Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,888
- 30,233
Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli za kunishughulikia zilipoaanza.
Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni kurekebisha mitambo.
Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu wa usalama.
Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.
Nilichukuliwa hadi kwenye chumba kimoja na hapo niliwakuta maofisa wa usalama watatu wakanikaribisha kwa taadhima kisha wakanambia kuwa niko chini ya ulinzi kwa kuwa zimewafikia taarifa zangu kuwa mimi nasafirisha mihadarati. Mpaka hapa sikuwa na hofu bado ilinijia picha kuwa yawezekana wamefananisha majina.
Niliwaambia huenda Mohamed Said muuza madawa ya kulevya siyo mimi niliye mbele yao. Wakaniambia kwa kujiamini kabisa kuwa taarifa zao ni madhubuti muuza unga ni mimi na wamekuwa wakinifuatilia siku nyingi. Hapo ndipo walipotoa pasi yangu na kuniomba niitambue kama hiyo pasi ni yangu au la. Niliwajibu kuwa hakika hiyo ndiyo pasi yangu khasa.
Wakaniamuru sasa tutoke twende nikachukue mizigo yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa haraka huku nikisoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imefika siku yangu.
Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza kufikiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike na shari yangu.
Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa sitokubali kugusa mizigo yangu bila kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka Tehran mizigo ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama.
Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha kuthibitisha kuwa kweli mie ni msafirishaji wa madawa ya kulevya. Jibu nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa zilizowafikia. Wakasema, “Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni msafirisha madawa ya kulevya.”
Nikawauliza,“Baada ya kupata taarifa hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli?” Wakasema, “Ndiyo maana leo tumekukamata.” Nikawaambia, “Si kweli kama kwa sababu mie nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni “Mzungu wa Unga” kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya.”
Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi nini katika hii safari ya Iran?
Niliwaeleza kuwa miezi michache iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano umefadhiliwa na serikali ya Marekani na wamenipa na tiketi toka Dar es Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha.
“Mbona hamkunikamata wakati ule?” Nikafungua mlango mwingine nikawaambia, “Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyasa Muislam?” Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.
Baada ya kukurukakara nyingi na mabishano makubwa kuhusu mie kukubali kufanyiwa upekuzi wa mizigo yangu alikuja binti mmoja katika wao na yeye akanihakikishia kuwa wao ni serikali na sio wahuni. Hawathubutu kuniwekea dawa katika mizigo yangu hivyo akanisihi sana kwa upole nikubali ili wajitoe wasiwasi na wataniachia endapo hakuna kitu.
Niliomba apatikane shahidi wa kushuhudia mizigo yangu kabla ya kufanyiwa upekuzi lakini hakuna mtu aliyekubali kuchukua dhima ile katika maofisa waliokuwa kazini pale uwanja wa ndege usiku ule. Upekuzi ukafanyika hadi mwilini. Hakuna kitu. Wakanipela katika choo maalum cha kutolea madawa kwa njia ya haja kubwa.
Nikakataa kujisaidia pale. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuona choo kama kile. Choo chenyewe ni cha aluminium. Tofauti na vyoo vya pale ambavyo siku zote ni vichafu, hiki kilikuwa kisafi sana kiasi mtu unaweza hata kutengewa chakula na akala bila ya kuhisi kinyaa.
Nilitegemea wataweka ahadi yao kuwa ikiwa hawatakuta madawa ya kulevya katika mizigo yangu watanirejeshea uhuru wangu wataniachia niende nyumbani. Haikuwa hivyo. Wakanirudisha ofisini kwao. Sasa wakaacha madawa ya kulevya wakahamia katika vitabu na “audio cassette” nilizokuwa nimepewa kama zawadi kule Tehran wakaniluliza kwa nini naingiza vitu vile khasa kanda za Khomeni na vitabu vyake nchini. Nikawauliza, “Kwani kanda na vitabu vya Khomeni haviruhusiwi kuingizwa Tanzania?