G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,595
- 36,015
Kwa kweli nakumbuka miaka kadhaa nyuma rais Kikwete enzi hizo alimwagia sana sifa rais mstaafu Benjamin William Mkapa kwa hatua yake ya kutumia fedha za walipa kodi yaani fedha za ndani kujenga daraja la mto Rufiji.
Mwisho wa yote kwa heshima aliyoionyesha Mkapa, rais Kikwete akaamuru daraja hilo liitwe "daraja la Mkapa" na hadi leo ndiyo jina lake. Huko ndiko kujengeana heshima na kithaminiana!!
Ukweli lazima usemwe, hata kama mtu kafanya madudu kuna mambo ambayo kayafanya yatakayo mfanya apewe sifa na kukumbukwa kila mara! Daraja la Kigamboni lilikuwa icon muhimu sana ya rais mstaafu Kikwete. Kikwete ndiye aliyesema daraja lijengwe na likajengwa hiyo ndiyo kumbukumbu yake muhimu kama rais wa wakati huo. Angekataa daraja lisingekuwa limejengwa!
Nilitegemea rais Magufuli angerudia kile ambacho mtangulizi wake alikifanya miaka kadhaa iliyopita lakini imekuwa kinyume.
Mimi naelewa hata Kikwete kwa asilimia kubwa alitegemea kuwa daraja lingepewa jina lake! Mambo yamekuwa kinyume na daraja limebatizwa jina la Nyerere. Hii nchi sasa kila eneo ni jina la Nyerere ah! too much!
Ngoja nijiulize; ina maana Ngosha hataki kabisa kulisikia jina la yule? Labda! Maana yanasemwa sana!!