Mnyonge atanyongwa na haki yake hapewi vilevile

Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
8,226
7,999
Habari...

Makato katika mshahara wangu wa sasa ni zaidi ya asilimia 25% ya mshahara wote, hapa ni kabla ya makato ya bodi ambayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni. Kwa hiyo kama na hayo yakiingizwa makato ya jumla yanaweza kufika au hata kuzidi asilimia 35%.

Mbali na PAYE ambayo wananikata hapo juu, naingizia Serikali hela kila siku kupitia matumizi au manunuzi yangu ya kila siku kupitia VAT ambayo ni kama 18% hivi. Sio mbaya uzalendo siyo?

Nikienda kupata huduma sasaaa daaaah sihesabiki kama nililipa hayo yote hapo juu, hata kama ni hospitali za selikali kwa mfano nitatakiwa kulipa, pamoja na kulipa bado huduma zao khaaaaa! Unaona bora tu ujikatae ukahudumiwe kwenye vituo binafsi.

Poa, basi nimeshafanya kazi sana na sasa nahitaji kujiajiri ili nipige hatua zaidi. Mtaji nategemea nichukue mafao yangu toka katika mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ilikuwa inachukua hela yangu bila ridhaa yangu na kukaa nayo pasipo kufaidika lolote. Nikifika naambiwa nisubiri miezi sita, nayo ikiisha inaanza miwili ya uchunguzi wajiridhishe kama kweli nimeacha kazi, miwezi miwili, kweli>

Naamini haya ni machache kati ya ambayo vijana wengi tunakabiliana nayo......ni jinsi ambavyo TUNANYONGWA kwa uchache tu.

Kwa inshu kama hizi najua jamaa watahitaji askari na wanajeshi wengi zaidi katika uteuzi wao ujao, na hapa ndipo HAKI za wanyonge zitapokwa na kukamilisha mzunguko.

Niliamua tu kuandka ninachohisi.
 
Back
Top Bottom