Mohamed Dewji: Ninamwachia Mungu Serikali kunidhulumu mashamba na viwanda vyangu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Ofisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL), Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema anamwachia Mungu suala la kampuni hiyo kupokonywa mashamba na mengine kuwekwa chini ya uangalizi na Serikali.

Hivi karibuni, Serikali ilitangaza kufuta umiliki wa mashamba sita yenye ukubwa wa ekari 12,915 yaliyopo Korogwe mkoani Tanga.

Pia, wiki iliyopita bungeni Serikali ilisema mashamba sita yanayomilikiwa na mfanyabiashara huyo bilionea yako chini ya uangalizi na kama atashindwa kutekeleza masharti yatafutwa.

Juzi, Mo akizungumza na Mwananchi mara baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya mwenendo wa timu ya Simba, alisema hayupo tayari kulizungumzia suala hilo la mashamba.

“Kaka naomba uniache tafadhali. Mambo mengine tumuachie Mungu,” alisema Mo kwa kifupi.

Mwezi uliopita, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiwa ziara wilayani Korogwe alitangaza uamuzi wa Serikali wa kubadilisha mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na kampuni hiyo.

Alisema mashamba yaliyofutwa ni yale yaliyopo eneo la Mombo, Mabogo na Kwalukonge wilayani Korogwe.

Naibu waziri huyo alisema uamuzi wa kufuta mashamba hayo umefikiwa baada ya mapendekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu.

Pamoja na mashamba hayo kufutwa wiki iliyopita bungeni, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii alisema awali mfanyabiashara huyo alipewa onyo kuhusu mashamba 12 kati ya 21 aliyokuwa akimiliki akitakiwa kuyaendeleza.

Alisema Serikali tayari imefuta hati za mashamba sita na kwamba bado sita ambayo yako kwenye uangalizi.

Waziri huyo alisema Tanzania ina mashamba makubwa 2,000 ya kilimo na ufugaji.

“Haijatokea nikapata agizo kutoka kwa Rais kuwa nifute hati ya shamba la mtu,” alisema Waziri Lukuvi.
 
MO hajaonewa na si wa kwanza yeye kufutiwa hati za umiliki wa mashamba kwa vigezo na sheria za nchi.....

Hata kama una mashamba lakini hujafuata vigezo vya umiliki wa hayo mashamba na ndiyo maana leo hii baadhi ya hati za mashamba yako zinafutwa.

Na kama umeonewa Mahakama zipo nenda kafungue mashitaka huko ili upate haki zako.kulalamika katika media hakusaidii kabisa.
 
mashamba ambayo hajaendeleza.. mapori
Kwahiyo ukinunua gari ukapaki nyumbani huendeshi unyang'anywe? Ukinunua TV ukaiweka ndani hutazami unyang'anywe?! Hivi mwenye mali si ndiye ana amua ni lini na kwa vipi atumie mali yake? Wewe ukimuuzia mtu nyumba unataka lazima alale humo? Tutumie akili huyu ntu alinunua kihalali kwanini anyang'anywe mali zake?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom