Mohamed Dewji: Ninamwachia Mungu Serikali kunidhulumu mashamba na viwanda vyangu

Baada ya kumaliza kuongea na wandishi wa habari kuhusu masuala ya timu ya Simba,Mwananchi alifuata kutaka kujua hatima ya mashamba yake

Mo akajibu"Hili suala la mashamba tuliache tu,ni kumuachia mungu"

My take :Hii kauli inaashiria maumivu anayopata Mo kutokana na vitendo vinavyofanywa na awamu hii ya 5,mara atekwe mara anyang'anywe mashamba,mara accounts zake zikaguliwe

Wakati ulaya na marekani serikali ziliwasapoti mabourgeoisie,wakaleta mapinduzi ya viwanda ulaya na marekani huku Tanzania wanaonwa kama ni watu hatari sana

Nani asiyejua mabourgeoisie kipindi cha marcantelism mbinu walizotumia kuacumulate wealth,hazikuwa fair,lakini hao ndo walisababisha ulaya kuwa kama ilivyo sasa ambayo kila mwafrika anatamani aishi ulaya

Ujamaa haujawahi kushinda duniani

2020 twende na Lisu

Sent using Jamii Forums mobile app
Na tunamnyang'anya tu maana ameyahodhi badala ya kuyafanyie shughuli za uzalishaji....kwani yeye nani bwana.
 
Unajua maana ya mashart?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna sheria nyingine ni kandamizi!Labda nimenunua ardhi ili nilime,nimeshindwa kuendeleza shamba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu,basi kwanini usifanyike utaratibu wa mimi kupata walau sehemu ya gharama niliyotumia?Maana hapa serikali inakuwa imeuza ardhi mara mbili!Nanyang'nywa mimi anauziwa mwingine!
 
Anyway, sijui bhana lakini picha ninayopata hapa ni ushahidi wa kimazingira kwamba Mo alitekwa na serikali!! Serikali ilimteka Mo kama njia ya kum-blackmail ili afunge mdomo kwa chochote kitakachotokea dhidi yake!

Tena nimekumbuka! Hivi yule jamaa ambae alikamatwa kwa madai ndie alihusika kwa namna moja au nyingine, hivi kesi yake ipo Mahakama ya Kisutu, Mahakama Kuu, Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Ilala, au Temeke?!

serikali ikifikia muda ku blackmail mtu, siyo serikali hiyo
waza vizuri
 
Binafsi naipongeza serikali kumnyang'anya naomba waendelee kumfuatilia kama kuna mengine anamiliki bila kuyaendeleza nayo pia anyang'anywe tu.

Anajifanya Mungu mtu alidhani serikali hii ni legelega kama zile alizokuwa anazichezea!

Eti amewatuma waandishi wa habari wanazi wa simba kuharibu mchakato wakuichangia Yanga maana wakifanikiwa simba wataamka na kumnyang'anya timu!

Ndo maana ana afya mbaya na roho yake nyeusi kama paka wa mchawi.
 
Kama alipewa bure akashindwa kuyaendeleza hapo Serikali inaweza kuwapa wanyonge ambao wanaweza kuyalima .Lakini kama ali aliyanunua na kuweka mtaji wake hapo sio sahihi his titles of occupancy kuwa revoked.
 
Baada ya kumaliza kuongea na wandishi wa habari kuhusu masuala ya timu ya Simba,Mwananchi alifuata kutaka kujua hatima ya mashamba yake

Mo akajibu"Hili suala la mashamba tuliache tu,ni kumuachia mungu"

My take :Hii kauli inaashiria maumivu anayopata Mo kutokana na vitendo vinavyofanywa na awamu hii ya 5,mara atekwe mara anyang'anywe mashamba,mara accounts zake zikaguliwe

Wakati ulaya na marekani serikali ziliwasapoti mabourgeoisie,wakaleta mapinduzi ya viwanda ulaya na marekani huku Tanzania wanaonwa kama ni watu hatari sana

