Mohamed Bakari: Wabunge wawili wa CCM, Nape Nnauye (Mtama) na Hussein Bashe (Nzega Mjini) wamekomaa kisiasa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Dar es Salaam. Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mohamed Bakari amesema wabunge wawili wa CCM, Nape Nnauye (Mtama) na Hussein Bashe (Nzega Mjini) wamekomaa kisiasa na hata bungeni michango yao inaonyesha ukomavu.

Akizungumza baada ya kuombwa na Mwananchi kutoa maoni yake kufuatia kauli ya katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuwa wabunge hao vijana wanahitaji kupikwa, kusikilizwa, kuaminiwa na kusimamiwa, profesa huyo alikuwa na maoni tofauti.

Profesa Bakari alisema wanayoyafanya wabunge hao yanaonyesha ukomavu, lakini anachokiona ni mtendaji huyo mkuu wa chama kuwa hajakomaa kisiasa.

“Wanayoyafanya wawapo bungeni ni jambo jema na la kikomavu kisiasa kwa sababu wanaisimamia Serikali katika suala zima la uwajibikaji, sijaona baya walilolifanya, nawaona wamekomaa na ninachokiona Dk Bashiru ndiyo hajakomaa,” alisema Profesa Bakari.

Juzi, Dk Bashiru alifanya mahojiano na televisheni ya ZBC2 yaliyonukuliwa na Mwananchi jana akisema kuwa wanasiasa hao vijana wanapaswa kupikwa, lakini pia akasisitiza kuwa ni watukutu na wadadisi wawapo bungeni.

Akimtolea mfano Nape, alisema anahitaji kusikilizwa, kuandaliwa, kuamini na kusimamiwa.
Dk Bashiru alikuwa akizungumza katika mahojiano maalumu na Tido Mhando kupitia ZBC2 kuhusu Muungano uliotimiza miaka 55.

Hata hivyo, alisema wanasiasa hao wana mchango mkubwa katika chama chao.
Katika maoni yake, Profesa Bakari alisema vijana hao ni wakomavu.

Alisema katika kila chama kuna kitu kinaitwa nidhamu ya chama ambayo wanachama wanatakiwa kuifuata ili kuwapo na hali ya utengamano na wasitofautiane hadharani.

Alifafanua kuwa bungeni kuna kitu kinafanyika mara nyingi kuwa wale wasiokuwa wanachama wa baraza la mawaziri, wana nafasi ya kuhoji na kutoa maoni yao ndani ya Bunge, hiyo ndiyo bahati waliyonayo Nape na Bashe.

Alisema Nape na Bashe wanazungumza nje ya boksi na wamejitoa kwenye hali ya kukubali kila linalofanyika.

“Nawaangalia kama wanachama wakomavu na wanasimamia kile wanachoamini nje na ndani ya Bunge, wanaowaona hawajapikwa na wanastahili kupikwa zaidi, ni wasiofahamu misingi ya demokrasia na uwajibikaji,” alisema.

“Utakumbuka kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015, CCM ilipoteza mvuto kwa wananchi, katibu mkuu wa wakati ule, Abdulrahman Kinana na aliyekuwa mwenezi, Nape Nnauye walizunguka sehemu mbalimbali za nchi kuisema Serikali na uwajibikaji mbovu wa viongozi wa chama, jambo hilo liliwasaidia wananchi wakiamini tena chama hicho.”

Mbunge Bashe, akizungumzia kauli ya Dk Bashiru, alisema alichokisema katibu mkuu ni sahihi akitolea mfano kuwa kocha wa timu ya mpira jukumu lake ni kuendelea kufundisha wachezaji kufikia viwango anavyovitaka.

“Kuelekezana, kufundishana ni utamaduni wa kawaida viongozi wakubwa kufundisha wadogo, siyo kitu cha ajabu na ndiyo nguvu ya CCM,” alisema.

Alisema moja ya majukumu aliyonayo kiongozi aliyepewa nafasi ya kuongoza chama hicho ni kuendelea kuwapika viongozi wake na zipo hatua mbalimbali za kufanya, ikiwamo kupitia chipukizi na Umoja wa Vijana, hivyo siyo jambo jipya ni kawaida.

