Mo Safi Mafuta ya kula rahisi kuibiwa na kila mtu, TBS mko wapi?

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
2,328
2,282
Habari wana jamvi? Rejea kichwa cha uzi juu hapo.

Kwanza kabisa nampongeza kijana mwenetu kwa bidii katika kazi aliachiwa na babake, Mo anakuja vizuri sana katika kila bidhaa kiasi kwamba Azam anaweza kuomva poo muda wowote,amejipatia sifa kutokaba na kuboresha vile vilivyopo sokoni na hata kuviongezea ujazo zaidi. Shida imekuja tu hapa.
Kwa wale ambao tayari wamenunua au kuona kifungashio cha mafuta ya Mo safi washaona hili tatizo, kwanza sokoni ndio mafuta ya mwisho kuuzwa (yananunuliwa baada ya mengine kuisha)
1071959

Mifuniko ya mafuta haya tunaweza kusema hayana seal, mtu anaweza kufungua akapunguza, akachanganya na kitu kingine na kufunga upya bila kujulikana.
1071960

Mamlaka zinazohusika sijui kwanini hawaoni hatari hii.
1071962

Vipi mtu akifungua na kuweka sumu, atauwa wangapi?

FAIDA KWA MO YA KUDHIBITI JAMBO
Vipi mpinzani wake kibiashara anaamua kutumia njia hiyo kuchezea rafu? Serikali haijapiga marufuku hayo mafuta? Mambo mengine tusiangalie urahisi tu, angalia na jamii pia.
 
MO yuko vizuri kwenye biashara zake, lakini mara nyingi naona hatulii kabla hajaamua kuanzisha jambo. Labda pressure ya ushindani.

Sasa mafuta kweli uyafunge namna hii mtu makini ayanunue kweli!!!! Wakati hata hayo yenye seal wahuni wanakata, wanafyonza wese vikombe kadhaa, kisha wanafunga tena seal.
 
Hata mafuta yaliyomo kwenye ndoo za lita kumi kama Sundrop hufunguliwa kwa kubangua mfuniko na kupunguza ujazo au kuweka mafuta mengine tofauti. Kwa ujumla mafuta yote vifungashio havina ubora na TBS hawana muda wa kusimamia viwango. Unajua viwango vya mikate havistahili kuwepo kwani hakuna mkate wenye ubora wa kuitwa mkate, jambo hili pia linahusu ubora wa vifungashio vya maji ambavyo hubanguliwa kirahisi na kuwekwa maji yasiyofaa.
 
MO yuko vizuri kwenye biashara zake, lakini mara nyingi naona hatulii kabla hajaamua kuanzisha jambo. Labda pressure ya ushindani.

Sasa mafuta kweli uyafunge namna hii mtu makini ayanunue kweli!!!! Wakati hata hayo yenye seal wahuni wanakata, wanafyonza wese vikombe kadhaa, kisha wanafunga tena seal.
Fact mkorinto, kutulia katika biashara ni Jambo la muhimu kuliko kila kitu, unaweza fungua hundreds of product line....na watu Waka take advantage, scaling ktk business inahitaji umakini, nampongeza Sanaa MO mfanyabiashara mwenye vision Tanzania ila Sasa nahisi watu inside MO enterprises wanamhujumu, ukiangalia si mafuta tu Hadi bidhaa Kama sabuni Tena hizi za maji za kuoshea vyombo ni Kama wana wanakusanya makopo na au seal then wanaweka sokoni, nafaka nazo the same thing.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye mwenyewe kwake hatumii maana anajua hayafai na TBS wanafanya mambo kwa mazoea tu,so hana haja ya kuhangaika na vifungashio
 
Yaani wanauza bidhaa nyeti kama hiyo bila seal?! Hii haiwezekani, ni bora mtu aibe lakini kuna wengine wanaweza wakaweka hata sumu humo, hi ni hatari sana!
 
Seal haizuii watu kufanya mambo,konyagi za uchochoroni zipo nyingi na hizo za uchochoroni zina seal kama kawa
 
MO yuko vizuri kwenye biashara zake, lakini mara nyingi naona hatulii kabla hajaamua kuanzisha jambo. Labda pressure ya ushindani.

Sasa mafuta kweli uyafunge namna hii mtu makini ayanunue kweli!!!! Wakati hata hayo yenye seal wahuni wanakata, wanafyonza wese vikombe kadhaa, kisha wanafunga tena seal.
Kweli kabisa mkuu, lakini afya za watu ni muhimu sana kuliko huo ushindani wake, akila ban ataweza kushindana kweli?
 
Yaani wanauza bidhaa nyeti kama hiyo bila seal?! Hii haiwezekani, ni bora mtu aibe lakini kuna wengine wanaweza wakaweka hata sumu humo, hi ni hatari sana!
Kweli kabisa bora mtu apunguze kuliko kuweka sumu na kuumiza afya za watu
 
Back
Top Bottom