Mo Dewji awa billionea wa 13 Afrika, kumwaga ajira laki moja, amshukuru Rais Magufuli

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
3,868
2,000
Mfanyabiashara kutoka Tanzania Mohammed Dewji ametangazwa kuwa anashika nafasi ya 13 kwa utajiri barani Afrika.! Mfanyabiashara huyo baada ya kupata habari hizo amekimbilia kumshukuru rais Magufuli kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji hapa nchini na kupelekea uwekezaji na utajiri wake kuongezeka maradufu kwa miaka mitano iliyopita..
Ili kuendelea kuunga mkono juhudi za rais Magufuli katika kuwaletea maendeleo watanzania, Mo Dewji ameahidi kumwaga ajira 100,000 kwa watanzania kuanzia mwaka huu 2021.

My take.
Hii ina maana gani kwa chadema wanaokesha wakipinga kila kitu kinachofanywa na rais Magufuli?
IMG_20210124_201911.jpg
 

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
10,271
2,000
Ulipokosea ni hapo ulipoanza kuleta siasa.Nimeupuuza uzi huu kwasababu muda wa kampeni ulishaisha.Lkn Mo simpuuzi naheshimu Mchango wake.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
52,692
2,000
Analipaje kiwango cha mshahara watanzania ?
Hebu tuweke itapendeza sana

Ova
 

kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
932
1,000
Huyu Mo Mungu aendelee kumfariji maana faida za uwekezaji wake ni nyingi saaaana. Chukulia Hii Simba Super Cup inayokuja itawapa ajira wajasilia mali wangapi? Mfikirie Muuza maji, mfikirie muuza njugu kipindi michuano inaendelea, Embu wafikirie wenye Daladala watakaoleta mashabiki pale kwa Mkapa..! Mungu ampe yeye na Familia yake Afya njema..!
 

holy holm

JF-Expert Member
May 6, 2017
2,764
2,000
Ajira laki moja? ckuiz kupata kazi kiwandan mpk uwe na koneksheni bila ivyo utasota.
Kingine ni mshahara wa laki mpk laki na nusu kazi zenyenyewe ni za suruba anyway tungoje tuone.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom