MOH kusomesha mtoto wa mkubwa UK ni uungwana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MOH kusomesha mtoto wa mkubwa UK ni uungwana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Olecranon, Nov 19, 2011.

 1. O

  Olecranon JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,371
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Ndugu wana JF,
  Ninajua kuna maswala mengi ambayo yako mbele yetu kwa ajili ya kuyajadili na kutafutia ufumbuzi. Lakini nimesikitishwa sana na list ambayo nimeona kwenye website ya wizara ya afya inayoonyoshe majina ya postgraduate students ambao watakuwa sponsored na wizara ya afya. List yenyewe ni hii hapa http://www.moh.go.tz/POSTGRADUATE-TO-BE-SPONSORED.pdf. Kilichonifanya niweke thread hii hapa ni kuwa Wizara imeamua kusomesha mtoto mmoja wa mkubwa UK ambaye kwa jina anajulikana SALAMA KIKWETE. Cha kusikitisha zaidi ukiangalia hitimisho la list hii kuna usemi huu: THOSE CANDIDATES WHO APPLIED FOR SPONSORSHIP FROM THE MINISTRY OF HEALTH AND SOCIAL WELFARE AND DO NOT APPEAR IN THIS LIST SHOULD CONSIDER THEMSELVES UNSUCCESSFUL .
  Je, ni wanafunzi wangapi zaidi wangesomeshwa hapa bongo kwa pesa hii itakayoyumika kusomesha huyu mtoto mmoja wa kigogo?
  Je, ni wanafunzi wangapi walipewa opportunity ku-compete na huyu mtoto wa kigogo kwa hii nafasi ya kusoma UK?
  Je, hatuna pediatric dentistry educators hapa bongo?

  Kama uliapply for sponsorship ukakosa na upo humu jamvini ni vizuri ukatujulisha ili tupate a true picture ya madakitari ambao hawakuweza kujiunga postgraduate kwa kukosa sponsor.
   
 2. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,396
  Likes Received: 10,610
  Trophy Points: 280
  jk alisema wanampango wa kusomesha PGs wengi akiwa newyork.cha kushangaza number ya PGs waliopata sponsorship ya serikali imepungua.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Tanzania zaidi ya uijuavyo.

  Nimeliona hapo Namba 30. Salama Kikwete Fedro Dentistry UK.
   
 4. A

  Ambassador goah New Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tnzania Tnzania nkpnd kw moyo wte......
   
 5. M

  Maega Senior Member

  #5
  Nov 20, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yaani hata mi nashangaa hii serikali hata hawaeleki wantumia vigezo gani. Kwa mfano Bodi ya mikopo vigezo vyao ni uwezo wa mzazi sasa mzazi wake na Salama yaan JK c ana uwezo! kwann wasimsomeshe mtoto wa mkulima badala yake? Kwan MOH wasingempa udhamini ina maana baba yake angeshindwa kumsomesha? Yaani mijitu pale MOH kwa kujipendekeza hadi kichefu chefu
   
 6. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  jamani muda mwingine tusiwe tunalalamika sana, hawa kwanza wengi ni waajiriwa chini ya hii wizara, halafu kama watu hawana admision za huko UK basi wawape tu scholarship? tuwe tunajishughulisha jamani , mbona yupo mmoja amepata toronto , canada hujamwongelea? Hata mimi mara ya kwanza nilikuwa na mentality kama yako kuwa aaaah ni watoto wa vigogo tu wanapata , siyo kweli niliwahi kujaribu na mimi nikapata tena UK. Tatizo ni kupata admision UK ndiyo tatizo , by the way masters yenyewe hapa UK ni mwaka mmoja tu.

  Wengi ya hawa wanafunzi wanafamilia tayari hivyo muda mwingine kwenda mbali sana inawawia vigumu.
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia list ya wanaoenda kusoma ni wengi sana na hata Salama Kikwete kuwemo si tatizo. Tatizo linakuja pale walipotoa nafasi moja ya UK na kumuweka mtoto wa Rais. Huu ni upuuzi na kujipendekeza kulikofanywa na watoa maamuzi wa Wizara. Japo hakuna justfication ya ubadhirifu ila ni dhahiri UNDUE INFLUENCE imetumika hapo na ni ktu kibaya sana. JK ana uwezo wa kumsomesha mtoto wake popote pale kwa kipato chake halali.

