Mochwari: Chimbo muhimu la wachawi na waganga

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,605
696,697
Mojawapo ya kazi ngumu duniani ukiachana na zile zinazotumia nguvu ni hii kazi ya mochwari! Kushinda ama kukesha kwenye chumba kilichojaa miili iliyonyamaa na kutulia tuli....kuandaa mwili wa marehemu ili uweze kuwa na sura inayotazamika mbele ya wafiwa.....lakini kubwa zaidi unapopata tenda ya kunyofoa kiungo/viungo vya marehemu kwa shughuli za kishirikina
Kuna biashara za siri zinaendelea kule...watu wanapiga hela na maisha yanaendelea
Maiti inatisha na kuna watu ni waoga kupitiliza! Hawa hupendwa mno na wahudumu wa mochwari! Mnatoa pesa na nguo ili awasaidie kumuandaa marehemu wenu......wahudumu wasio waaminifu hufanya yao kipindi hiki
6003a035dc853c2eb8110957b21f2c29.jpg

Usiku mmoja mochwari si kitu rahisi hata kidogo!
Watakuja wachawi
Watakuja wanga
Watakuja wapiga dili za kitapeli
Watakuja wala nyama za wafu
Watakuja wataka viungo kwa shughwuli wanazojua wao
Watakuja wanaotaka maiti kamili ya mtoto binti kijana mtu mzima nk nk....wote ni wako hawa
Wanga na wachawi watakuja na vitisho hasa kama uko fit kiasi fulani, utafanyiwa michezo mpaka uikimbie mochwari, hawa wengine watakujia live kwa cash money na baadhi watakutisha vyovyote vile
Usiku wa mochwari ni dunia nyingine kabisa. Yenye mambo yasiyoelezeka yakaeleweka kwa urahisi. .ni dunia yenye mtifuano mkubwa wa kiroho na uvutano wa dunia halisi
Pale ndio kituo cha kwanza baada ya roho kutengana na mwili...kwahiyo kuna vurugu mechi kubwa hasa kwa vile vifo vya kishirikina ugomvi dhuluma na zile roho ambazo bado zilikuwa haziko tayari kuachana na mwili....!!! Asikwambie mtu makaburini kuna nafuu kuliko mochwari
Mochwari kuna maiti hununa hucheka hukasirika husogea husonya na mambo mengine mengi ya ajabuajabu lakini muda nwingine yakichombezwa na wachawi na wanga!
Hata hivyo pamoja na changamoto zote hizi, bado inabaki kuwa kazi kama kazi nyingine tu ILA ukimuona mhudumu wa mochwari MHESHIMU sana! Kazi yake imebeba siri kubwa
 
Weee Mshana!. Wee noma. Ujue watu mishale hii wanasoma post kama hii hadi usingizi unawapotea.
Mwanadamu kaumbwa na hofu ya Mungu. Kaumbwa na huruma pia hivyo roho ilitolewa huruma na hofu huweza kufanya lolote bila hofu.
Imagine mida hii unainyemelea maiti na kisu chako mkononi ili uikate kiungo fulani lakini ghafla inafungua macho
 
Kuna watu huwezi beba kiungo chake kwa mambo ya utamaduni.
Kuna jamaa walifukua maiti ya ajali wakaenda porini kuchoma wapate mafuta na mengineyo usingizi ukawazidia wakaamka wakakuta ni majivu tu hawakuambulia kitu.
Dunia duara.
Marehemu aliwahurumia mno. . . kuna watu walipewa million tano tasilimu wakanunue maiti.....wakapata moja kwa bei poa sana wakaifungasha wakaondoka! Kufika kwa tajiri kilichotoka ni joka
 
Nakumbuka moja ya Visa ulivyoviadithia ukiwa mfanyakazi wa Mochwari.

Kuna maiti ya Kiume ilikuwepo hapo, lakini punde ikaletwa maiti ya msichana mrembo sana, mlimbwende mwenye umbo maridadi. Kipindi cha Uhai wake alikuwa mrembo haswa, alivutia mno.

Cha Kushangaza, baada ya ile maiti ya Kike kufika, ulipoanza kumuandaa umueke katika eneo lake, ulimlaza pembeni ya ile maiti ya mwanaume....

Maiti ya Kiume ikasimamisha Dushelele hahahaha!. Anataka mambo hata kama ni mfu tayari.

Ndipo ujue, vita ya mwanamke mrembo haijawahi kumuacha mtu salama. Hata mfu atamtamani tu....
 
40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom