MO Ibrahim Governance Index Ranks Tanzania 15th in Africa

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
113
Tanzania attained 15 spot in 2001 before it slip well down to 21 in 2005. From 2006, the country experienced ups and down before attains its 15th spot in 2009.

However, the general observation from the index shows that while most of the countries have made progress in economic and health gain but the reverse trend is widely seen on the rule of laws and corruptions. For the countries which have recorded peace stability such as Tanzania, the performance of human development has been noted relatively poor in its region.

For Africa countries the top 5 are Mauritius, Seychelles, Botswana, Cape Verde and South Africa and the bottom ones are Somalia, Chad, DR Congo, Zimbabwe and Eritrea.

The modality of the index works on the scale of 0 to 100 with the higher performing countries rated closely to 100.

For the East Africa, Tanzania is leading followed with Uganda (24), Kenya (27), Rwanda (31) and Burundi (32).

Source: http://www.moibrahimfoundation.org/en/section/the-ibrahim-index/scores-and-ranking
 
Soma na uelewe:

Ranked 15th in the continent, Tanzania is the best governed country in EAC, followed by Uganda (24), Kenya (27), Rwanda (31) and Burundi (32), the Mo Ibrahim 2010 Index country rankings.
 
inatia moyo na matumaini ya maendeleo kwa nchi yetu, hivyo hongera serikali yetu uzi huo huo na sisi tuko pamoja nanyi! Sio tuongoze afrika mashariki tu bali tunataka tuongoze bara lote la afrika!
 
haya ndiyo tunayotaka kusikia!! tangu nijiunge juzi katika jf kwa kweli nilikuwa naogopa kuchangia maana utafikiri kuna vita hapa!! oo tuta mwaga damu, oo sijui nini!! sasa mpaka serikali yetu inasifiwa na kuongoza kwa utawala bora kwanini sisi wananchi tusiisifu?
 
haya ndiyo tunayotaka kusikia!! tangu nijiunge juzi katika jf kwa kweli nilikuwa naogopa kuchangia maana utafikiri kuna vita hapa!! oo tuta mwaga damu, oo sijui nini!! sasa mpaka serikali yetu inasifiwa na kuongoza kwa utawala bora kwanini sisi wananchi tusiisifu?

Zubeda usijali, wewe ongea unachotaka kuongea.

Huonekani kwa sura wala mtaa unaoishi. Achana na baadhi ya members wa JF waliokwenye payroll ya CHADEEMA, wewe kata ishu. Neno demokrasia kwa members wa CHADEMA walio JF halina maana yeyote.

Kwa taarifa yako jazba za member wa CHADEMA hapa ndizo zinazozifanya threads za Malaria Sugu zipendwe na wengi. Heshima ambayo mara zote nitampa Malaria Sugu ni uwezo wake wa kutorudisha matusi na badala yake kuja na hoja hadi hoja. Sijui kama ningeweza kuvumilia matusi anayopata Malaria Sugu.
 
Utawala wa jk kama unaonekana unafanya la maana mbele ya macho ya dunia ni uvimilivu wa kisiasa. Na hii siyo matokeo ya ccm wala serikali yake bali ni hulka ya watanzania tangu uhuru ya kutopenda makuu. Uganda na Kenya bado hakujatulia kisiasa ndiyo maana kwa vyovyote vile sisi tunaonekana bora kuliko wenzetu.

Kwa upande wa uchumi, sielewi ni vigezo gani vimetumika lakini huwezi kwa namna yoyote ile kulinganisha uchumi wa nchi yetu na Kenya. Kwa taarifa yenu tu, Kenya ni nchi ya pili kwa uwekezaji nchini Tanzania ikiongozwa na Afrika Kusini. Na sasa wamepitisha Katiba mpya ambayo ndiyo msingi mkuu wa maendeleo yao kiuchumi na kijamii. Vivyi, hivyo, kwa upande wa Uganda tatizo ni siasa tu ndiyo iliyowaangusha. Museveni bado anatumia vyombo vyake vya dola kunyanyasa vyama vya siasa jambo ambalo halileti sura nzuri mbele ya jamii ya kimataifa. Lakini kwa upande wa uchumi, Uganda inakwenda vizuri sana ikilinganishwa na sisi waTZ. Ni hivi karibuni tu, mafuta yamegundulika nchini Uganda na wanajiandaa kupaa kiuchumi.