Nani asiyejua mabourgeoisie kipindi cha marcantelism mbinu walizotumia kuacumulate wealth,hazikuwa fair,lakini hao ndo walisababisha ulaya kuwa kama ilivyo sasa ambayo kila mwafrika anatamani aishi ulaya

Ujamaa haujawahi kushinda duniani

2020 twende na Lisu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mlitaka kwasababu ni mfadhili wa simba ahodhi ardhi bila kuitumia na kuchukulia mkopo benki. Rais Magufuli yupo sahihi kabisa kwenye suala hili wala huyo Mungu hawezi kukubali dhulma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani wakijisikia tu wanakunyang'anya!Kama ndivyo,kwanini serikali huwa inalipa fidia pale barabara inapofuata mashamba au ardhi za watu?Kwanini wasichukue tu maana ardhi ni yao?Nchi za watu ukimiliki shamba ni utajiri,huku kwetu unaweza kunyang'nywa muda wowote!
Ni kweli kuwa kama eneo ulilopo unalimiliki Kisheria ni lazima watakulipa fidia kwa ajili ya maendeleo uliyoyafanya kwenye ardhi hiyo pamoja na usumbufu ukataoupata. Lakini ukitaka kujua ardhi siyo yako, wewe goma kupokea fidia kwa madai kuwa ardhi yako unaipenda na hauko tayari kuiachia. Hapo ndipo utajua kuwa hata fidia uliyokuwa unapewa ni kama neema tu.
 
Tujikumbushe bei za magunia above market rate....leo ndio Mungu anakumbukwa. Masharti ya mashamba kushindwa kufuatwa...la kufanya sasa anatakiwa alipe wafanyakazi wake vizur
 
Kuna dhambi ambazo serikali hii inafanya hakika shetani anaweza kusema mbele ya Mungu kuwa mimi sijawadanganya?

Serikali hii ni zaidi ya shetani
Kwa hiyo unakubali mashamba yashikiliwe bila kuendelezwa. Hii nchi inamiliki ardhi yote, mwananchi unaruhusiwa kuhodhi ardhi ila kwa sheria kuwa uitumie kwa dhumuni lililokusudiwa, ndomana hata km una kiwanja usipokiendeleza unapokonywa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amerudishiwa hela alizonunua hayo mashamba? Pili kwa kawaida serikali inaandaa mazingira wezeshi kwa wananchi katika kufanya shughuli za uzalishaji,na kuwawezesha kimkopo,serikali hii kila kitu kodi,kila taasisi utakayofika ili kuanzisha mradi kodi,kodi,kodi,kodi,

Wakati huo for instance mazao yakikosa soko hawana shida wao wanachojali ni kodi

Serikali hii ipo kiujamaa zaidi,inachukua mashamba inawapa wananchi ili walime sijui,mahindi na watakati huo tunataka viwanda kwa raw materials zipi?

Kwa hali hii hatutasonga mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda hautasonga mbele wewe na mmeo lakini nchi inasonga na itazidi kusonga mbele no matter unalia au unacheka.
Mtu anamiliki thousands of acres kwa zaidi ya miaka 20 bila kuyaendeleza halafu unataka serikali imchekee tu?
Kama mnaonewa nenda mahakamani.
KIFINYO KINAENDELEA
 
Ofisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL), Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema anamwachia Mungu suala la kampuni hiyo kupokonywa mashamba na mengine kuwekwa chini ya uangalizi na Serikali.

Hivi karibuni, Serikali ilitangaza kufuta umiliki wa mashamba sita yenye ukubwa wa ekari 12,915 yaliyopo Korogwe mkoani Tanga.

Pia, wiki iliyopita bungeni Serikali ilisema mashamba sita yanayomilikiwa na mfanyabiashara huyo bilionea yako chini ya uangalizi na kama atashindwa kutekeleza masharti yatafutwa.

Juzi, Mo akizungumza na Mwananchi mara baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya mwenendo wa timu ya Simba, alisema hayupo tayari kulizungumzia suala hilo la mashamba.

