Mohamed Dewji: Ninamwachia Mungu Serikali kunidhulumu mashamba na viwanda vyangu


Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,950
Likes
30,768
Points
280
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,950 30,768 280
Ofisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL), Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema anamwachia Mungu suala la kampuni hiyo kupokonywa mashamba na mengine kuwekwa chini ya uangalizi na Serikali.

Hivi karibuni, Serikali ilitangaza kufuta umiliki wa mashamba sita yenye ukubwa wa ekari 12,915 yaliyopo Korogwe mkoani Tanga.

Pia, wiki iliyopita bungeni Serikali ilisema mashamba sita yanayomilikiwa na mfanyabiashara huyo bilionea yako chini ya uangalizi na kama atashindwa kutekeleza masharti yatafutwa.

Juzi, Mo akizungumza na Mwananchi mara baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya mwenendo wa timu ya Simba, alisema hayupo tayari kulizungumzia suala hilo la mashamba.

“Kaka naomba uniache tafadhali. Mambo mengine tumuachie Mungu,” alisema Mo kwa kifupi.

Mwezi uliopita, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiwa ziara wilayani Korogwe alitangaza uamuzi wa Serikali wa kubadilisha mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na kampuni hiyo.

Alisema mashamba yaliyofutwa ni yale yaliyopo eneo la Mombo, Mabogo na Kwalukonge wilayani Korogwe.

Naibu waziri huyo alisema uamuzi wa kufuta mashamba hayo umefikiwa baada ya mapendekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu.

Pamoja na mashamba hayo kufutwa wiki iliyopita bungeni, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii alisema awali mfanyabiashara huyo alipewa onyo kuhusu mashamba 12 kati ya 21 aliyokuwa akimiliki akitakiwa kuyaendeleza.

Alisema Serikali tayari imefuta hati za mashamba sita na kwamba bado sita ambayo yako kwenye uangalizi.

Waziri huyo alisema Tanzania ina mashamba makubwa 2,000 ya kilimo na ufugaji.

“Haijatokea nikapata agizo kutoka kwa Rais kuwa nifute hati ya shamba la mtu,” alisema Waziri Lukuvi.
 
F

Fursa Pesa

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2012
Messages
2,605
Likes
1,048
Points
280
F

Fursa Pesa

JF-Expert Member
Joined May 30, 2012
2,605 1,048 280
Kwani hapo zamani mashamba hayo yalikuwa ni ya nani?
Na je IRR ya waliokuwa wamehodhi bado haijafikiwa?
Vipi kuhusu muda na masharti ya hati miliki ya mashamba/ardhi hayo/hio una/ina semaje?
 
R

Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2017
Messages
838
Likes
723
Points
180
R

Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2017
838 723 180
Viwanda vya Nyerere hivyo. Yule Sir Chande aliwapendelea watanzania wenye asili ya asia
 
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
2,063
Likes
7,086
Points
280
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
2,063 7,086 280
Nyerere aliulizwa!, Anadhani ni mistake gani aliifanya katika utawala wake?

Akasema ni kutaifisha mashamba ya Mkonge!.

Leo hii Jiwe anataifisha mashamba ya Mkonge huku akiwa hana plan yoyote ya kuyaendeleza!

Wait and see matokeo yake!
 
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
2,063
Likes
7,086
Points
280
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
2,063 7,086 280
Watu wanaona kilichochukuliwa ni mashamba tu Vipi kuhusu Viwanda?.
Watamgawia nani?
 
Mzee Kigogo

Mzee Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Messages
1,639
Likes
1,978
Points
280
Mzee Kigogo

Mzee Kigogo

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2018
1,639 1,978 280
MO hajaonewa na si wa kwanza yeye kufutiwa hati za umiliki wa mashamba kwa vigezo na sheria za nchi.....

Hata kama una mashamba lakini hujafuata vigezo vya umiliki wa hayo mashamba na ndiyo maana leo hii baadhi ya hati za mashamba yako zinafutwa.

