Mnyukano ndani ya CCM ni vita ya 'kusikika na kusikilizwa' sio vita ya Urais 2020!

Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,373
6,756
Moja ya njia ambayo jeshi linapoteza ushindi kwenye vita, ni pale wanaposhindwa kuelewa aina ya vita wanayopigana au aina ya adui wanayepambana naye...
Vita, (sio vita per se! Huu ni mnyukano baina ya makundi madogo madogo ndani ya chama ambapo kila kundi likitaka kusikika.) Wengi walioandika juu ya mnyukano huu, kwa kiasi kikubwa wameupotosha. Mfano myukano wa Kinana na Makamba, haukua dhidi ya Rais bali dhidi ya Musiba ambaye kwa sasa ndiye ameonekana kupora haki ya kusikika. Baada ya Musiba kukwapua haki ya wanachama, haki ya kusikika na yeye kujifanya msemaji mkuu 'nje ya chama' na kuanza kurusha mishale kwa wanachama wengine huku akijificha nyuma ya mgongo wa mwanaharakati mwenye kumtetea Rais, basi lazima wanachama wapigane au wapingane naye huku wakidai haki yao ya kuisikika.
Ukifuatilia mazungumzo yaliyonaswa ya Makamba mkubwa na Kinana, wasi wasi wao mkubwa ilikuwa ni kuwa je wanaweza wakasikika kupitia waraka wao? Unaona makamba mkubwa akiuliza Makamba mdogo kuwa je, magazeti yatachapisha waraka wao? Na pia unaona Kinana akimuuliza Nape huo waraka ukipelekwa kwenye media mida ya jioni, je utafanikiwa kuchapishwa? Their success was to be measured kwa ule waraka wao kuchapishwa na hivyo kuwapa haki ya kusikika, haki ambayo Musiba ameipora na kuifanya kuwa ni mali yake binafsi.
Ili upepo mwanana uweze kurejea ndani ya chama, ni lazima Musiba anyang'anywe haki hii ambayo ni mali ya wanachama wote. Pili watu wote wazee kwa vijana wanapoongea mitazamo yao kuhusu mambo ya siasa za chama na serikali, wasichukuliwe kuwa ni wanaharakati ndani ya chama wenye lengo la kumkwamisha Rais, bali wachukuliwe kama wanachama wanaotumia haki yao ya kikatiba, haki ya kusikika na kusikilizwa...
Mwisho wa siku nawaombea wote amani ya Bwana iwatawale na tuwe na utulivu huku kila mmoja akijipanga kimya kimya kwa ajili ya kinyang'anyiro cha uchaguzi wa serikali za mitaa na baadaye serikali kuu mnamo 2020!
 
Back
Top Bottom