  Kama watoa maamuzi wa Wizara wangekuwa na open mind wangetoa angalau nafasi tano na kumjumuisha huyo Salama. OTHERWISE THIS IS CLEAR PREFERENTIAL TREATMENT. Ningekuwa mshauri wa JK ningekataa Salama kwenda UK peke yake. Hii ina undermine my presidency. Sihitaji preferential treatment toka kwa mtu yeyote yule.

  Ndiyo maana akina Madaraka Nyerere na Makongoro walikuwa wanachanganywa na nawatanzania wengine kuondoa dhana ya mtoto wa rais. Kwa hili MOH wamechemka period kwa kuonesha upendeleo wa wazi, na wanahitaji kumuomba radhi JK kwenye hili.
   
 8. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  jamani ktk kada ya afya kuna scholarship za kumwaga especially kwa post graduate.Za kina mama ndo usiseme maana hizo ziko nyingi mno.Hata ukitaka kwenda kusoma huko New Papua Guinea utapata sponsor tu hivyo hamna cha ajabu hapo.Huyo dada aliomba kama walivyoomba wengine hivyo tusilalamike tu bila kufanya uchunguzi
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ningekubaliana na wewe kama statement hii isingekuwepo
  'THOSE CANDIDATES WHO APPLIED FOR SPONSORSHIP FROM THE MINISTRY OF HEALTH AND SOCIAL WELFARE AND DO NOT APPEAR IN THIS LIST SHOULD CONSIDER THEMSELVES UNSUCCESSFUL '
   
 10. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Hebu nisaidie wewe, kwa ninavyofahamu mimi, pamoja na mambo mengine hususani suala la uwezo wa mzazi...lingine la msingi ni academic standing; na more often than not, hii inakuwa ndiyo priority ya kwanza na zingine zinafuatia. sasa assume umebaki na majina mawili, salama kikwete na salama kintukute....salama kikwete ana second upper na kintukute ana second lower; je, scholarship ungempa nani hususani ukizingatia scholarship sio favor?!
   
 11. O

  Olecranon JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,371
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  You just touched the point we are raising, which is, was she subjected to competition with other candidates or she was just awarded the scholarship merely based on her second/family name? My speculation is that this scholarship was created just for her, and I will retreat from this view if proved beyond reasonable doubt that this position was publicly advertized for other qualifying candidates to apply.

   
 12. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ni mtoto wa Rais, sifa anazo lakini ni mtoto wa Rais, watu wa MOH walipaswa kujua kitendo cha kumpa sponsorship Binti wa Rais pekee udhamini akiwa ni mwanafunzi pekee picha yake kwenye umma wakti wowote ingeweza kuleta picha kwa raia yoyote yule.Japo binti huyo anastahiki kama Mtanzania yoyote yule cha msingi ni kuwa amekidhi sifa za kupewa udhamini huo.

  Cha msingi kozi hiyo wangepelekwa japo watatu,lakini si katika unique way kama hii.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Olecranon, nakuomba usiingie kwenye long list ya 'hate preachers' wa humu jamvini.
  Kila Mtanzania kwanza ni Mtanzania ndipo mengine yote yanafuati ni jinsia gani, ni kabila gani, ni familia gani, ameolewa na nani etc. Kuwa mtoto wa rais, hakumuondolei haki yake kama Mtanzania mwingine yoyote.

  Bahati nzuri au mbaya, nimetokea kumfahamu huyu binti, Dr. Salama na pia nawafahamu baadhi ya watoto wengine wa JK japo sio wote nane, kwa opinion yangu, kati ya watoto wote wa JK ninaowafahamu mimi, Dr. Salama pekee ndie anaesimama mwenyewe kama Salama bila ile pride ya mtoto wa rais ambayo nduguze wanayo!. She is so humble na down to earth, fortunately kaolewa na kijana mwenye uwezo kumlipia shule popote, lakini huko hakumuondolei right yake ya kupata fellowship kama rai mwingine yoyote. Hata kama unatoka familia ya mamilioneo, kupata fellowship kunakuongezea heshima kwa sababu ili kuipata lazima uishindanie na wengine toka nchi mbalimbali duniani. Wizara sio determinant nani anapata, sponsors ndio determinant, japo recomendation ya wizara pia inanguvu.

  Kama huyo dr ana sifa, na ameomba kama Mtanzania mwingine yoyote, sasa ndio anyimwe eti kwa sababu ni mtoto wa rais?.

  Wanabodi, tuendelee kumsakama JK kwa maroroso yake, ya chama cheke na serikali yake, au tuwasakame watoto wake wanaofanya wanayoyafanya simply kwa sababu baba ni rais, lakini nawaomba sana tusiisakame familia ya rais kwa mambo yasiyohusika, hiyo scholarship ni issue ya proffesionalism hata kama preferential ime play part lakini she deserves and she is capable!

  Please leave her alone!.
   
 14. u

  utantambua JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hahahaha pro magamba wapo bize kutetea hapa mpaka raha yaani wanavyovuja jasho kutetea visivyoteteeka.
   
 15. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,812
  Trophy Points: 280
  sina la kuongeza mkuu .... u have said all ...
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Iko siku haya yatajibiwa hadharani mkiangalia kwenye runinga .KM wa wizara lazima alipe fadhil kama hapakuwa na haki for sure .Mie yangu macho .
   
 17. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  tungepata na list ya waliokosa na qualification zao tungekuwa kwenye better position to judge.,pasco hapo juu unaongea kihisia zaidi labda siku moja alikusalimia kwenye corridor basi amekublind.
   
 18. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Siku nyingine muwe mnafanya karesearch kidogo kabla ya kuja ushuzi wa kupreach chuki.

  Huyo binti ni daktari, na ana uwezo wa kitaaluma na anataka kujiendeleza kwenye fani adimu, na
  inaonesha anapenda kushindanishwa,...na ikumbukwe nchi nzima wataalam wa pediatric dentistry
  hawafiki watano, ila kwa vile baba yake ni JK, ishakua nongwa!

  Tumkosoe JK kwa mapungufu yake mengine jamani, kwa hili hapana TUMEZIDI!
   
 19. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Pasco tafadhali ongea vitu unavyovifahamu. Gharama atakayolipiwa salma Uk ingetosha kusomesha specialists wengine 7 tanzania ambapo kozi anayoenda kusomea inatolewa pia Muhimbili na ninafahamu watu wanaosoma kozi hiyo Muhimbili (paediatrics dentistry).

  Kama ni kusoma nje angejipeleka kwa private sponsorship ili pesa nyingine zitumike kugharamia watanzania wenye uhitaji. Nasisitiza angeweza kusoma Tanzania kwa gharama nafuu. Kama hujui wizara ndio wanaoamua nani anapata sponsorship na nani hapati, tena kwa vigezo wanavyojua wao.

  Nimesikitishwa sana na mtoto huyu kulipiwa na wizara nje. Tunahitaji madaktari bingwa wengi, tungetumia kasungura ketu kadogo kupata specialists wengi.

  Kwa sasa tuna tatizo kubwa sana la vifo vya akina mama na watoto, tunahitaji madaktari bingwa wengi kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama hawa. wanafunzi wa masters katika fani ya udaktari bingwa wa watoto waliodahiliwa na chuo kikuu Muhimbili mwaka huu wa masomo walikuwa 17, wizara imetoa udhamini kwa wanafunzi sita tu, 11 wamekosa udhamini, kwa hiyo watu hao hawawezi kuwa madaktari bingwa na akina mama wataendelea kufa. Hapo hapo mtu mmoja anaenda kusomeshwa UK kwa gharama kubwa kozi ambayo inapatikana hapa nchini na ambayo nadhani sio priority ukilinganisha na hao walonyimwa mikopo. Kma kweli ni mzalendo angesoma hapa hapa ili pesa nyingine zitumike kusomesha wenzake.

  Naomba nieleweke sina tatizo la yeye kupata udhamini, tatizo langu ni yeye kwenda kusomeshwa UK na wengine wakakosa kabisa udhamini. Baba mwenye watoto wawili kumlipia mtoto mmoja UK na akashindwa kumlipia mwingine kabisha wakati angeweza kuwalipia wote hapa hapa huo ni ujuha. She might be capable lakini upendeleo umetumika.
   
 20. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mahela ya Baba yake nanafanya kazi gani?
   
Loading...