Mo Dewji press: Hakuna anayependa kudharauliwa

beny jr

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
822
1,133
Habari wanajamvi tukiwa tunaendelea na kujikinga na gonjwa la covid wimbi la tatu ni bora kukumbushana kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka na kutumia sanitizer na hakika hili wimbi la tatu tutalishinda kama yale mawili yaliyotangulia.

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja jana nimefuatilia press ya billionea kijana barani Africa Mohammed kulamali Dewji kama nitakua sijakosea kuandika jina kuna jambo moja nimejifunza ambalo hata uwe umezaliwa kwenye familia yenye kipato ila kudharauliwa kwa kigezo huna kipato kinaumiza sana mo anasema alikua anaumia watu wanavyosema hana iyo pesa billion ishirini hili jambo nilijua hutokea kwa maskini baada ya kupata ndio hua na hii jeuri kumbe hata waliotoka familia yenye kipato kikubwa huwa wanaumia kwanini naadika haya?

Takriban wiki tatu staa wa muziki barani Africa kutoka kwenye familia yenye ufukara mkubwa Diamond Platnumz baada ya minong'ono mingi kutoka kwa wapinzani wake kuwa hana pesa ya kununua gari ya kifahari Rolls Royce aliweza kukata ngebe za watu kwa kushusha gari mpyaaa hiyo ya kifahari naomba wapinzani wa mtoto wa tandale wasione kama diamond limbukeni ni hali inawatokea hata matajiri nawasilisha

Kapuku mwenzangu ukiambiwa huna uwezo wa kununua iphone 12 huwa unareact vipi?

Nauchukia sana umaskini tufanye kazi Mungu atafungua milango ya fedha na kuwa kama moo dwj au diamond tukidharauliwa tunafanya kweli kuwazima watesi wetu
 
Habari wanajamvi tukiwa tunaendelea na kujikinga na gonjwa la covid wimbi la tatu i bora kukumbushana kuvaa barakoa,kunawa mikono kwa maji tiririka na kutumia sanitizer..na hakika hili wimbi la tatu tutalishinda kama yale mawili yaliyotangulia
.
.
.
Naomba niende kwenye mada moja kwa moja jana nimefuatilia press ya billionea kijana barani africa mohammed kulamali dowji kama ntakua sijakosea kuandika jina kuna jambo moja nimejifunza ambalo hata uwe umezaliwa kwenye familia yenye kipato ila kudharauliwa kwa kigezo huna kipato kinaumiza sana mo anasema alikua anaumia watu wanavyosema hana iyo pesa billion ishirini hili jambo nilijua hutokea kwa maskini baada ya kupata ndio hua na hii jeuri kumbe hata waliotoka familia yenye kipato kikubwa huwa wanaumia kwanini naadika haya?
.
.
.
Takriban wiki tatu staa wa muziki baran africa kutoka kwenye familia yenye ufukara mkubwa diamond platnumz baada ya minong'ono mingi kutoka kwa wapinzani wake kuwa hana pesa ya kununua gari ya kifahari rolloyce aliweza kukata ngebe za watu kwa kushusha gari mpyaaa hiyo ya kifahari naomba wapinzani wa mtoto wa tandale wasione kama diamond limbukeni ni hali inawatokea hata matajiri nawasilish
.
.
Kapuku mwenzangu ukiambiwa huna uwezo wa kununua iphone 12 huwa unareact vipi?
.
.
Nauchukia sana umaskini tufanye kazi Mungu atafungua milango ya fedha na kuwa kama moo dwj au diamond tukidharauliwa tunafanya kweli kuwazima watesi wetu
Unaweza ukawa una hoja lakini umeandika kindezi sana. Hebu soma na hariri huo uzi wako. Umeandika kama unakunywa chang'aa. Hata jina la MO Dewji ulivyoliandika halieleweki.
 
Umaskini siupendi.....kuna ndezi m1 ananiambia sitoweza kufanya kitu flani Ngoja nimuoneshee......"Heiraaaz"(haters)hawaishi maneno na ndio wanaotupa hamasa
 
muwe mnakuja na mada za utu uziima sio mada unayoleta ya boarding school pumbavu
 
Back
Top Bottom