuna wakati wanafikiria hivyo hivyo.
 
Uislamu wala waislamu hawajasahaulika bali wamejisahau.Kujisahau kwao ni tatizo lao wenyewe na halina uhusiano na nafasi yao katika taifa bali linahusiana zaidi na nafasi wanayoitaka katika taifa.Kwa mtazamo wao ni kwamba wao wananyimwa haki katika nchi yao wanachosahau ni kwamba hata hao wakristu kuna wakati wanafikiria hivyo hivyo.
Ndio maana nikasema "anavyoamini", kuna waislamu wengi wanaamini serikali imekuwa ikifanya juhudi kukandamiza watu wa imani yao, including kufuta mchango wao kwenye kupambania uhuru etc.
 
Back
Top Bottom