Tatizo letu waTZ ni kujivunia sifa bandia za vyombo vya kimataifa kuhusu utekelezaji wa masuala mbalimbali bila kujali hali halisi ya wananchi wetu wengi. Mtanzania wa kawaida leo ukimwambia uchumi wetu unakua hatakuelewa unaongelea Tanzania ya wapi. Kama wakati wa uongozi wa Mhe. Mkapa sukari ilikuwa inauzwa Sh 600 na leo Sh 1800, unga wa mahindi ulikuwa ni Sh 230 leo Sh 700, n.k. Bidhaa hizo na nyingine nyingi ndizo anazokutana nazo mwananchi wa kawaida kila siku. Unapomwambia uchumi unakua kwa kweli kwake ni tusi.

Kwa upande wa Wanyarwanda ambao eti tumewazidi sana hadithi ni nyingine kabisa. Kwa sisi tunaoifahamu Rwanda, tunaelewa vizuri namna nchi inavyosonga mbele kiuchumi na hata kijamii. Leo hii ukifika Rwanda, unaanza kuona tofauti ndogo sana kati yake na baadhi ya nchi Ulaya. Wananchi wake wanachakalika kwelikweli kujenga nchi yao na uchumi wake ni mzuri sana. Mazingira yake kwa ujumla ni masafi sana tofauti na nchi yetu ambapo uchafu umetapakaa kila mtaa na viongozi wetu wanapita kujali. Sasa leo ukiwaambia wanachi wa Rwanda eti nchi yenu haifanyi vizuri kwenye matokeo ya Mo Ibrahim sijui kama watakuelewa na Mo yako hiyo.

Ninachotaka waTZ wenzangu wanielewe ni kwamba nchi yetu ina rasilimali nyingi za asili na mazingira mazuri kwa shughuli za kiuchumi lakini tunachokosa ni uongozi wa kuunda na kusimamia sera nzuri za kuwaletea wananchi maendeleo. Tatizo la viongozi wetu ni kutekeleza sera zinazoletwa na mataifa makubwa. Tatizo hili aliwahi kuliongelea Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alipokuwa anapinga ubinafsishaji wa benki ya NBC.

Kwa ujumla, matokeo ya Mo Ibrahim hayana maana yoyote kwa mtanzania wa kawaida.
 
Yaani kushika namba 15 out of 30 ndio jambo la kujivunia? Mmeishiwa wote!
 
Yaani kushika namba 15 out of 30 ndio jambo la kujivunia? Mmeishiwa wote!
Unajua hawa jokers bana haweshi vituko! mie nilidhani imeongoza walau hata ka-index kamoja kumbe HOLLA! nways, hizo ranks mara nyingi ni za UWONGO kwa sababu in Afrika mojawapo ya matatizo sugu ni uwepo wa reliable statistics. Thats the bottom line.
 
Hiyo Mo Ibrahim Index ni reliable kiasi gani?

Sielewi kabisa hayo yanayosemwa. Labda wenye hiyo index nao wanakuwa influenced na vijisenti?
 
Mnashangilia nini nyinyi vibaraka wa CCM? Mnazijua indicators ambazo MO wamezitumia? Cha kwanza angalia sarafu ya Kenya na yetu ipi ina thamani? Kenya they can fight for their right hapa tunaweza? Mnachekea ujinga wenu...

Mngeuliza vigezo gani vimetumika kufanya tafiti hizo au msome kwenye internet then ndo mje kulalalama, usikute watu kama nyie hata report ya MO hamjasoma ila mmesikia redioni tu sentence moja. fanyeni analysis kwanza.
 
HONGERA UTAWALA WA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUSHINDA TUZO LA MO IBRAHIM 2010


nadhani shida itakuwa ni kiingereza, imeandikwa wapi kuwa mmeshinda tuzo ya Mo? Acheni emotions zinazowafanya msielewe mada!
 
unga wa mahindi ulikuwa ni Sh 230 leo Sh 700, n.k. .


Mkuu Unga wa mahindi ni sh 900 sasa hivi. Jiji limejaa taka, ma plastic kila mahali, bara bara vumbi tu....pale manispaa along morogoro road (maeneo) pavement zinashindikana, jamani utawala bora wa wapi?

Mafisadi na mikataba mibovu kila mahali eti utawala bora..inasikitisha! Wabongo wengi elimu ni ndoto, ukiongea na watu mtaani unaona aibu mwenyewe kwa ajili ya uelewa finyu wa mambo..eiti Serikali inasifiwa! Loh, nchi hii imerogwa si bure! Watu wa nje ni wanafiki, wanawasifu ili waendelee kuwaibia!

This is nonsense and hypocricy of the highest order!
 
Inasikitisha kutoa taarifa za kuipongeza serikali ya JK kwa kuongoza wakati hata kumi bora imechemka, lol!
 
Back
Top Bottom