“Kaka naomba uniache tafadhali. Mambo mengine tumuachie Mungu,” alisema Mo kwa kifupi.

Mwezi uliopita, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiwa ziara wilayani Korogwe alitangaza uamuzi wa Serikali wa kubadilisha mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na kampuni hiyo.

Alisema mashamba yaliyofutwa ni yale yaliyopo eneo la Mombo, Mabogo na Kwalukonge wilayani Korogwe.

Naibu waziri huyo alisema uamuzi wa kufuta mashamba hayo umefikiwa baada ya mapendekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu.

Pamoja na mashamba hayo kufutwa wiki iliyopita bungeni, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii alisema awali mfanyabiashara huyo alipewa onyo kuhusu mashamba 12 kati ya 21 aliyokuwa akimiliki akitakiwa kuyaendeleza.

Alisema Serikali tayari imefuta hati za mashamba sita na kwamba bado sita ambayo yako kwenye uangalizi.

Waziri huyo alisema Tanzania ina mashamba makubwa 2,000 ya kilimo na ufugaji.

“Haijatokea nikapata agizo kutoka kwa Rais kuwa nifute hati ya shamba la mtu,” alisema Waziri Lukuvi.

Hayo mashamba yametelekezwa vipi wakati kuna kiwanda cha katani ndani yake , nyumba za wafanyakazi na kila kitu, hii dhulma mbaya sana serikali inafanya
 
Watoto wanao zaliwa korogwe hawana mashamba afu mhindi mmoja ahodhi mamilioni ya ekari za mashamamba yote hayo upuuzi wa hivi ata Mungu akiachiwa atapenda ujinga wa hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ofisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL), Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema anamwachia Mungu suala la kampuni hiyo kupokonywa mashamba na mengine kuwekwa chini ya uangalizi na Serikali.

Hivi karibuni, Serikali ilitangaza kufuta umiliki wa mashamba sita yenye ukubwa wa ekari 12,915 yaliyopo Korogwe mkoani Tanga.

Pia, wiki iliyopita bungeni Serikali ilisema mashamba sita yanayomilikiwa na mfanyabiashara huyo bilionea yako chini ya uangalizi na kama atashindwa kutekeleza masharti yatafutwa.

Juzi, Mo akizungumza na Mwananchi mara baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya mwenendo wa timu ya Simba, alisema hayupo tayari kulizungumzia suala hilo la mashamba.

“Kaka naomba uniache tafadhali. Mambo mengine tumuachie Mungu,” alisema Mo kwa kifupi.

Mwezi uliopita, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiwa ziara wilayani Korogwe alitangaza uamuzi wa Serikali wa kubadilisha mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na kampuni hiyo.

Alisema mashamba yaliyofutwa ni yale yaliyopo eneo la Mombo, Mabogo na Kwalukonge wilayani Korogwe.

Naibu waziri huyo alisema uamuzi wa kufuta mashamba hayo umefikiwa baada ya mapendekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu.

Pamoja na mashamba hayo kufutwa wiki iliyopita bungeni, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii alisema awali mfanyabiashara huyo alipewa onyo kuhusu mashamba 12 kati ya 21 aliyokuwa akimiliki akitakiwa kuyaendeleza.

Alisema Serikali tayari imefuta hati za mashamba sita na kwamba bado sita ambayo yako kwenye uangalizi.

Waziri huyo alisema Tanzania ina mashamba makubwa 2,000 ya kilimo na ufugaji.

“Haijatokea nikapata agizo kutoka kwa Rais kuwa nifute hati ya shamba la mtu,” alisema Waziri Lukuvi.
"Naibu waziri huyo alisema uamuzi wa kufuta mashamba hayo umefikiwa baada ya mapendekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu."Hii ni kweli au sio kweli?Kama ni kweli analalama nini.Sheria ni msumeno,he is not above the law.
 
"Hakuna aliyesalama kwenye utawala wa huyu diktekta" Nikikumbuka hii kauli huwa namtazamaga TL kwa jicho la Unabii
 
Back
Top Bottom