Mohamed Said na Mwanakijiji; Kwanini Hamtaki Tujifunze?

KAMBOTA

Senior Member
Mar 21, 2011
176
103
Nimekuwa nikifatilia makala zako Bw Mohamed Said, nimegundua kitu kimoja "WEWE NI MTETEZI MZURI WA WAISLAMU" vema, pia nimefatilia makala za Bw Mwanakijiji "WEWE NI MTETEZI MKUBWA WA NYERERE".

Ingawaje ninyi ni waandishi wawili wenye mitazamo tofauti lakini inaonyesha ninyi wote si watu wa kukurupuka, huwa mnasoma sana. Kuhusu huu mjadala mkali kuhusu historia sahihi ya mapambano ya uhuru wa Tanganyika nashindwa KUWAELEWA NINYI WAWILI.

Mnaonyesha mnafahamu mambo mengi ambayo ni nadra sana kwa sisi vijana wa siku hizi kuyajua, ila HAMTAKI kuyaweka wazi , mfano nikianza na Bw Mohamed Said wewe unaeleza maswala kadhaa ya kihistoria lakini naona kama vile unaipindisha kwa kuukita mjadala wako kwa waislamu pekee hususani pale Gerezani, pia Mwanakijiji yaelekea unafahamu udhaifu mkubwa wa kihistoria hasa nyakati za Mwalimu Nyerere ila cha ajabu haupo tayari kueleza bayana.

Mimi natoa wito kwenu kama waandishi mahiri na wakongwe, hebu kuweni wazi , tutendeeni haki vijana wa sasa, tupeni uhondo wa kihistoria, watu tupo kwenye computer tangu asubuhi tunafatilia huu mjadala, hivi kwanini HAMTAKI TUJIFUNZE?
 
Wanataka ujifunze labda mjadala umepamba moto sana kiasi cha kukuchanganya.

Wasome kwa kituo na uliza maswali pale usipoelewa utafahamishwa, ni wengi tumenufaika na tunaendelea kunufaika na historia inayosimuliwa na pande zote.
 
Mi pia nimejfunza sana,na nitahfadh ktk kumbukumbu zangu hstoria zote mbili...ili nami mwenyezi Mungu akinijalia uzima,ktk uzee wangu Insha-Allaah niwajuze wajukuu zangu...Japo M.SAID namuona yupo so SPECIFIC....Kwa "Waislamu" na "Wazee" wa Gerezani na Mission Quarter
 
Back
Top Bottom