Licha ya kuulizwa maoni yake juu ya kauli ya Dk Bashiru, Nape alikataa kuzungumza chochote.
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbusho alisema, “ni vizuri zaidi kuambiwa na vijana hawa kuliko akisema Mchungaji (Peter) Msigwa (mbunge wa Iringa Mjini-Chadema) au (Joseph Mbilinyi-mbunge wa Mbeya Mjini-Chadema) Sugu hii ni afya na faida zaidi kwa chama,” alisema.

“Wakae naye (Dk Bashiru) awaeleze (Nape na Bashe) wapi panapoleta joto sana wapunguze, hilo linawezekana kwa sababu ni kijana mwenzao.”

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema kwenye chama chochote siyo vijana wote watakuwa na mawazo yanayofanana.

“Sioni ubaya kuweka wazi maoni yao, hawakubaliana na kila jambo, wana misimamo yao, sasa anaposema wapikwe sijui anataka wapikwe kwenye upande wa huo udadisi wao, tofauti na hapo nawaunga mkono asilimia 100,” alisema.

“Nawaambia waendelee na misimamo hiyo inaleta changamoto kwa chama tawala, hakipati ukosoaji kutoka upinzani lakini hata ndani ya chama ni jambo zuri katika misingi ya vyama vingi.”

Nape alipotafutwa jana aligoma kuzungumzia suala hilo, na Dk Bashiru mara zote simu yake iliita bila kupokelewa.
 
Mtasifia kila mtu ili kupinga sasa unamsafisha Nape na Bashe vijana ambao kutwa kuchwa mlishinda mkiwaponda enzi wakiwa madarakani.Ujinga mzigo
 
Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mohamed Bakari amesema wabunge wawili wa CCM, Nape Nnauye (Mtama) na Hussein Bashe (Nzega Mjini) wamekomaa kisiasa na hata bungeni michango yao inaonyesha ukomavu.

Akizungumza baada ya kuombwa na Mwananchi kutoa maoni yake kufuatia kauli ya katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuwa wabunge hao vijana wanahitaji kupikwa, kusikilizwa, kuaminiwa na kusimamiwa, profesa huyo alikuwa na maoni tofauti.

Profesa Bakari alisema wanayoyafanya wabunge hao yanaonyesha ukomavu, lakini anachokiona ni mtendaji huyo mkuu wa chama kuwa hajakomaa kisiasa.

“Wanayoyafanya wawapo bungeni ni jambo jema na la kikomavu kisiasa kwa sababu wanaisimamia Serikali katika suala zima la uwajibikaji, sijaona baya walilolifanya, nawaona wamekomaa na ninachokiona Dk Bashiru ndiyo hajakomaa,” alisema Profesa Bakari.

Juzi, Dk Bashiru alifanya mahojiano na televisheni ya ZBC2 yaliyonukuliwa na Mwananchi jana akisema kuwa wanasiasa hao vijana wanapaswa kupikwa, lakini pia akasisitiza kuwa ni watukutu na wadadisi wawapo bungeni.

Akimtolea mfano Nape, alisema anahitaji kusikilizwa, kuandaliwa, kuamini na kusimamiwa.
 
Kama wasemavyo wadau wengi..huwezi kuhisi baridi ukiwa ndani mvua ikinyesha kama unapokuwa unanyeshewa na mvua. Kauli ya Dr. Bashiru iko sahihi kama kauli ya Prof wangu Bakari. Ila Prof. kaongea uhalisia kama mtu huru na mchambuzi tofauti na Katibu Mkuu (KM) wangu ameongea maoni ya Chama sio matakwa yake. Ninauhakika angeongea Kama Prof. Bakari kama tu angekuwa sio KM wa CCM.
 
Huyu professor kaitendea haki Elimu yake na taifa. miongoni mwa wabunge waliokomaa kifikra na kiuzalendo ni nape na bashe. bashiru anajua siasa za kinadharia tu. hajui lolote Zaidi ya kutetea ugali wake.
 
Bashiru yuko sahihi kutokana na eneo alilosimama, kwa sasa ukiwa mwanaccm kumsifia na kumnyenyekea rais ndio kuiva.
 
Lkn kama ulimsikia vyema Dr. Bashiru hakua na nia inayotafsiriwa, alimaanisha namna ya utukutu wa hawa wabunge ni njema na wanafaa kwa matumizi ya baadae ktk uongozi
 
Back
Top Bottom