kwa hiyo nafasi ya uwakilishi mbunge wa CUF(kura275) amembwaga vibaya mbunge wa chadema(kura47)........?
poleni...subirini nafasi nyingine labda mtapata...!
Mh Sophia Simba si angejieleza tuu kwa kiswahili kwani Kiingereza siyo lugha yetu badala ya kutumia mbinu ya kupita bila kupingwa
Kuhusu jambo hili vifungu vya kanuni vinasema hivi:
5: (1):
Katika kutekeleza majukumu yake yaliyotajwa katika Ibara ya 84 ya Katiba, Spika ataongozwa na Kanuni hizi na pale ambapo Kanuni hazikutoa mwongozo, basi Spika atafanya kazi kwa kuzingatia Katiba, Sheria nyingine za nchi, Kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya awali ya Maspika wa Bunge pamoja na mila na desturi za Mabunge mengine yenye utaratibu wa kibunge unaofanana na
utaratibu wa Bunge la Tanzania.
5: (2):
Spika atawajibika kutilia nguvu Kanuni zote za Bunge, na Mbunge yeyote anaweza kusimama mahali pake na kumwarifu Spika kuwa Mbunge fulani amekiuka Kanuni.
5: (3):
Spika anaweza kumtaka Mbunge yeyote anayekiuka Kanuni hizi kujirekebisha mara moja.
5: (4):
Mbunge yeyote ambaye hataridhika na uamuzi wa Spika anaweza kuwasilisha sababu za kutokuridhika kwake kwa Katibu wa Bunge ambaye atawasilisha malalamiko hayo kwa Spika.
5: (5):
Spika atawajibika kuitisha kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge na kulijulisha Bunge kuhusu uamuzi utakaotolewa na Kamati hiyo.
5: (6):
Spika au Naibu Spika hatakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge inapokaa kujadili uamuzi unaolalamikiwa, bali wajumbe watachagua Mwenyekiti wa muda kwa asilimia 50 ya kura za siri.
Tuzichambue.