Mohamed Dewji: Ninamwachia Mungu Serikali kunidhulumu mashamba na viwanda vyangu

Mohamed Dewji: Ninamwachia Mungu Serikali kunidhulumu mashamba na viwanda vyangu!
 
Waende na huko Babati vijijini yapo mashamba mengi tu yamegeuka mapori, halafu wananchi hawana ardhi wanageuzwa vibarua kwenye mashamba ya miwa.
 
Kwahiyo ukinunua gari ukapaki nyumbani huendeshi unyang'anywe? Ukinunua TV ukaiweka ndani hutazami unyang'anywe?! Hivi mwenye mali si ndiye ana amua ni lini na kwa vipi atumie mali yake? Wewe ukimuuzia mtu nyumba unataka lazima alale humo? Tutumie akili huyu ntu alinunua kihalali kwanini anyang'anywe mali zake?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania ardhi yote ni mali ya serikali ya ccm mtu hawezi kumiliki ardhi TZ
 
Baada ya kumaliza kuongea na wandishi wa habari kuhusu masuala ya timu ya Simba,Mwananchi alifuata kutaka kujua hatima ya mashamba yake

Mo akajibu"Hili suala la mashamba tuliache tu,ni kumuachia mungu"

My take :Hii kauli inaashiria maumivu anayopata Mo kutokana na vitendo vinavyofanywa na awamu hii ya 5,mara atekwe mara anyang'anywe mashamba,mara accounts zake zikaguliwe

Wakati ulaya na marekani serikali ziliwasapoti mabourgeoisie,wakaleta mapinduzi ya viwanda ulaya na marekani huku Tanzania wanaonwa kama ni watu hatari sana

Nani asiyejua mabourgeoisie kipindi cha marcantelism mbinu walizotumia kuacumulate wealth,hazikuwa fair,lakini hao ndo walisababisha ulaya kuwa kama ilivyo sasa ambayo kila mwafrika anatamani aishi ulaya

Ujamaa haujawahi kushinda duniani

2020 twende na Lisu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kuuliza,hivi hayo mashamba walioewa bure?Kama siyo bure,kwanini mtu akishindwa kuendeleza shamba alilonunua ananyang'anywa?Kwanini asipewe hela yake aliyonunulia?
 
Lakini wao wanasema wameyachukya kisheria, ila sielewi kivipi?! Mchezo huu unakomaa ccm, kwa kuwasingizia wanyonge.
Nyerere alifanya nao wanaiga, ili tu wafanane naye.
Wangeyataifisha wayalime, lakini wanagawia wananchi, je, ni nani anastahili kupewa nani hastahili kupewa?! Au wanapewa wana ccm a.k.a wazalendo?!
 
Naomba kuuliza,hivi hayo mashamba walioewa bure?Kama siyo bure,kwanini mtu akishindwa kuendeleza shamba alilonunua ananyang'anywa?Kwanini asipewe hela yake aliyonunulia?
Hahaha wanataka vyote mashamba, pesa aliyotumia kununulia na kodi pia.
 
Hakika serikali hii inapenda kula pale ambapo hawajapanda............

Hiki kinachofanyika hivi sasa cha kuwanyang'anya mashamba waliyoyapata kihalali hao wafanyibiashara ni "pure" ujambazi!
 
Anyway, sijui bhana lakini picha ninayopata hapa ni ushahidi wa kimazingira kwamba Mo alitekwa na serikali!! Serikali ilimteka Mo kama njia ya kum-blackmail ili afunge mdomo kwa chochote kitakachotokea dhidi yake!

Tena nimekumbuka! Hivi yule jamaa ambae alikamatwa kwa madai ndie alihusika kwa namna moja au nyingine, hivi kesi yake ipo Mahakama ya Kisutu, Mahakama Kuu, Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Ilala, au Temeke?!
 
Hivi hao Mapebari Na Mabwanyenye wa Ulaya unaowatolea mfano walipokuwa wanamiliki Mashamba makubwa waliyatumia kwa Uzalishaji Au waliyaacha mapori tu kwa Miaka mingi?

MO angefanya Kama walivyofanya Mabepari wa Ulaya kwa maana ya kuyatumia kwa kuzalisha nani angempora?

Mo kanyang'anywa Mashamba kwa kushindwa kuyaendeleza Au Nyie mnaona ingefaa yaendelee Kuwa Mapori?
 
Anyway, sijui bhana lakini picha ninayopata hapa ni uthibitisho kwamba Mo alitekwa na serikali!
Hiyo ipo wazi watekaji wa wananchi ni hawa hawa
FB_IMG_1549863480324.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kuuliza,hivi hayo mashamba walioewa bure?Kama siyo bure,kwanini mtu akishindwa kuendeleza shamba alilonunua ananyang'anywa?Kwanini asipewe hela yake aliyonunulia?
Kwasababu kisheria ardhi yote ni mali ya Serikali ni si ya mwananchi, Haijalishi umeinunua kwa shilingi ngapi, na haijalishi una docs kiasi gani za kuhalalisha umiliki wako, bado ardhi yote ni ya serikali na hivyo wana maamuzi ya kukunyang'anya wakati wowote wakijisikia, maana ni yao.
 
Hivi hao Mapebari Na Mabwanyenye wa Ulaya unaowatolea mfano walipokuwa wanamiliki Mashamba makubwa waliyatumia kwa Uzalishaji Au waliyaacha mapori tu kwa Miaka mingi?

MO angefanya Kama walivyofanya Mabepari wa Ulaya kwa maana ya kuyatumia kwa kuzalisha nani angempora?