Na kama umeonewa Mahakama zipo nenda kafungue mashitaka huko ili upate haki zako.kulalamika katika media hakusaidii kabisa.
Hajalalamika kwenye Media bali amesema amemwachia Mungu. Soma vizuri habari
 
Ramadhan James

Ramadhan James

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2015
Messages
1,040
Likes
544
Points
280
Ramadhan James

Ramadhan James

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2015
1,040 544 280
Serikali wachukue tu, Haiwezekani muda wote huo hamjaendeleza alafu mnalalamika!
 
utukufu mwanjisi

utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2017
Messages
1,079
Likes
890
Points
280
utukufu mwanjisi

utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2017
1,079 890 280
Naona bavicha chumvi zinazidi sasa hadi kuongeza baadhi ya maneno ya MO kwenye heading "viwanda vyangu"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Interest

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Messages
1,752
Likes
2,883
Points
280
Interest

Interest

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2015
1,752 2,883 280
Mohamed Dewji: Ninamwachia Mungu Serikali kunidhulumu mashamba na viwanda vyangu!
 
Kaiche

Kaiche

Member
Joined
Jan 23, 2017
Messages
50
Likes
20
Points
15
Age
28
Kaiche

Kaiche

Member
Joined Jan 23, 2017
50 20 15
Kwahiyo ukinunua gari ukapaki nyumbani huendeshi unyang'anywe? Ukinunua TV ukaiweka ndani hutazami unyang'anywe?! Hivi mwenye mali si ndiye ana amua ni lini na kwa vipi atumie mali yake? Wewe ukimuuzia mtu nyumba unataka lazima alale humo? Tutumie akili huyu ntu alinunua kihalali kwanini anyang'anywe mali zake?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili za mikia hizi, acha ushabiki wa kipumbavu. Gar, au nyumba ndio ufananishe na hayo mapori,,, Athari zake unazifahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
C

christeve88

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2018
Messages
448
Likes
372
Points
80
C

christeve88

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2018
448 372 80
Waende na huko Babati vijijini yapo mashamba mengi tu yamegeuka mapori, halafu wananchi hawana ardhi wanageuzwa vibarua kwenye mashamba ya miwa.
 
K

Kifoi

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2007
Messages
918
Likes
286
Points
80
K

Kifoi

JF-Expert Member
Joined May 12, 2007
918 286 80
Kwahiyo ukinunua gari ukapaki nyumbani huendeshi unyang'anywe? Ukinunua TV ukaiweka ndani hutazami unyang'anywe?! Hivi mwenye mali si ndiye ana amua ni lini na kwa vipi atumie mali yake? Wewe ukimuuzia mtu nyumba unataka lazima alale humo? Tutumie akili huyu ntu alinunua kihalali kwanini anyang'anywe mali zake?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania ardhi yote ni mali ya serikali ya ccm mtu hawezi kumiliki ardhi TZ
 
cutelove

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Messages
1,001
Likes
1,472
Points
280
cutelove

cutelove

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2017
1,001 1,472 280
Baada ya kumaliza kuongea na wandishi wa habari kuhusu masuala ya timu ya Simba,Mwananchi alifuata kutaka kujua hatima ya mashamba yake

Mo akajibu"Hili suala la mashamba tuliache tu,ni kumuachia mungu"

My take :Hii kauli inaashiria maumivu anayopata Mo kutokana na vitendo vinavyofanywa na awamu hii ya 5,mara atekwe mara anyang'anywe mashamba,mara accounts zake zikaguliwe

Wakati ulaya na marekani serikali ziliwasapoti mabourgeoisie,wakaleta mapinduzi ya viwanda ulaya na marekani huku Tanzania wanaonwa kama ni watu hatari sana

Nani asiyejua mabourgeoisie kipindi cha marcantelism mbinu walizotumia kuacumulate wealth,hazikuwa fair,lakini hao ndo walisababisha ulaya kuwa kama ilivyo sasa ambayo kila mwafrika anatamani aishi ulaya

Ujamaa haujawahi kushinda duniani

2020 twende na LisuSent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,262,459
Members 485,588
Posts 30,122,935