Mo Dewji toa billion 20 ambazo zipo kimkataba, acha kutengeneza mazingira ya kuonewa huruma na ujanja ujanja

Hisa ni unapewa sehemu ya umiliki, kama mimi namiliki gari, halafu nakuuzia wewe sehemu ya umiliki kwamba tunamiliki kwa ubia, mimi nitoe pesa ya nini tena?
Hivi unajua unacho kizungumza mkuu, hebu rejea kwenye maelezo juu ya mchakato wa mabadiriko ya klabu. Mali ni dhamana kwenye uwekezaji. Ndio maana upande wa simba hisa zake zitagawanywa na kuuzwa kulingana na thamani ya klabu, pesa hiyo itakayo patikana itakuwa sehemu moja na ile ya upande wa mwekezaji mwenye hisa 49%. Kiufupi hisa ni umiliki unaokupa wajibu wakuchangia mtaji kwenye sekta ya biashara na faida itakayo patikana hugawanywa kwa wanahisa
 
UTOPOLO BHANA!! sasa atatoaje wakati mchakato haujakamilika, na una dosari na upande wapili wataweka lini maana MO anatoa b 20 kwa hisa 49% so upande wa simba nao inatakiwa waweke pesa zao. Propaganda za kiutopolo huwa hazi zai matunda Katu!!.
UTOPOLO MTAJIJU!!😁😁
Kwani memorandum of understanding, ilikuwa inasemaje? Kwa kukusaidia ilikuwa inasema kuwa muwekezaje ataweka hiyo bilioni 20,kwenye escrow account ndani ya miezi mitatu tu!! Tukubali huu uwekezaji una tatizo, tusiendeshwe na ushabiki, na changamoto nyingi zinaweza zikawa ni za mfumo uliokuwepo sasa kuuunganisha, ndio shida ipo hapo, ndio maana sasa unaona simba inaendeshwa kana kwamba mchakato umeshakamilika wote!!
 
Hivi unajua unacho kizungumza mkuu, hebu rejea kwenye maelezo juu ya mchakato wa mabadiriko ya klabu. Mali ni dhamana kwenye uwekezaji. Ndio maana upande wa simba hisa zake zitagawanywa na kuuzwa kulingana na thamani ya klabu, pesa hiyo itakayo patikana itakuwa sehemu moja na ile ya upande wa mwekezaji mwenye hisa 49%. Kiufupi hisa ni umiliki unaokupa wajibu wakuchangia mtaji kwenye sekta ya biashara na faida itakayo patikana hugawanywa kwa wanahisa
Mimi siufahamu huo mkataba wala unachosema, nimeongelea concept ya hisa objectively; sasa kama huo mkataba unamtaka hadi mmiliki wa awali wa 100% ambae sasa amegawa sehemu ya mali yake kwa Mo at a fee ya 20billion na bado yeye tena anatakiwa atoempesa basi huo mkataba ni wa Kifisadi, uchunguzwe.
 
Hiyo B20 sielewagi walikubaliana kutoa yote kwa mkupuo au kwa awamu, maana MO alisema anatoa kwa awamu sasa nani yupo sahihi, utopolo tuacheni tukawatafutie viti maalum vya club bingwa
 
Si bure utakuwa una uhusiano na Amsterdam 😂 😂 😅

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Nielewe nin mkuu? Mo ni mwanachama halali wasimba yupo hapo kama ambavyo wanasimba wengine wanavyoweza kuwepo. Kwan katiba ya simba inasemaje mkuu?!
Kuwa mwanachama halali sio sababu ya kutaka kufanya mambo bila kufuata utaribu, sababu za vilabu vya ulaya kuwa na ukwasi mkubwa huu utapeli unaofanywa na mo dewji walishauacha mda sana
 
Mimi siufahamu huo mkataba wala unachosema, nimeongelea concept ya hisa objectively; sasa kama huo mkataba unamtaka hadi mmiliki wa awali wa 100% ambae sasa amegawa sehemu ya mali yake kwa Mo at a fee ya 20billion na bado yeye tena anatakiwa atoempesa basi huo mkataba ni wa Kifisadi, uchunguzwe.
Labda unisaidie kitu kimoja, juzi MO alinukuliwa akisema kwamba thamani ya hisa zitakazo uzwa kwa wanachama wa simba ni sh mil 400 kwa hisa 1%, so kwa logic yako hapo juu fedha za mauzo ya hizo hisa zinatofauti gani na b 20 za Mo kwenye uwekezaji kwa Simba sc?
 
Ni Tanzanian pekee mwekezaj anaanza kunufaika matunda ya kampuni bila hata ya kutoa ela ya umiliki (hisa) haya ndo maajabu ya afrika

Na mwekezaj anapoambiwa ela ya umiliki wa hisa anakua mbogo, swali la kujiuiza mo dewji ameachwaje miaka mitatu bila hata ya kuchukuliwa hatua na mamlaka husika.

Mfano timu za ulaya huwezi enda miliki timu kienyeji enyeji na kijanja Kama anavyofanya Mo dewji, na lazima kuwe na uwazi juu ya mikataba inayoingia, mfano jezi ya Simba imejaa matangazo ya dewji je ni shilingi ngapi timu inapata.

Kwa nchi nyingine dewji angetakiwa apigwe penalty, na billion 20 sio kuja kusema Mara timu inapata hasara hizo ni janja janja.

Simba na Yanga ziko Kama zilivyo na zitabaki Kama zilivyo Kama zikiendelea na wawekezaj Kama dewji au Manji, na hata gsm anachofanya Yanga ni njia zile zile za kienyeji enyeji
Amini nakuambia mashabiki wa izi timu wanataka ushindi tu......hayo mengine hayawahusu
 
Labda unisaidie kitu kimoja, juzi MO alinukuliwa akisema kwamba thamani ya hisa zitakazo uzwa kwa wanachama wa simba ni sh mil 400 kwa hisa 1%, so kwa logic yako hapo juu fedha za mauzo ya hizo hisa zinatofauti gani na b 20 za Mo kwenye uwekezaji kwa Simba sc?
Mo aliahidi kwa kinywa chake atatoa bill 20 ikaweka kwenye mkataba, Leo anaambiwa atimize takwa la kimkataba anakua mbogo, alafu Cha ajabu mashabiki Kama wewe wamesha shahau tukio la 2017 ajabu sana
 
Labda unisaidie kitu kimoja, juzi MO alinukuliwa akisema kwamba thamani ya hisa zitakazo uzwa kwa wanachama wa simba ni sh mil 400 kwa hisa 1%, so kwa logic yako hapo juu fedha za mauzo ya hizo hisa zinatofauti gani na b 20 za Mo kwenye uwekezaji kwa Simba sc?
Landa unifahamishe, Simba SC kabla ya kutaka kugawa hisa zake kwa kuuza, ilikuwa inamilikiwa na nani?
 
Eti thank you for guidance on simbas development Pique ndo mtoa guidance hahahaha jamaa anawajulia sana hawa mambumbumbu yaaani kila akiambiwa atoe bil 20 yeye anakuja na kituko
 
Eti thank you for guidance on simbas development Pique ndo mtoa guidance hahahaha jamaa anawajulia sana hawa mambumbumbu yaaani kila akiambiwa atoe bil 20 yeye anakuja na kituko
Ni Msanii sana, balaa aongee na kina Daniel levy, au Ed Woodward unaongea na pique ambaye ana zero knowledge kwenye management jamaa ni mjanja mjanja sana
 
Back
Top Bottom