Mo ndiye hataki kuweka Tsh. bilioni 20 au Serikali ndiyo hairusu mtu mmoja kuwekeza kwenye hivi vilabu?

vieira77

Member
Apr 10, 2014
61
45
Nimekuwa nikifuhatilia kwa muda sana linapofikia swala mtu kutaka kuwekeza kwenye hivi vilabu vya Yanga na Simba panapofikia Mwisho kabisa mchakato kukamilika panatokea mkwamo tena kwa wale wale waliokuwa wanataka mabadiliko mbaya zaidi kufikia hata kutoleana maneno makali ya kutishiana, mfano ni juzi tu malumbano kati ya Kigangwala na Mo ambayo kimsingi huyu mmoja ni Waziri kabisa ila ni wa kwanza Kuanzisha malumbano kwamba Mo aweke B20 na Kwanini Mo haweki? Amekwama wapi na kwa nini?

Kuna vitu vingi vyakujiuliza, kwanza mimi kwa upande wangu nimekuwa nikijiuliza Serikali kweli wapo tayari hivi vilabu vimilikiwe na watu binafsi?

Kama hawapo tayari Kwanini wasiwe wazi tu tukajua ili tuwe washangiliaji tu ila maendeleo tujue hakuna. Niliwahi kumsikia nadhani alikuwa Katibu mkuu wa BMT Bw Kiganja kwamba hizi Team ni za Serikali kahanzisheni za kwenu ila naona Mo yeye kakomaa kaenda karibu nakufika mwisho nakumbuka Mwakembe alisema hanaruhusiwa kumiliki asilimia 49 badae tena akasema hizo 49 inatakiwa wawe watu wasiopungua 3 sasa najiuliza kama Serikali imeamua hivyo mbona naona Simba na Mo wanajidanganya kwani bado kuzimiliki hizi Team ambazo ni Simba na Yanga haiwezekani

Wachambuzi wa mpira Bongo semeni ukweli msituzungushe ukweli unauma ila ni bora .
 
No alishasema,wanachama ndiyo wenye hisa nyingi,hivyo wanachama watoe kwanza hizo pesa,na yeye atatoa zake,ili zichanganywe kwa pamoja na ziwekwe kwenye akaunti maalumu,ndipo zipangiwe matumizi na kuleta maendeleo ya simba.
 
Mwakyembe ndio tatizo sijui aliwezaje kupata phd au kuwa mwalimu wa sheria ujinga wake alioufanya kwenye richmond kauleta kwenye mpira.
Kwa kifupi alishindwa kusimamia sheria akaingiza siasa kwani sheria inasema kwa timu kama Simba na yanga zilizoanzishwa na wananchi mwekezaji anaruhusiwa kuniliki si zaidi ya asilimia 49 na asilimia hizo zimilikiwe na watu wasiopungua watatu.
Inawezekana mo anasita kuweka pesa kwani akija kiongozi mwingine atakayesimamia sheria wakati yeye keshaweka pesa nyingi atakula hasara.
 
Back
Top Bottom