You need to go and see optician.
I am an optician!
You need to go and see optician.
Quote:
Mwakyusa:Natafakari ushauri wa kujiuzulu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, amesema ushauri wa kutakiwa kujiuzulu kufuatia matatizo yaliyojitokeza ya watoto kuzirai baada ya kupewa dawa za chanjo ya kichocho na minyoo, amelipokea, lakini bado anautafakari.
Ni kawaida hata kwenye msafara wa mamba na makenge huwa wamo ndani yake. Lete hoja na si vinginevyo.
Nadhani sasa umepoteza dira, wewe umedai kuwa mimi ni mwanachama wa chama cha mafisadi. Nimekufahamisha kuwa hoja yako umeijenga kutokana na hisia kwani hunifahamu na huna ushahidi kwamba mimi ni mwanachama wa chama cha mafisadi. Zaidi ya hapo nikakueleza kuwa sijawahi kukisikia chama kinachoitwa chama cha mafisadi, sasa unataka nikueleze kitu gani ambacho mimi sikifahamu? Samahani kwa kutengua ubashiri na hisia zako kuwa ni za kufikirika na zisizokuwa na ukweli wowote. Please lete hoja za kweli na siyo za kupandikiza.
We punda
Kama unaona JK ni smart na intelligent kwa haya aliyoyafanya, basi Tanzania haina viihiyo wala mataahira.
Sasa kafanya nini kizuri katika EPA! Kusema kakamata passport wakati watu wanasafiri bado!!!! Wanasafiria za bandia au? Kakufurahisha wapi wewe wakati anashughulikia suala la jinai kama vile la madai!!!!!!! Ikifika November akawapeleka mahakamani wahusika kwa kesi ya madai kutakuwa na tofauti gani na kesi za akina manji na mengi, au mengi na ze comedy, au mtikila na wengineo wanaodaiana mabilioni huko mahakamani!!!!! Zuri liko wapi sasa! Yaani, umetumwa-umetumwa na kama hujatumwa basi wewe ni jamii ya akina Kigunge!
grrr yani nyumbani kwako watoto wamevaa nguo zimechanika,wana njaa na nyumba ni mbavu za mbwa,hali ya hapo inatisha na kila siku unacheka cheka unawaambia msihofu eeeh nipeni muda mambo yatakuwa mazuri. Ukienda kujiweni unasema aah kwangu mambo mazuri sanaaa, basi kijiwe kizima kinakusifu aisee we kiboko wa kutunza familia. Jirani yako ilhali akijua kabisa wanao wana njaa na nyumba yavuja anaenda nae kujiweni kusema aisee mzee wa jirani mambo yake safi?
does it even click on ones mind hali yetu ilivyo,shillingi yaendelea kuanguka,mafuta juu, rushwa ya viongozi juu, wezi wanafichwa. Hivi kuna asieona? wakati mwingine nahisi akili zetu hazina akili basi.Au tukiona tope tunaona ni chocolate cake?
What a wastage of resources and time kufanya maandamano kuunga mkono hotuba? hata kijana wangu wa form 1 aliuliza mbona sisi wajinga?
Nashindwa kabisaa kuelewa nini hasa kilikuwa special kwenye ile hotuba? eti kafanyaje?ooh punda just spare my breath, u know very well whats cooking? you know very well the money revolves among them, huyo huyo anayetangaza nawapa hadi novemba knows exactly kuna nini? tusipende kupotosha umma,amehandle vema wakati ukata wa maisha unazidi.
kweli tunahitaji uamko wa fikra otherwise tupo kama brainwashed vile.
Nasikia hotuba ya KIKWETE ina makosa na hivyo inabidi irekebishwe. Sasa hata haya ya EPA unaweza kukuta yanamakosa. Wanaokaa na kusifu kazi ya Kikwete kwa hili wakati HOTUBA INAMAKOSA, wanafikiria sawasawa?
Duuu, nilifikiri PUNDAMILIA SI PUNDA.
NB: Niongozeni kwenye listi ya watu wanaoona Muungwana hajafanya kitu na EPA.
CCM inatembeza U-SODOMA, inatulaaa!!! Mafisadi na Wawekezaji nao kwa sana tu.
I am an optician!
Hivi IMF wana msaada gani tanzania kazi yao ni kumonitor monetary systems na hawatupi hata senti moja hela zilizoibiwa sio zao. Lets wait for the real donors and see what they will say to their tax payer.
Mimi huwa situmwi, ninajituma na niko huru kutoa mawazo yangu kwa yale ambayo ninaamini kuwa ni sahihi na nitaendelea kusimamia mawazo ambayo ni sahihi wakati wote.
Hata kama ningekuwa na tofauti zozote na Kikwete kama rais au vinginevyo, hainizuii hata kidogo kusema kuwa 'hapa Mh. Rais amefanya kazi nzuri'. Hili ninaweza kumpongeza mtu yeyote, sina uchoyo inda wala wivu. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Tuko pamoja kichuguu. Si hotuba wala maamuzi ya Prezda yanaonesha usiriazi katika kushughulikia mafisadi wa epa.
pundamilia,
Pundamilia, pamoja na kwamba umeniita kenge kwenye kundi la mamba, ndiyo nakubali. Lakini wewe unayempa sifa huyo Raisi nikuite nini na kwenye kundi la nani. Nafikiri jibu ni rahisi na ninakuachia hilo jibu ulitafute wewe mwenyewe. Toka umetoa mada yako, nathubutu kusema umeona wananchi wazalendo walivyokushukia kama linyundo la chuma. Jiunge nasi tuikomboe nchi.
Hata siku moja siwezi kupoteza dira. Sichangii chochote hapa kwa kumchukia mtu yeyote yule bali nachukia sana viongozi ambao wanaiangamaiza Tanzania kwa kufanya maamuzi mbali mbali ambayo hayana maslahi na Tanzania. Hakuna hoja ya kupandikiza hapa. Unaishi nchi ya kusadikia ndiyo maana hujasikia chama kinachoitwa chama cha mafisadi, vingineyo ungekuwa unafahamu chama cha mafisadi ni chama kipi. Nimetoa na data za kuonyesha kwamba huyo njemba unayemsifia si lolote si chochote wewe unasifia kama kipofu tu na kuimba kama kasuku hata ukiulizwa maana ya wimbo unaouimba hujui maana yake. Nitakuwekea tena data hizo ili kukuonyesha kwamba siandiki mambo ambayo siwezi kuyathibitisha kama ulivyo wewe na kuimba nyimbo kama kasuku. Zipitie tena data hapo chini halafu ujaribu kuzijadili moja baada ya nyingine.
1. Ahadi za kupitia mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania zilikuwa nyingi mno wakati wa kampeni, kilichofanyika hadi hii leo unakijua au kwa kukumbusha tu ni sifuri, zero, ZILCH.
2.Ahadi za maisha bora kwa kila Mtanzania hakuna chochote, bali tunachokiona ni ahadi za maisha bora kwa kila fisadi.
3. Fisadi Mkapa kakupua Kiwira mchana kweupe mgodi ambao unathamani ya shilingi bilioni 4. Amejiuzia kwa shilingi milioni 700, lakini kalipa shilingi 70 milioni tu. Juhudi zetu Watanzania kuhakikisha mgodi huu unarudishwa chini ya miliki ya Watanzania hadi hivi sasa zimegonga ukuta. "Viongozi" wanajifanya kama hawaelewi yale tunayoyazungumza.
4. Ahadi za ari mpya, nguvu na kazi mpya hatuoni chochote bali midebwedo tu kila kukicha, usanii na uVDG.
5. Ufisadi wa rada, mpaka leo hii Watanzania tuko gizani kuhusiana na pesa zetu shilingi bilioni 12 walizolipana mafisadi katika ununuzi wa rada hiyo akiwemo mzee wa vijisenti aliyekuwa na vijisenti katika bank account ya nje ya nchi.
6. Kwa kifupi hakuna chochote kilichofanywa ambacho kinamhamasisha Mtanzania yeyote yule mwenye mapenzi ya kweli na Tanzania kumpigia kura JK, lakini kwenye chama cha mafisadi bado huyu ni mwenzenu anayestahili kuchaguliwa tena 2010 na si ajabu hata kubadilisha katiba ili aendelee kuwepo madarakani mpaka 2025!!! Halafu mnadai mna mapenzi ya kweli na Tanzania pamoja na kuona nchi inaangamia!!!!! kumbe mnatumia madaraka yenu kujitajirisha na kuwalinda mafisadi wenzenu!!!!
Pundamilia said:Na nimepewa miwani
In fact sioni wapi pa kubadilisha pamoja na maelezo yako marefu ndiyo umezidi kuharibu na kuonesha kwa kiasi gani umepoteza mwelekeo. Tafuta mtu atayeweza ku-refresh your mind.