Mnyukano wa Kikubwa kati ya USA vs. China nani ataibuka mshindi ( Trump vs. Xi Jinping)

chipa GM

JF-Expert Member
Jan 21, 2012
1,769
2,858
USA alianza kufanya figisu za kibiashara kwa bidhaa za china kwa kuweka kodi kubwa bidhaa km steel, electronics pamoja na kupiga propanganda na marufuku kwa simu za huawei Nchni USA. Wachina nao wamejibu bidhaa aina 168 zimeongezwa kodi kwa 25% zikiwemo bidhaa kilimo, nyama hasa hasa kitimoto. USA wanaamini China kapiga hatua za kimaendeleo kwa sababu ya kupata access a kuuza USA.. Mchina anasema yupo teyari kurudi kwenye negotiations na USA but wakimwaga ugali watazifurusha kampuni za usa zilizo invest China. Binafsi naona wote wataloose kwenye vita hii..Mchina anajidai kwa population ya 1.3 billions na majority wakiwa kipato cha kati binafsi usa wanahtaji soko la china.. Usa wana population zaidi ya 300mil na majority wakiwa kipato cha kati na kikubwa..Mchina analitaka soko hili. Wakubwa wanapambana vita ya kiuchumi...Hatari sana..Madogo tushike jembe tukalime. Mgogoro huu pia najua unachangiwa sana na Korea Peninsula. Waziri wa Fedha wa Canada ameshaingia viunga vya Beijing kuona ni jinsi gani wanapush biashara na mchina. Canada wanataka waibebe fursa ya hiyo nimemsikia waziri anabisha changamoto ya Canada hakuna spenders km usa kwanza hata population yao ndogo sana km Australia tu around 36 Milions.

Vita hii now kubwa sana. Mataifa makubwa yameshaona yanatumika na usa kwa manufaa ya usa pekee. Kasi ya maendeleo ya china imemtisha usa.tukubali au tukatae USA now amekuwa km mbwa koko duniani siyo marekani yule..hana influence tena duniani km zamani. Siku hizi unaweza ona hata vitaifa vidogo vikaenda against naye rejea suala la jerusalem. hata sisi tulisema No for USA..Ushawishi wa USA ndani ya Jumuiya ya Ulaya umepungua sana na hii inatokana na U.K ambaye mshirika mkuu wa USA kujitoa ndani ya Ulaya. USA kujitoa kwenye Paris agreement nayo iliwaudhi sana wa Paris na sidhani km Rais kijana wa Paris(france) anazielewa sera za Trump. U.K kujitoa ulaya ni mkakati wa U.k kuwa na wafuasi wake na yeye. Return ya british great again. Ulaya wameshtuka zaidi ya miongo mitano USA imekuwa ikiwatumia kwa manufaa yake tu.. Na chini ya kapeti U.K wanaanzisha uhusiano wa kibiashara na CHINA (bilateral). Nilisoma gazeti moja, USA now wanalalamika China kaichukua influence yao Africa..Na hiyo ni kweli, Viongoz wa Africa wanampenda mchina kwakuwa hawaangilii masuala ya ndani hasa ya politics na human rights not like USA. Na of-course ili uwe great nation lazma uitawale Africa tu..huku ndiyo sehemu ambayo unaweza ukapata rasilimali ka bei ya cheee. Mchina lazma aje tu sana. Mchina anachimba mafuta South Sudan na hiyo ya vita ya yenyewe kwa yenyewe haitoisha mpka kaka mkubwa (USA) apate na yeye sehemu ya kuchimba..la sivyo.. hapata tulia.

Vita kubwa kati ya Trump Rais mwenye roho ya kibepali na mfanya biashara jeuri asiye na miiko kwenye kusema Vs. XI Jinping Rais mpole usoni km JK but liJasusi km Putin. Hii ni vita kati ya mzungu na mvimba macho au kati ya white na red. Tushike majembe tukalime


Ukiangalia balance of trade (export - import) kati ya usa na china.. trade imbalance kwa usa. yaani usa ana imports in china than exports (https://www.census.gov/foreign-trade/balance/c5700.html)..kumbe USA alikuwa anapigwa 3 bila nyumbani.

Je vita hii ya kiuchumi Africa tunajifunza nini..au bado tunaomba Mungu atuletee mvua wakati ametupa akili ya kutengeneza mvua/ kupanda miti.
 
Mwisho wa ujambazi wa China umefika. Hivi inakuaje bidhaa ikiingia Marekani itozwe 2% Kodi halafu za Marekani zikiingia kwenye nchi hizo zinatozwa Hadi 15%-20%?!

Lazima heshima itawale ukitoza 20% na wewe kubali kutozwa 20%.
siyo kweli mkuu
 
Embu nenda kapitie Mikataba ya kibiashara ambayo Trump ameiondoa USA ukianza na ule wa TPP,uone ulivyo wa hovyo.

Wewe jiulize kwanini Marekani yenyewe haipigi kelele Ila wanaopiga kelele ni hao wengine.
Mbona China haipo Tpp mzee
 
Mzee population ya marekani ni ndogo ukilinganisha na china ila sio ndogo hivyo,ni 300m naaa.

Pia hao wote wanajua wanachokifanya,sie tuyajenge yetu.
Shida sio Population kubwa shida ni kwamba hiyo population yako ikoje kiuchumi?!

Marekani Raia wake wengi ni wa kipato Cha Kati hivyo kwenye kutumia wanatumia Sana kuliko yule mwenye population kubwa ambayo haina kitu.

Mfano Report ya hivi majuzi (ya Tanzania) inaeleza kwamba Kati ya watu 10 bhas 8 Ni tegemezi. Sasa hapo huwezi fananisha mfano labda na Botswana ambapo Ina Raia wachache lakini wapo vzuri kiuchumi
 
Mwisho wa ujambazi wa China umefika. Hivi inakuaje bidhaa ikiingia Marekani itozwe 2% Kodi halafu za Marekani zikiingia kwenye nchi hizo zinatozwa Hadi 15%-20%?!

Lazima heshima itawale ukitoza 20% na wewe kubali kutozwa 20%.
unaweza ukaweka uthibitisho wa hii..nafunua masource yangu siioni hiyo 2% Mkuu..may be umechanganya
 
Kiufupi China sio waumini wa Free Trade hivyo wasilete malalamiko wapambane na Hali zao.
 
Kuku akiwa anachinjwa hutapatapa sana, kinachomtokea USA sasa!..China ni next Super power in the World!..
China anaa maamuzi ya Soko la Dunia kwa sasa sawa na Marekani!..
 
Embu nenda kapitie Mikataba ya kibiashara ambayo Trump ameiondoa USA ukianza na ule wa TPP,uone ulivyo wa hovyo.

Wewe jiulize kwanini Marekani yenyewe haipigi kelele Ila wanaopiga kelele ni hao wengine.
Mwalimu gani kakufundisha uchumi wewe PIMBI
 
Wote ni wa moja hao kazi yao ni kuiadaa dunia, mrusi, North Korea, usa wote kwa ujumla lao ni moja !
 
Back
Top Bottom