Modems (contd.)

Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,234
531
Tangu tumepata hizi modems imekuwa tabu sana, ila tuvumiliane. Hakuna anayependa kubanwabanwa. Sio kwamba hazifanyi kazi; tunataka ziwe huru.

Tatizo:

Ku-unlock ZTE modems unahitaji kuondoa ISO iliyopo ili utumie ISO ambayo iko unlocked, na hii unlocked ISO unaisanikisha kwenye memory card. Sawa? Sasa zipo hizi modem Vodafone K3570-Z (ZTE) tatizo ni kuwa hazina sehemu ya kuweka memory card. Memory yake ni ROM kama inavyodai --- huwezi kufuta au kuandika chochote ndani yake.

Nikubali kushindwa?
 
hakuna kisichowezekana kama ilikuwa Locked basi jua inaweza kuwa unlocked. may be kwa kupdate something like firmware ya Modem. au hata ku update ROM yenyewe. There must be me work around.

Kama una muda na unahobby na mambo ya teknolojia uki google utapata suluisho. Alafu nadhani simcard kwenye hizo model zimefichwa sehemu isiyokuwa rahisi kuona. Chunguza vizuri.

Hakuna simu inaweza kufanya kazi bila simcard na hivyo hivyo in this case hata modem.

Ebu jaribu kucheki hii video kama inawe kukupa concept
 
Last edited by a moderator:
ilikuwa Locked basi jua inaweza kuwa unlocked.
Sometimes impossible especially kama process ya kutengeneza ROM ilikuwa ni blowing of fuse or transistor. Lakini kama firmaware can be upgraded then sio ROM bali ni PROM/EPROM/EEPROM :target:
 
jamani moderm yangu ni ya voda huwawei, hii nayo procedure zake za kuichakachua ni ngumu? naomba mnielekeze ingawa mi si fundi sana nitajaribu.
 
Binafsi, nadhani hizi link zote za humu JF zinazoeleza namna ya kuchakachua Modem aidha ni za zamani na hazijakuwa updated ama kuna mahali zinatofautiana kati ya za huko na hizi za haya makampuni yetu ya simu. Wikiendi iliyopita nilijaribu kutumia link zote zilizoko humu ndani pamoja na msaada wa wanaJF kuchakachua Modem yangu ya Voda E220 iwe pia inakandamiza Zain/Airtel lakini hamna kitu. Procedure zoote zinafika mahali zinakwama! Ni wangapi humu Ukumbini wana Modem za Voda E220 wamezichakachua na sasa wanaweza kuzitumia hata na Airtel kupata Internet?? Walifanyaje??
 
kuna hizi software utahitaji:

  1. XV132 Hex Editor inapatikana hapa
  2. PSAS ambayo utaipata hapa
  3. e220 SIM lock Unlock nayo unaweza kuigugol tu, utaipatahttps://www.jamiiforums.com/hapa
Halafu fuata maelekezo yaliyopo hapa. Jaribu hii, mimi sijaijaribu ila nadhani itafanya kazi.
 
Back
Top Bottom