Mo kanyang'anywa Mashamba kwa kushindwa kuyaendeleza Au Nyie mnaona ingefaa yaendelee Kuwa Mapori?
Amerudishiwa hela alizonunua hayo mashamba? Pili kwa kawaida serikali inaandaa mazingira wezeshi kwa wananchi katika kufanya shughuli za uzalishaji,na kuwawezesha kimkopo,serikali hii kila kitu kodi,kila taasisi utakayofika ili kuanzisha mradi kodi,kodi,kodi,kodi,

Wakati huo for instance mazao yakikosa soko hawana shida wao wanachojali ni kodi

Serikali hii ipo kiujamaa zaidi,inachukua mashamba inawapa wananchi ili walime sijui,mahindi na watakati huo tunataka viwanda kwa raw materials zipi?

Kwa hali hii hatutasonga mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kumaliza kuongea na wandishi wa habari kuhusu masuala ya timu ya Simba,Mwananchi alifuata kutaka kujua hatima ya mashamba yake

Mo akajibu"Hili suala la mashamba tuliache tu,ni kumuachia mungu"

My take :Hii kauli inaashiria maumivu anayopata Mo kutokana na vitendo vinavyofanywa na awamu hii ya 5,mara atekwe mara anyang'anywe mashamba,mara accounts zake zikaguliwe

Wakati ulaya na marekani serikali ziliwasapoti mabourgeoisie,wakaleta mapinduzi ya viwanda ulaya na marekani huku Tanzania wanaonwa kama ni watu hatari sana

Nani asiyejua mabourgeoisie kipindi cha marcantelism mbinu walizotumia kuacumulate wealth,hazikuwa fair,lakini hao ndo walisababisha ulaya kuwa kama ilivyo sasa ambayo kila mwafrika anatamani aishi ulaya

Ujamaa haujawahi kushinda duniani

2020 twende na Lisu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania ilipata nuksi na mkosi mkubwa mno 2015

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi ina ardhi kubwa ajabu, ina maana serikali imekosa sehemu za kuwapa hao wanyonge hadi imnyang'anye mfanyabiashara mkubwa kama Mo Dewji?
 
Hivi mali ni nini hapo? Ni ardhi au shamba? Na unaposema mtu hajaendeleza shamba una maana gani?
Mimi nilidhani hili ni suala la umiliki wa ARDHI. Ukiwa na ardhi unaweza kukopa fedha benki ukaendeleza miradi au biashara zako zingine.
Hii sera ya kurasimisha miliki za ardhi kimila au katika makazi holela mijini lengo lake ni nini?
Mbona kuna elements uholela (arbitrariness) na ubaguzi hapo? Kama sio mizengwe (capriciousness).
Tuna sera isiyoeleweka au inayojikanganya (ambiguous) kuhusu umiliki wa ARDHI.
Na sababu kubwa hapo ni unafiki na uchoyo. Tunapenda ujamaa lakini rohoni tuna ulafi wa kibepari, halafu ubinafsi na uchoyo pia! Ndio maana sera zetu zina ubaguzi, uonevu, mizengwe na unafiki wa ajabu!
Unampa mtu kitu kwa mkono wa kulia halafu kwa mkono wa kushoto unamnyang'anya! Leo bosi kasema hivi, kesho mtu wake anasema kinyume na bosi!
Leo huyu anafukuzwa kazi kwa kughushi vyeti na mwingine anapandishwa cheo!
Haya ndiyo yanaitwa
1. Arbitrariness
2. Ambiguity
3. Capriciousness na
4. Impunity
Usitegemee utawala wa sheria hapo, sjui bora au haki yoyote!
 
Amerudishiwa hela alizonunua hayo mashamba? Pili kwa kawaida serikali inaandaa mazingira wezeshi kwa wananchi katika kufanya shughuli za uzalishaji,na kuwawezesha kimkopo,serikali hii kila kitu kodi,kila taasisi utakayofika ili kuanzisha mradi kodi,kodi,kodi,kodi,

Wakati huo for instance mazao yakikosa soko hawana shida wao wanachojali ni kodi

Serikali hii ipo kiujamaa zaidi,inachukua mashamba inawapa wananchi ili walime sijui,mahindi na watakati huo tunataka viwanda kwa raw materials zipi?

Kwa hali hii hatutasonga mbele

Sent using Jamii Forums mobile app

Maendeleo Kwenye Sector zote zinategemea Uzalishaji sio umiliki

Kama una miliki shamba Na halitumii kwa Uzalishaji haliwezi kuleta faida wala Maendeleo
Acheni kukosoa Kila kitu bila ya facts

Wewe unaweza ukataja Nchi Hata Moja ambayo iliendelea kwa Wawekezaji kuhodhi Maeneo ya Kilimo Halafu wakawa hawalimi?
 
Kwasababu kisheria ardhi yote ni mali ya Serikali ni si ya mwananchi, Haijalishi umeinunua kwa shilingi ngapi, na haijalishi una docs kiasi gani za kuhalalisha umiliki wako, bado ardhi yote ni ya serikali na hivyo wana maamuzi ya kukunyang'anya wakati wowote wakijisikia, maana ni yao.
Yaani wakijisikia tu wanakunyang'anya!Kama ndivyo,kwanini serikali huwa inalipa fidia pale barabara inapofuata mashamba au ardhi za watu?Kwanini wasichukue tu maana ardhi ni yao?Nchi za watu ukimiliki shamba ni utajiri,huku kwetu unaweza kunyang'nywa muda wowote!
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom